Friday, October 22, 2021

HUDUMA YA UIMBAJI NDANI YA KANISA

Mwalimu: Musa (Moses) Zephania Mgema
Ijumaa tarehe 22/10/2021
FPCT -Singida town centre church.
Uimbaji ni nini ?
Ni sanaa ambayo inatumika kuwasilisha ujumbe kwa njia ya lahani (chord) na mpangilio wa sauti wenye kutengeneza ladha yenye mvuto kusikiliza.
➡️Uimbaji asili yake ni mbinguni. Huduma hii ilianzia mbinguni na kiongozi wa huduma hii huko mbinguni alikuwa anaitwa lusifa kabla ya kuasi.
Ezekieli 28:13-15
➡️Huduma ya uimbaji ni moja kati ya huduma muhimu ndani ya kanisa kwa sababu imefanyika chumvi nzuri kwa ustawi wa kanisa na hata huduma nje ya kanisa.
Uimbaji katika mfumo wa injili kwa maana ya nyimbo za kiroho sio burudani bali ni huduma nyeti na ya msingi wala sio burudani au huduma ya ziada ndani ya kanisa.
➡️Huduma ya uimbaji ni huduma ambayo haina mwisho maana hata baada ya unyakuo kazi pekee tutakayoifanya huko mbinguni ni kuimba tu.
Ufunuo 5:9-10
Ufunuo 15:2-4
➡️Hapa duniani kazi ya uimbaji ilianza muda mrefu tangu enzi za agano la kale ni hii ni mara tu baada ya kuumbwa kwa Adamu na Hawa.
Mwanzo 4:21

KWA NINI HUDUMA YA UIMBAJI NDANI YA KANISA.
1petro 4:10-11
1Nyakati 6:31-32
1. Huduma ya uimbaji ikitumika vyema kwa kuongozwa na Roho mtakatifu, maombi na Neno la Mungu huleta mavuno mapya ndani ya kanisa.
2. Hufanya moyo wenye huzuni kupata furaha na Amani.
3. Hubadili moyo mgumu kuwa laini 
      1samweli 16:23
4. Mtu dhaifu hutiwa nguvu na uzima 
     1samweli 18:6-9
5. Hudhihilisha uwepo wa Mungu.
      2Nyakati 20:21-22
     2Falme 3:15-16
     Matendo 16:25-26
HUDUMA INAYOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU, MAOMBI PAMOJA NA NENO LA MUNGU-
1.  Huonya na kufundisha kolosai 3:16
2.  Ni mahubiri kamili  Isaya 48:20
3.  Huleta faraja kwa waliokosa tumaini.
4. Humsifu na kumshukuru Mungu kwa matendo makuu 
Nb:
Zipo pia nyimbo za upuuzi kama ambavyo 
 Amosi 6:5 anaonyesha.
➡️Kama mtumishi wa Mungu unaetumika kwa njia ya uimbaji ni muhimu haya yafuatayo kuwa sehemu ya wimbo unaohudumia watu
1. Roho mtakatifu kuhusika
2. Neno la Mungu kujaa kwa wingi ndani ya mwimbaji.
3. Kufanya maandalizi kabla ya huduma kwa maana ya kuomba, kusoma neno na kuruhusu Roho mtakatifu kukuongoza ili kufanya huduma yenye connection ya mbingu na wewe kama mhdumu.
➡️Huduma ikiwa na uongozi wa Mungu lazima iwe ni ibada kamili ambayo itadhihilisha matendo makuu ya Mungu, mfano uponyaji, Faraja, nk.

➡️Tunaweza kujifunza kupitia wimbo alio imba Musa mtumishi wa Mungu na Israel baada ya kuwashinda wamisri.
 Ufunuo 15:3
➡️Ulikuwa wimbo wa matendo makuu ya Mungu
Aina nyingine ya nyimbo ni nyimbo ya mwanakondoo (Wimbo mpya) ambao unaelezea namna Yesu anavyostahili kuabudiwa, kupewa sifa kwa matendo makuu ambayo ametenda kupitia msalaba.
Zaburi 40:1-3
Ufunuo 14:1-3
Ufunuo 15:5-9
Wimbo ukitungwa kwa uongozi wa Mungu mwenyewe huwa ni wimbo wenye nguvu na huleta matokeo kusudiwa.
Ukiona waimbaji/mwimbaji anaimba na wala hakuna connection ya Kimungu, hiyo ni ibada ya sanamu ambayo imebeba kujiburudisha nafsi na ni makelele mbele za Mungu.
➡️Mwimbaji lazima ajawe na Roho mtakatifu kwa wingi ndani yake, Neno la Mungu na awe mtu ambae anaiombea huduma yake kwa kujitoa ili kuwa na huduma bora na yenye nguvu za Mungu.
➡️Ipo mifano ya huduma za uimbaji katika agano jipya na agano la kale ambavyo Mungu alohudumia watu kupitia waimbaji 
Luka 1:41&67
Efeso 5:18-20.
Kwa ufupi uimbaji ni kazi ya Roho mt. nje ya Roho mt.  uimbaji unabaki kuwa burudani tu, maana ni ngumu sana kuyaona matendo ya Mungu yakidhihilika.
➡️Uimbaji ukiwa na uongozi wa Mungu hiki tegemea kukiona kwa ukubwa katika huduma yalo ya uimbaji  2Nyakati 5:13-15
Neno la Mungu ni huduma kamili ya uimbaji hivyo kwa sababu neno ni chanzo cha ujumbe na mafunuo mengine ya kimungu lazima mwimbaji awe amejaa neno ndani yake, hii husaidia kuwa na huduma yenye matokeo.
Zaburi 45:1
Wakolosai 3:16
Mwisho.
Msingi wa huduma yeyote ya kimungu lazima iongozwe na 1. Neno la Mungu
                       2. Roho mtakatifu
                       3. Maombi na utii wa Mungu.
Ukiwa na hivi vyote lazima uwe na huduma ya nguvu za Mungu ndani yake
Mungu akubariki sana kwa kunisikiliza
0715366003 whatsup
0755632375 call and sms
mgemamoses@gmail.com




4 comments:

  1. Mungu akubariki sana mtumishi, nimebarikiwa sana na ujumbe huu.

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe Mtumishi kwa Somo zuri, binafsi nmejifunza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu akubariki sana pia kwa kunitia moyo kwamba umepata kitu

      Delete