Sunday, April 14, 2019

MAARIFA KWENYE KARNE YA 21 NI MSINGI WA MAFANIKIO YAKO

Nimekuwa na muda mzuri sana wa kujifunza kila siku, na hayo yamekuwa ni maisha yangu sasa, na kupitia aina hii ya maisha nimejikuta binafsi nikipata nguvu na imani kwamba kwa kila jambo lina sababu ya kuwa mahali popote lilipo.
Kujifunza kama ambavyo waandishi wamekuwa wakiandika nami naungana nao kwa kusema: Kujifunza ni mchakato endelevu kwa yeyote ambae anaendelea kuishi.
Na tunajifunza kupitia mazingira yanayotuzunguka na Yale mapya tunayokutana nayo kila muda tunaopata tukitoka nje ya maeneo yetu tuliyoyazoea.

Kupitia kujifunza huku, tunawezesha akili zetu kushiba na kuwa na afya ya maarifa ambayo kwa namna moja ama nyingine maarifa hayo yakitumika vyema ndiyo yanayoweza kubadilisha mfumo mzima wa maisha ya mtu kutoka vile alivyo, namna anavyotazama, fikiria, kiwango cha kuamini kuwa alipo yawezekana si mahali pake lakini pia kupitia maarifa anaweza gundua kuwa ndani yake kuna uwezo wa ajabu kiasi kwamba akiamua kuutumia vyema unaweza kumpeleka mbali zaidi maishani.

Niliwahi kusikia msemo maarufu nchini Tanzania kuwa: " UKITAKA KUMFICHA JAMBO MTANZANIA BASI WEKA KWENYE MAANDISHI UTAKUWA UMEMALIZA KILA KITU" maneno haya sio mazuri sana kwa sababu yanajaribu kuelezea udhaifu wa watanzania wengi kuwa hatupendi kujifunza kwa Uhuru labda kwa shuruti kama inavyofanyika kwenye mfumo rasmi wa Taaluma ambao ni haki ya kila mtanzania kupata elimu hiyo.

Lakini kwa mtu ambae amekubali kuyafanya maisha yake kuwa ni yakujifunza kila muda, mtu wa namna hii huwa anakuwa na nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya mambo yake kwa sababu

1. Maarifa hujenga uwezo wa kufanya mambo kwa ufasaha hasa kwenye eneo husika.
2. Maarifa hujenga imani na kujiamini.
3. Maarifa huvumbua fursa zilizojificha.
4. Hujenga uwezo wa kufikiri zaidi.
5 unaufanya ufahamu wa MTU kuwa updated muda wote na active
6. Kujua mahitaji ya wakati uliopo na kuweza kuitabili kesho.
Hizi ni baadhi ya faida ambazo mtu anaweza kuzipata kama tu amedhamiria toka ndani kuwa maisha ya kujifunza yawe ni maisha yake.

Niliwahi kusoma kitabu kimoja hivi kilichoandikwa na Brian Trace kinaitwa "NO EXCUSES" niligundua mambo mengi sana ambayo yamechangia watu wengi kuishi maisha ambayo hayawastahili Kati ya mambo makuu niliyojifunza kupitia kitabu hicho ambacho pia kilibadili kabisa mtazamo wangu ni
1. Kuishi kweye sababu.
2. Kuamini mtu alipo ni kwa sababu ya mtu Fulani.
3. Kutokuwa na nidhamu binafsi nk.

Pamoja na kusoma kwa undani niligundua kuwa maisha ya mtu yapo ndani ya mtu mwenyewe bila kujali umekulia mazingira yapi as long as umeshakuwa mtu mzima na unaafya njema basi wewe ndiye utabaki kuwa mwamzi sahihi wa maisha yako au mwamzi wa maisha yangu.

Kufeli, kutokwenda shule, wazazi kutokuona umuhimu wa jambo Fulani yaani elimu nk, bado haiondoi uhalisia kwamba maisha ya mtu yako ndani ya maamzi yake mwenyewe.

Watu wengi tumekuwa wavivu sana kwa mambo mengi, kuwaza, kujitoa kuanzisha shughuli ndogodongo kama kuuza matunda, kuuza bidhaa zilizo na uwezo wa kuwa na mtaji mdogo badala yake tunawalalamika au kuwalalamikia wengine

Wengine wamepata nafasi ya kufanya kazi, kujiajiri kwa kazi zao lakini wamekosa nidhamu ya kazi yao, wanachelewa kwenda kazini, wanafanya kazi kana kwamba wamelazimishwa kufanya hivyo, hawana upendo na kile wanachokifanya mwisho wa siku ubora au ufanisi wa kazi umekuwa mdogo kitu kilichopelekea kupoteza ajira zao au hata biashara zao kufa.
Nidhamu mbovu juu ya vipato vyao kitu kinachopelekea mtu kuonekana ana kazi au biashara lakini hatua ya maendeleo iko pale pale kila mwaka unapopinduka ajabu sana.

Lakini kumbe chanzo cha haya yote ni ukosefu wa elimu na maarifa ya namna gani yakufanya ili kwa kila jambo ambalo mtu anafanya liweze kuwa endelevu na lenye kumfanya apige hatua ya maendeleo yake binafsi lakini pia familia.

Pamoja na kwamba ukisoma vitabu vingi sana hasa hizi inspirational books unaweza jikuta unaona ni kama umechelewa, au uone kumbe kufanikiwa ni rahisi, lakini kuna umuhimu wa kujifunza maana mazuri ni mengi kuliko mabaya kupitia elimu.

Tuwe ni watu wakujifunza, kupitia kujifunza utapata shuhuda za watu waliofanikiwa, utaongeza ujuzi na maarifa mapya juu ya kazi au biashara unayofanya na unaweza kuiboresha zaidi.

Utapata mbinu mpya za namna ya kufanya kazi zako lakini pia kama ni biashara unaweza gundua vitu vipya ambavyo kwenye mazingira yako havipo na wewe kuwa mwanzilishi wake.

Kwa hiyo kujifunza jambo nyeti na muhimu sana kwenye maisha yetu hasa kama unataka kufikia ndoto na malengo yako, tunafanikiwa kwa kuangailia wengine walifanya nini.
Elimu ina transform namna yakuwaza, kufikiri na namna ya kutenda.
Note.
Kusoma sana vitabu au kupata muda mwingi wa kujifunza na kuhudhuria semina za wajasirimali haimanishi kwamba ndiyo tiketi ya mafanikio hapana.
Kujifunza na kupata maarifa ni jambo moja lakini utekelezaji wa maarifa hayo ni jambo LA muhimu zaidi na hilo ndilo linaweza kuwa ndo msingi na ngao ya ushindi wa maarifa hayo.

Maarifa na ujuzi bila utekelezaji wake ni sawa na kukubaliana na msemo wa wahenga usemao, "PENYE MITI HAPANA WAJENZI"
JIFUNZE+ WEKA KWENYE UTEKELEZAJI = MAFANIKIO
Mungu ayape nguvu maono yako kwa nguvu unayoitumia kuhakikisha unafikia malengo yako.

Elimu ni mtaji wa kila jambo

Moses z. Mgema
0715366003/0755632376
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam, Tanzania

Tuesday, January 8, 2019

KWA KILA JAMBO ANZA, TEMBEA NA MALIZA NA MUNGU.

Pamoja na maarifa, ujuzi, elimu, shauku, uwezo mkubwa wa kufanya kazi, bidii ya kufanya kazi bila kuchoka.

Haitoshi kwenda pekee yako na kujitegemea mwenyewe au watu wanaokuzunguka.

Fedha na kila aina ya rasimali ulizonazo haziwezi kukubeba katika kila jambo.

Ufanyaje sasa ?
Kwa kila jambo tembea na Mungu, mshirikishe Mungu, mwache Mungu awe kiongozi kwa kila kazi yako.

Ukitembea na Mungu hakika huwezi kuona unaanguka kibiashara au katika kazi zako kwa sababu yeye atasimama na kupigana  na maadui wa kazi zako.

Ukiwa Mwaminifu kwa Mungu kwa kutoa fungu la kumi, hakika Mungu ataibariki kazi ya mikono yako.

Ukiwa mwaminifu kwa Mungu, Mungu atakutetea wakati wa ukame wako.

Kumbuka Biblia inasema yeye alikujua kabla ya misingi ya dunia kuumbwa, kwa hiyo hatima ya maisha yako iko mikononi mwake.

Kwa hiyo hata alipokuumba aliweka kusudi na maono yake ndani yako ili uyatimize kwa utukufu wake.

Kwa hiyo unapaswa kufahamu kuwa mafanikio yote, maarifa yote, ujuzi wote na utajiri ulio nao ni kwa sababu Mungu alipanga maono yake kupitia wewe, na amekupa uwezo wa kujua na kutambua uwezo wako na wewe kufanyia kazi, fahamu huyo ni Mungu.

Usikubali kutembea pekee yako mwaka huu tembea na Mungu hakika utaona matunda mazuri kwa sababu Mungu atakuwa na wewe.
Wakati mwingine biashara, kazi zetu hazisimami kisawasawa kwa sababu tujiona kuwa tunaweza bila Mungu.

Tumejitegemea sana sisi pasipokujua kuwa wakutegemewa pekee ni Mungu

Jiepushe na watu ambao wanaushauri mbaya kuhusu Mungu, acha kutegemea mwadamu, mfano kwenda kwa waganga, maana Biblia inasema kwamba amtegemeae mwanadam amelaaniwa kabisa.
Kwa hiyo kila mmoja lazima amtegemee Mungu kwa akili yake yote.
Pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni zote zinazotakiwa kwenye kanuni za kazi bado kanuni kubwa na yenye nguvu basi ni kumtegemea Mungu
Yeye ndiye anajua hatima ya maisha yako.
Msingi wa mambo yote mema ni Mungu tu.

Barikiwa kwa kusoma ujumbe huu mwanzoni kabisa kwa mwaka huu
Mwaka huu tembea Na Mungu
Acha kutembea pekee yako.

Moses zephania Mgema
0755632375.
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam Tanzania

*-2019 Is the year of achievements-*

Sunday, January 6, 2019

MAISHA YA YESU DUNIANI NI PAKITI KAMILI YA MAISHA HAPA DUNIANI.

Habari,
Natumaini kila mmoja watu amepata neema nyingine ya upendeleo kuifikia siku ya leo akiwa mzima wa afya.

Nitoe pole kwa yeyote ambae anapitia changamoto yoyote ambayo inamnyima furaha yake ya kila siku.

Niende moja kwa moja kwenye somo la kwanza la mwaka huu tangu kuanza, naamini utakuwa msingi mzuri wa kuunza mwaka huu baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Somo letu kama linaposomeka katika kichwa cha habari, basi tuambane ili kuweza kufahamu nini hasa tunajifunza, lengo na nini matokeo yake baada ya kujifunza.

Yesu au Mesia sio jina geni kwa watu wote, ni mtu ambae alikuwepo duniani kwa hali ya mwili na aliishi kati ya maisha ya kwaida kabisa. Yesu alizaliwa kwa hali ya kawaida na akaishi kwa uhalisia wote wa dunia.

Na ndiyo sababu iliyonifanya kuja na somo hili kama msingi wa kila mtu ambae, ana shauku ya kuona ndoto, malengo, nia na matamanio yake yanatimia siku moja.

Yesu alikuwa na malengo ya yeye kuwepo duniani, na lengo kuu lilikuwa kuleta ukombozi wa maisha ya kiroho lakini hata katika mwili, lakini lengo kuu ilikuwa kukomboa watu waliokuwa wamepotea.
Hiyo ndiyo ilikuwa main purpose ya Yesu kuwepo duniani.
Pamoja na yote hayo, mimi nimejaribu kutafuta na kufikiri zaidi juu ya ujio wa Yesu duniani.

kusudi kuu la yeye kuja duniani linafahamika kwa kila mtu, lakini je ni hilo pekee ? hilo ni swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza zaidi.

Naufahamu uwezo wake, nguvu zake, mamlaka yake, uwezo wa kuona kesho kabla ya siku kufika lakini kwa nini alikubali kuja kufa huku duniani, je hapakuwa na njia nyingine ya ukombozi?.
Jibu hapana Yesu anajia nyingi ambazo zingemfanya kuikomboa dunia bila yeye kupata maumivu na mateso.
Kuna zaidi ya shughuli za kiroho zilizomfanya yesu kuja duniani. Na kama dunia ingemwelewa vizuri au ingeelewa vyema sababu zingine  zilizomlazimu yesu kuja duniani basi huyu pekee ndo angekuwa Role model wa wote.

Yesu ni pakiti kamili (Full package) ameenea kila kona ya maisha ya binadamu, anaemkubali na hata asiemkubali ila kiuhalisia Yesu anagusa kila kona na pembe ya maisha yetu.

Yesu ni mwalimu, na alikuja kufundisha uhalisia wa maisha ya duniani.

NAMNA GANI TUNAJIFUNZA KWAKE.
Lesson 1.
Yesu aliamini katika kufanya kazi kwa  bidii sana na kwa muda mrefu sana huku akiwa na focus na nia ya kufikia kile ambacho amedhamilia kukitimiza kwa siku. Ndiyo maana unaweza kuona kwenye mkusanyiko wa wanaume 500 na wanawake na watoto alilazimika kufanya muujiza watu wapate msosi palepale ili ratiba yake ya siku itimie hata kama ni usiku wa manane.
 
> Hapa tunajifunza kufanya kazi kwa bidii sana lakini kuhakikisha kila ratiba unapopanga mambo ya kufanya kwa siku, wiki, mwezi na hata mwaka lazima uhakikishe unapambana kutimiza ratiba ili kuepuka viporo, bora kuchelewa kurudi nyumbani lakini ukiwa umetimiza majukumu ya ratiba yako.
Lesson 2
Alipata habari ya kuumwa kwa lazaro rafiki yake, lakini tayari alikuwa kwenye ratiba ya mambo mengine aliyokuwa anayatimiza, kwa hiyo alilazimika kumaliza kwanza kazi zilizokuwa ndani ya ratiba yake ndo akaenda alikokuwa ameitwa.
Jiulize swali.
Je ni mara ngapi rafiki yako amekuondoa kwenye ratiba yako ?
    Majibu unayo wewe

>Hapa anatufundisha kuwa usikubali mtu awae yeyote kukuharibia au kuingilia ratiba yako pasipo sababu, hata kama kuna sababu ipime uzito wake kama unaona unaweza kuisolve hata kwa wakati mwingine basi timiza kwanza ratiba uliyonayo ili kuondoa uwezekano wa kuloose focus na concentration.
Ukikubali kila mtu aingilie ratiba yako na wewe umtimizie haja yake, basi wewe ni ngumu sana kufikia malengo kwa wakati ambao ulitazamia kutimiza. Maana mtu asiyekwenda na ratiba huyo ni kama bendera.
Kuna wakati unapokea taarifa ngumu ni vyema kutulia na kuonesha ukomavu, ukifanya hivyo basi utaipa akili kupumua vyema, hata unapoamua kufanya maamzi basi unatakuwa na asilimia kubwa ya kuamua vyema.
Lesson 3
Kutimiza malengo yako kwa wakati sio rahisi usipokuwa, mkomavu na mwenye nia ya dhati.
> pamoja na uwezo alokuwa nao lakini kuna wakati alikiri wazi kwamba yasingekuwa mapenzi ya Mungu basi yeye angeomba kikombe kimwepuke.

Maana yake nini kwenye maisha yetu ya kupambania ndoto zetu, kuna wakati unaona mlima mkubwa, huoni kama utaweza, kila unalofanya ni gumu lakini bado unapaswa kusimama kupambana ili kuvuka hapo

Hakuna mafanikio au kutimiza ndoto kirahisi lazima utoke jasho kweli kweli, no way ya kuepuka jambo hili.

4. Yesu anatufundisha kuvumilia sana kuna wakati mambo hayaendi, changamoto, unajisikia kuchoka, kukata tamaa lakini  bado hata kama hayo yanakuja bado unapaswa kupambana hata mwisho utakapoona umetoboa.

5.katika kila jambo unalofanya, watu watakudhihaki, kukusaliti, majungu, kukusengengenya, utaanguka au kutaitiwa mahali basi utasikia hata marafiki zako wakisema anajifanya eti mpambanaji basi ajitoe hapo alipokwama, wengine utasikia wanasema si alijifanya ana hela kwa sababu yeye ni mjasiriamali mbona siku hizi.....maneno mengi yote hayo yaache yapite ni upepo tu.

Mfano wa maisha ya Yesu
Wakati anachapwa mijeledi alithihakiwa, alitukanwa na kuambiwa kama yeye ni Mwana wa Mungu basi ajiokoe lakini hakutaka kuluzi focus kwa kuwajibu watu.

Lesson 6
Kupenda kile unachokifanya hata kama ni cha muda, maana yake nini hicho unachofanya ndiyo daraja la wewe kuifikia ile ndoto kubwa ya maisha yako.
Yesu alikubali kuja duniani lakini alikuwa anafahamu lengo ni nini. Alijua maisha ya duniani ni ya muda, pamoja na hayo aliithamini sana kazi yake hapa duniani, ndiyo maana leo tunamwita Mfalme wa wafalme.
Lesson 7.
Sio kila unachoombwa basi utoe, kuna wakati unapaswa kuwafundisha watu wanaokuomba namna yakufanya ili kuondoa jamu njiani wakati mwingine.

Yesu akawachia mwanafunzi wake kutoa pepo yeye akiwa hayupo, alitaka wajue na wawe na uwezo wa kujitegemea hata kama yeye hayupo. Hii ina jikita zaidi pale unapokuwa umefanikiwa, wengi hasa ndugu watakuja kukuomba fedha, wafundishe namna fedha inatafutwa.

Lesson 8.
Yesu ni mtoto wa tajiri ambae alikuja kuwafundisha masikini namna njema ya kuishi, hakuna lawama bali ni kufanya kazi bila kujali mazingira gani yanakukabili.

Alikuwa ni Mungu aliye uvaa utu ili kutufanya tujifunze kwa vitendo
Alifundisha pia yafuatayo
Kuwa na nia ya dhati.

General Lesson kwa mwaka huu 2019
Jitahidi sana kuwa wewe.
Fanya kazi zako bila kujali hali.
Focus kwenye malengo yako usipeperushwe na kelele za watu.
Fanya kwa bidii sana kila unapopata nafasi ya kufanya.
Simamia malengo yako.
Simamia ratiba zako.
Toa muda wa kujifunza na kuongeza maarifa ujuzi na taaluma mpya.
Fanya kazi kwa malengo na bidii
Baada ya yote.......
Kwa kila jambo Mungu ni wa kwanza.
Omba soma neno tafakari mtolee mungu kile kidogo anachokupa Mungu

Mwisho.
Yesu alikuja duniani kubadilisha fikra za watu kutoka mtazamo hasi mwenda Mtazamo chanya.
Mageuzi ya fikra yalianzia kwake.
Uaminifu na utii ndo yalikuwa maisha yake, hivyo yakupasa kuwa hivyo pia.
Kuthubutu hata kama huelewi, hata kama upo katika nchi ya ugeni mazingira   ni magumu
Yesu alikuja kukomboa
Roho
Fikra
Na ukombozi ulifanya katika aspects zote za maisha ya binadamu.
Mwaka huu ukawe mwaka wa mageuzi
Ya fikra, mitazamo na tuishi kwa malengo na targets huku tukimtumaini Mungu.

Mungu akubariki sana mwaka huu 2019 hasawewe uliemua kufanya kazi kwa bidii maarifa na ujuzi mwingi
Kwa utukufu wa Mungu utafanikiwa.

Prepared by:
Moses zephania Mgema
0755632375.
Mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam Tanzania

Wednesday, January 2, 2019

THAMANI YA WAZO LAKO.

Mungu amenissaidia, nmeamka salama kabisa. Nitoe pole kwa ndugu jamaa na marafiki ambao wanapitia changamoto mbalimbali, kwamba Mungu yupo atarejesha neema ya uzima au kuiondoa changamoto yoyote unayopitia sasa.
Mungu ni yule yule aliyemtendea Ayubu, lazaro na wengine, hata sisi pia lakini jambo jema ni kuendelea kumtumaini Mungu siku zote.

Leo ningependa tujifunze tena kitu muhimu na cha msingi sana hasa tunapoendelea na mchaka mchaka wa maisha ya kila siku.

Leo tutajifunza kitu kinaitwa        

*-THAMINI YA WAZO LAKO-*

Mungu wetu ni Mungu wa maarifa na maajabu mengi ambayo kiufupi tu hakuna mtu anaweza kuyaelewa zaidi ya kukiri tu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha yetu.

Mungu alituumba akatupa uwezo na akili yakuweza kutumia ili kuzitambua fursa na kuzitumia vyema kwa manufaa binafsi, familia, jamii lakini kwa ajili ya utukufu wake yeye Mungu.

Wazo  (Idea) ni moja ya silaha kubwa ambayo Mungu alimpatia mtu, na akampa uwezo wa kulinyumbua wazo hilo na kuwa faida kwake. Hapa ndipo tunaona watu wanagundua fursa mbalimbali zinazoendesha maisha yao.

Wazo (idea) ilimwijia Biligate, Wallace Wattle, mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg, wamiliki wa Twitter, whatsup, na mitaondao mingine ya kijamii hatimae leo tunatumia vitu hiv, Microsoft, Fb nk.  ni kati ya viungo vya mawasiliano ambavyo vimerahisisha sana njia za mawasiliano ukilinganisha na zama za kale.

Wazo la wagunduzi wa baiskel, pikipiki, gari, treni, meli na ndege, liligeuka kuwa fursa ambayo imeleta mageuzi makubwa sana kwenye nyanja za usafiri na usafirishaji.
Wazo ni kitu cha Thamani sana kama kikiheshimiwa na kupewa heshima yake, wazo hugeuza umasiki kuwa utajiri, wazo hugeuza woga kuwa ujasili, hapo ndipo tunapata watu waliojitoa muhanga bila kujal hadhi zao na leo ni watu wa mfano na matajiri duniani kote.

Kila jambo huanza kama wazo, liwe jambo baya au zuri lakini asili yake ni wazo moyoni na kwenye ufahamu wa mtu kabla halijaja katika ubayana wake.
Mpira wa miguu ulianzia nchini England kama wazo la wafanyakazi kujiburudisha baada ya kazi, lakini leo ni kati ya sekta inayozalisha ajira na utajiri mwingi kwa vijana na jamii kwa ujumla hapa (IDEA WAS IMPLEMENTED)

Mifano ni mingi mno ambayo tunaweza kuitumia, *-WALLACE WATTLE-* moja ya matajiri waliotokea kwenye familia masikini huko nchini marekani mwishoni mwa miaka ya 1880s hadi alipofariki dunia miaka ya 1900s aliwahi kusema, kila mtu ana wazo jema lakini namna ya kulitekeleza hilo wazo.

Watu duniani wana Mawazo mazuri sana na baadhi ya Mawazo ya watu masiki leo, yaliwahi kuwa ngazi ya watu matajiri duniani.
Kupitia vijiwe vya kawaha na vijiwe vya stori mawazo mengi huzalishwa na ni mawazo kuntu sana, shida iliyopo wale wanao zalisha mawazo hayo wengi wao hufanya ivo ili kunogesha vijiwe na kufanya siku iende wakalale.

Wachache sana wanaokuwa ndani ya vijiwe hivyo hung'amua mawazo hayo na kuyakusanya na kuyafanyia kazi na leo hawa matajiri tulio nao duniani na hapa Tanzania.
Hujawahi kupita mitaa ya jiji la Dar es salaam ukawasikia wazee wakisema huyu Bakhresa tulikuwaga tuko hapa anatuuzia kashata na kawa na wana feel proud kabisa kusema ivo, yawezekana ndani ya stori hizo kuna Mawazo bora kabisa Bakhresa aliyapata na kuyaboresha na leo yamemfanya kuwa  moja ya matajiri Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Nimekutana na mawakala na watu wengi wanaosema tulimpokea Shigongo alipotoka kwao Mwanza, na baadhi yao wanamwelezea kama mtu aliyekuwa duni sana lakini mwenye focus na malengo kwenye Idea yake.

Wengine wanasema waliuza naye magazeti,hata alipokuwa anaanzisha gazeti la uwazi akiwa hana kitu wengi wao walikuwa wanamtazama wanasema, wakati mwingine aliwaomba pesa ili kuzalishia gazeti la siku inayofuata na mengine mengi, lakini  leo Ndugu Shigongo ameajili zaidi ya watu mia kuanzia kwenye hotel zake, Global publishers, Global online Tv na vitega uchumi vyake vingine kama, Dar live mbagala ukumbi maarufu kabisa wa burudani.

Wazo ni kito cha Thamani sana, Je ni namna gani unaitumia, hakuna masikini duniani maana kila mtu ana wazo, wakati mwingine mawazo yetu ni bora kuliko waliofanikiwa, lakini hayaonekani bora kwa sababu hatujayaweka katika utekelezaji kwa kumaanisha toka ndani.

Wazo bila kuamua kulitekeleza ni sawa na midori ya wauza nguo sokoni kariakoo.
Amua leo bila kujali mazingira ya kiuchumi, kimaisha, nk. Amua kutoka moyoni.
Kufeli na kufaulu huwa ni maamzi ya mtu binafsi, ukiamua kufeli ni rahisi, ila ukiamua kufaulu au kufanikiwa ni maamzi magumu ya kutamani kutoka hapo ulipo kwenda eneo lingine.
Wazo ni jema pale tu unapolifanyia kazi kwa uaminifu, na kumaanisha, maisha yamekuwa na changamoto nyingi sana lakini hatuwez kuacha kupambana.
Kila mtu huwa na wazo, hivyo hakikisha unapopata wazo hilo lifanyie kazi immediately, bila kuchelewa, unapochelewa wengine wataliona na kulifanyia kazi.
Epuka kushirikisha ideas zako kama unaona kwamba bado huna uwezo wa kutekeleza kwa wakati huo, maana ukishare tu na watu, watu wenye nafasi zao watalitumia na wewe kubaki kwenye kushangaa.
Tumia wazo lako vyema, kuna wakati kama utakuwa na mawazo mazuri na huyatendei kazi basi kuna hatariya wewe kuumia kila siku kwa kuona watu wengine wakiyatumia mawazo yako
Heri ya mwaka mpya.
Moses zephania Mgema
0755632375
mgemamoses@gmail.com

ASANTE 2018, KARIBU SANA 2019

Mwaka 2018 umepita, tuna sababu ya kumshukuru Mungu sana kwa mengi mazuri aliyotutendea, mengi magumu aliyotuvusha, haikuwa rahisi hata kidogo maana ndugu jamaa, marafiki, majirani wameshindwa kuambatana nasi kwa kuunza mwaka huu.

Wengi wamefariki na wengine wameingia wakiwa wagonjwa na wengine wanapitia changamoto mbalimbali, lakini yote juu ya yote ni vyema kumshukuru Mungu tu.

Ni kwa neema wala sio kwa welevu, ujanja, ubora na utakatifu mwingi uliotufanya kuwa hai, is by Grace tu ndiyo maana tuko ndani ya mwaka huu tena, hakika ni kwa neema tu.

2019 tumeuanza kwa amani na furaha kubwa, wengi tukiwa na matumaini makubwa kwa kuset, mipango, malengo, shauku na hamasa ya kwamba mwaka huu basi ni mwaka ambao ni mwaka wa taofauti kabisa.

Kiuhalisia imekaaje, kiuhalisia kabisa kugeuza mwaka ni kama kulala na kuamka siku mpya, au kutoka mwezi mmoja kwenda mwezi mwingine in short ni mwendelezo wa maisha yaleyale tu.

Kwa kweli ndugu yangu tufanye kazi zaidi kuliko kuongea, mipango bila utekelezaji wa majukumu au wa mipango hiyo, kikawaida imekuwa ni mazoea ya kila unapoanza mwaka watu kupanga mipango na malengo, lakini kadri siku zikiwa zinasonga basi watu wanafunika diary zao na kusahau zile hamasa za mwanzo wa mwaka kabisa.

Kuanza mwaka sio kigezo cha wewe kubadilika kitabia na kimtazamo bali, maamzi ya dhati ya kuacha tabia za mazoea ndiyo kitu kinaweza kukufanya kufikia malengo ya kile ulichokifanya.

Pasipo Kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kuongea bila kutekeleza unachozungumza tutakuwa tunaanza na kumaliza miaka na miaka tukiwa kwenye tabia zilezile.

Lazima mabadiliko yaanzie kwenye fikra na maamzi ya dhati toka moyoni hapo ndipo unaweza kuona kweli mwaka umebadilika na uko tofauti na mwaka uliopita.

Katika kila jambo unalofanya mshirikishe Mungu, maana Mungu ndiyo  mwamzi na maratibu wa kila jambo tunalofanya, ni signatory wa kila jambo kwenye maisha yetu hakuna sababu ya kuishi bila kumtegemea Mungu.

Kufanya mambo ambayo yanamsikitisha mzazi wako basi jua Mungu anasikitika zaidi na hapo unajichumia laana utakuwa ukifanya mambo lakini hufanikiwi kumbe umeishi maisha yenye kumchukiza muumba wako.

God ni kila kitu fanya kila jambo kwa kumshirikisha Mungu, toa sadaka, fanya ibada, achana na waganga, na kuwategemea viumbe ambao pia kesho na kesho kutwa watakufa, na Biblia inasema amtegemeae mwanadam amelaaniwa achana na kuwategemea viumbe kama wewe.

Jifunze mara kwa mara ili kuujengea ubongo wako maarifa mengi kwa ajili ya matumizi yako binafsi na jamii.

Epuka mogogoro isiyo ya Lazima, hata kama ni ya lazima basi jitahidi kuepukana nayo kwa kila hali.

Samehe kwa kadili uwezavyo, ni afya ya akili nafsi na moyo, ukiombwa msamaha samehe, ukijua kuwa kila mtu anakosea, waweza kukosewa kama binadamu samehe maana hujui kesho yako wewe

Usiwe mtu wa kubeba mambo yasiyokuwa na faidia hata kidogo, kumbuka jambo likitokea limetokea huwezi kulifuta zaidi ya kusamehe tu.

Ushirika na wenzako liwe ni jambo la lazima kwa mwaka huu, baraka zingine za mafaniko zimefungwa kwenye ushirikiano na watu, kupitia ushirika mzuri na watu hapo ndipo unajenga connection na channels zingine ambazo huwezi zipata ukiwa pekee yako kama mkiwa jangwani.

Hekima, Busara  ni jambo jema kwa mwelekeo mzuri wa maisha yetu.

Nikutakie baraka za Bwana kwa mwaka huu, ukawe mwaka wa ushindi na utajiri kwa kila nyanja ya Maisha yako.

Kumbuka mkono mlegevu huleta umasikini bali mkono wenye bidii hutajilisha.
2019 Is the year of achievements
By
Moses zephania Mgema
0755632375

Tuesday, December 11, 2018

YOUR THE LIVING TESTIMONY/WEWE NI USHUHUDA UNAO ISHI.

Habari.
Mungu akubariki sana kwa kuendelea kuamini katika mfumo wa mabadiliko na mapinduzi ya fikra.

Mtu anae amini katika uwezo wake bila kujali mazingira, watu wanaomzunguka, hali ya kimaisha, Kielimu, kiimani na kadhalika mara nyingi mtu wa namna hii hufanikiwa sana kwenye maisha.

Mara nyingi huishi kwenye ndoto yake, malengo yake bila kujali amefikia ndoto na malengo hayo akiwa kwenye umri upi mwanzo kati au mwisho.

Mtu wa namna hii huwa hawaogopeshwi na hali yake, mazingira ila anachokiamini ni ule uwezo ulio ndani yake na kuamini kupitia uwezo huo ndiyo sababu ya yeye kuishi ndoto zake.

Sababu kubwa inayomfanya awe hivyo ni kuamini kuwa hakuna mtu aliumbiwa kuishi maisha ya hali fulani milele (uduni) na wengine kuwa na hali nzuri za kimaisha (utajiri).

Kupitia changamoto anazopitia humjengea shauku na imani kubwa ndani yake, kwamba kama wazazi wangu walishindwa kusapoti taaluma yangu kwa sababu ya Maisha duni,  umasikini wa kutisha basi, soluhisho la kuachana na hali hii duni, nikutumia uwezo mkumbwa ndani yangu kama daraja halisi la kunivusha hapa nilipo leo kwenda hatua bora zaidi ya kimaisha.

Hakuna kitu kizuri kama kuamini uwezo wako bila kujali wangapi wanakuona unajifurahisha, huwezi kufika popote  pale.

kuna watu wanavipaji katika maeneo tofauti tofauti ambao walipitia changamoto za kudharauliwa na kuonekana si chochote lakini kwa sababu waliamini walichonacho basi walipambana leo hii imebaki historia vijijini kwao na kuwaacha waandika historia za watu wakiendelea kujinasibu kuwa wanawajua sana huku wao wakila vyuku na bata mijini.

UMEWAHI KUJIULIZA UNA UWEZO GANI ?
Hili ni swali nyeti sana na muhimu kujiuliza hasa kwenye kipindi hiki cha ulimwengu kuamka na kutaka kila mtu kufanikiwa.
Mungu ameniumba mimi nikiwa na uwezo fulani, wewe pia...lakini je umeshatambua ?

Historia huandikwa na wengi lakini sababu ya historia kuandikwa na wengi kama hujua basi jua leo kuwa ni wewe.
Waandishi, marafiki ndugu  majirani na taifa kwa ujumla wanatamani kukusubilia wewe kwenye viwanja cha ndege vya  KIA au Julius k. Nyerere ukitoka nchi fulani ughaibuni kuiwakilisha nchi kwenye kwenye mashindano  fulani na hapo hapo una medani ya mashindano  hayo.

Ninachokijua na kukiamini ni kwamba kila jambo linawezekana kuandikwa kwa kusema wewe ni mshindi na mshindi ni yule ambae alitambua na kutumia uwezo wake ipasavyo.

Wewe ni ushuhuda unaoishi amini hivyo na jambo la msingi la kufanya ni wewe kujitafuta na kugundua uwezo wako uko kwenye eneo gani.

Kuandika, kucheza mpira, kuimba, kuigiza, kuongoza, kuongea, kucheza, kushauri, kushawishi, kuchora, kutawala eneo lolote, kufanya kazi na kufanya jambo la uwezo wako ni maeneo ambayo unaweza wekeza nakujitambulisha duniani kuwa wewe ni nani.

Wakati dunia ikimjua Bwana Samatta, Thomas ulimwengu, Diamond, Ally Kiba, Paul Clement, Joel Lwaga, Joel Nanauka, Eric Shigongo, Donie Moen, Mr Bin, Steven kanumba na jamii kutengeneza shauku ya kuwatazama basi hawa ndugu wanatengeneza fedha na utajiri wa kutisha sana.

Nini ulichonacho je unakijua je umepata njia ya kuiambia dunia kuwa wakati Mungu anaruhusu uje duniani alikupa uwezo fulani kwa ajili ya wanadamu kupata sababu ya kukupa fedha wakikutazama,  wakihangaika na mitandao kugugo ili wajue leo umefanya nini, nakinunua magazeti ili tu wajue una nini ?.....swali kubwa na muhimu sana kujiuliza.

Bado nina nafasi, bado una nafasi kaa chini jitathimini jiulize je umetumia kipaji chako kwa manufaa yako.
Nilipokuwa nikisoma historia ya Mwandishi Joel Nanauka na Eric Shigongo ndiyo mahali ambapo nilijua unaweza kuwa The living testimony kama ukijua thaman yako.

Nilikuwa nasoma tena na kusikiliza jitihada za Diamond, Mbwana Samatta, Watoto au wachezaji kutoka America ya kusini na wengine wengi ndipo nilipojua kuwa hakuna mtu ambae hana uwezo wa asili au (Natural ability) ambayo inaweza badilisha maisha yake.

Usikatishwe tamaa kuna wakati unapambana kwa bidii lakini mazingira sio rafiki,umasikini lakini mwisho wa siku Mungu hubariki sana mikono yenye bidii hasa kwenye eneo la kusudi lako.
Mbwana Samatta amelala sana kinesi, Uhuru stadium yote haya aliyafanya akiwa mbagala na alikuwa anawahi sana toka nyumbani ili program ya mazoez ya simba asikose hata point leo imebaki records kwenye vitabu ila yeye yuko ulaya.

Diamond, Harmonize na wengine wengi wamepambana sana kuwa mahali walipo leo jiulize wao waweze wana nini na wewe ushindwe una nini......Your the living Testimony jitambue.

Unaweza jiulize mimi nina nini.....ntakujibu mimi ni Ushuhuda unao ishi mwishoni mwa mwaka ujao utajua bila kusimuliwa kwa nini mimi ni The living testimony.

Hata wewe unaweza jipambanue, unaweza kuwa fulani kupitia kipaji chako, kazi unayofanya, biashara, kilimo na eneo lolote lile ulilopo ukishajitambua tu na kutambua thamani ya kile umekibeba ndani yako...
Mazingira, marafiki hukarii aina fulani fulani ya maisha, hapo ulipo unaweza nyanyuka vizuri kabisa acha visingizio pambana ongeza maarifa ujuzi na kupata wingi wa maarifa kwa kuendelea kusoma ili usiwe nje ya track.
Mgema Moses
P.o.box 166....
0755632375

Sunday, December 2, 2018

HONGERA SAMSON ERNEST KWA KUWA MFANO KWETU

Hongera katibu kwa uthubutu ambao hakika bado inatupa changamoto vijana wengine.
Chepeo ya Wokovu imeanza kama utani lakini leo ni moja ya website inayokuwa kwa kasi sana.
Kidogo kidogo leo umekuja na notebook, calendar kesho kitu kingine
Maisha yanahitaji sana, maamzi, bidii na juhudi, kujituma na kufanya kile ambacho unahisi ni sahihi kwa wakati sahihi, nidhamu, maarifa sahihi lakini ya kutosha, socialization. Juu yote haya Mungu lazima awe mbele kabisa maana ndo anahesabu kila hatua ya kila mtu.
Wakati najiunga na kundi la chepeo ya wokovu Facebook lilikuwa ni kundi dogo sana lakini leo ni kundi kubwa sana.

kila jambo lina vikwazo vyake kama vile  kukatishwa tamaa, watu kukuambia wewe huwezi, walikuwa kina fulani wakashindwa ije iwe wewe wapi..... vitu kama hivyo ni changamoto kwenye njia ya kila mtu lakini mwisho wa siku lazima uitambue focus na nia yako ni nini hapo ndipo unaweza thubutu na ukafanya kwa vitendo na vitendo vikaonekana kwenye matokeo.

Kalenda, Notebook vinaweza onekana ni vitu vidogo sana kwa Mtazamo wa watu wengi lakini kiufupi hili ni jambo kubwa sana ambalo kila mwenye akili anapaswa kulipongeza angawa kupongeza au kutokupongeza ni uamzi wa mtu Binafsi.
Vijana wezangu ni wakati wa kuamka na kutumia kila fursa inayopatikana Mbele yetu au kwenye mazingira yetu ili tuweze kuondoka kwenye maisha tuliyonayo kwa sasa.
Wakati wa kukaa tu, kulaumu, kuponda na kudharau na kujiona mwenye hadhi fulani huwezi kufanya mambo fulani umepotea na wakati ukiendelea kukaa kwenye mtazamo huo utajikuta unabaki mwandika historia za watu, kwamba huyu amekuwa tunamwona,tumesoma nae, amesoma hapahapa au amekuja akiwa hivi huku wenzako wameshasepa na maisha yao yako juu tayari.

Katibu ni somo kubwa sana kwangu, alinieleza alikoanzia mpaka alipo leo hakika ni mfano wa kuigwa sana ni mtu mpanaji asie kata tamaa, anafanya kazi sana, ana nidhamu sana kazini lakini ni mtu mwenye malengo makubwa, anaamini katika kile kidogo anapata ndicho kinaweza kumfanya akawa na kikubwa kesho.

Huwezi kuwa fulani kesho kama unakosa uthubutu, bidii, nidhamu katika kile kidogo unachopata, lakini bila malengo na nia ya dhati toka moyoni.
Kila mtu ana fursa kila mtu ana muda sawa na mwingine lakini namna ambavyo tunaweza kutumia huo muda.

Fedha watu tunapata lakini namna ya mgawanyo na matumizi ya hiyo fedha wapi unawekeza ni changamoto nyingine ambayo inatukumba vijana wengi, jitahidi kuheshimu kila kile kido unachopata ili kikufanye uwe na uwezo wa kusogea kesho huku ukijua kuwa hakuna siku utakuja kuwa na pesa nyingi kiasi kwamba utaanza kung'aa juu kwa juu ila katika vichache tunachopata ndicho chaweza kuleta kikubwa
Samson Ernest ni darasa kubwa sana kwa vijana wa Fpct Singida Mjini hakuna ubishi wala mashaka. Najua wapo wengi wamefanikiwa lakinikwangu mimi huyu ni mfano kwa vijana wengi
Tabua Thamani yako, tumia muda penda kujifunza ili kuongeza maarifa na ujuzi kwa ajili ya kuendelea kuwa bora