Sunday, December 2, 2018

HONGERA SAMSON ERNEST KWA KUWA MFANO KWETU

Hongera katibu kwa uthubutu ambao hakika bado inatupa changamoto vijana wengine.
Chepeo ya Wokovu imeanza kama utani lakini leo ni moja ya website inayokuwa kwa kasi sana.
Kidogo kidogo leo umekuja na notebook, calendar kesho kitu kingine
Maisha yanahitaji sana, maamzi, bidii na juhudi, kujituma na kufanya kile ambacho unahisi ni sahihi kwa wakati sahihi, nidhamu, maarifa sahihi lakini ya kutosha, socialization. Juu yote haya Mungu lazima awe mbele kabisa maana ndo anahesabu kila hatua ya kila mtu.
Wakati najiunga na kundi la chepeo ya wokovu Facebook lilikuwa ni kundi dogo sana lakini leo ni kundi kubwa sana.

kila jambo lina vikwazo vyake kama vile  kukatishwa tamaa, watu kukuambia wewe huwezi, walikuwa kina fulani wakashindwa ije iwe wewe wapi..... vitu kama hivyo ni changamoto kwenye njia ya kila mtu lakini mwisho wa siku lazima uitambue focus na nia yako ni nini hapo ndipo unaweza thubutu na ukafanya kwa vitendo na vitendo vikaonekana kwenye matokeo.

Kalenda, Notebook vinaweza onekana ni vitu vidogo sana kwa Mtazamo wa watu wengi lakini kiufupi hili ni jambo kubwa sana ambalo kila mwenye akili anapaswa kulipongeza angawa kupongeza au kutokupongeza ni uamzi wa mtu Binafsi.
Vijana wezangu ni wakati wa kuamka na kutumia kila fursa inayopatikana Mbele yetu au kwenye mazingira yetu ili tuweze kuondoka kwenye maisha tuliyonayo kwa sasa.
Wakati wa kukaa tu, kulaumu, kuponda na kudharau na kujiona mwenye hadhi fulani huwezi kufanya mambo fulani umepotea na wakati ukiendelea kukaa kwenye mtazamo huo utajikuta unabaki mwandika historia za watu, kwamba huyu amekuwa tunamwona,tumesoma nae, amesoma hapahapa au amekuja akiwa hivi huku wenzako wameshasepa na maisha yao yako juu tayari.

Katibu ni somo kubwa sana kwangu, alinieleza alikoanzia mpaka alipo leo hakika ni mfano wa kuigwa sana ni mtu mpanaji asie kata tamaa, anafanya kazi sana, ana nidhamu sana kazini lakini ni mtu mwenye malengo makubwa, anaamini katika kile kidogo anapata ndicho kinaweza kumfanya akawa na kikubwa kesho.

Huwezi kuwa fulani kesho kama unakosa uthubutu, bidii, nidhamu katika kile kidogo unachopata, lakini bila malengo na nia ya dhati toka moyoni.
Kila mtu ana fursa kila mtu ana muda sawa na mwingine lakini namna ambavyo tunaweza kutumia huo muda.

Fedha watu tunapata lakini namna ya mgawanyo na matumizi ya hiyo fedha wapi unawekeza ni changamoto nyingine ambayo inatukumba vijana wengi, jitahidi kuheshimu kila kile kido unachopata ili kikufanye uwe na uwezo wa kusogea kesho huku ukijua kuwa hakuna siku utakuja kuwa na pesa nyingi kiasi kwamba utaanza kung'aa juu kwa juu ila katika vichache tunachopata ndicho chaweza kuleta kikubwa
Samson Ernest ni darasa kubwa sana kwa vijana wa Fpct Singida Mjini hakuna ubishi wala mashaka. Najua wapo wengi wamefanikiwa lakinikwangu mimi huyu ni mfano kwa vijana wengi
Tabua Thamani yako, tumia muda penda kujifunza ili kuongeza maarifa na ujuzi kwa ajili ya kuendelea kuwa bora

No comments:

Post a Comment