Monday, October 8, 2018

GUNDUA UWEZO NDANI YAKO

DISCOVER YOUR POTENTIAL IN YOU/ GUNDUA UWEZO NDANI YAKO ----1

Kila mtu ana uwezo wa kipekee.Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuongoza lakini bado hajafahamu uwezo alio nao .Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuzungumza lakini bado hajielewi .Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuandika lakini hadi anavyosoma makala hii bado hajielewi maana hajawi kuanza kuonesha uwezo wake .Kwa kutambua uwepo wa watu wengi wasiojua uwezo walio nao nimekuandalia makala zitakazoamsha uwezo ulio ndani yako ili ukufikishe kule unakotaka kufika.

Mungu alivyokuumba aliweka ndani yako uwezo mkubwa sana kwa bahati mbaya watu tumeshindwa kutambua uwezo tulionao.Ni lazima kama unataka kufika kule unakotaka kufika kufahamu kabisa nini unaweza kufanya vizuri kwa uwezo uliopewa na Mungu .Acha kuwasikiliza watu wanaokukosoa na watu wanaokurudisha nyuma .Wewe amini katika uwezo wako ambao uko ndani yako .

Kama unaweza kuimba vizuri fahamu huo ndio uwezo Mungu alikupa .Tumia vizuri uwezo huo bila kugeuka nyuma na utafika mbali sana .Acha kuangalia madhaifu uliyonayo lakini angalia uwezo ulio nao .

Watu waliofahamu uwezo wao (maeneo yao ya kujidai ) na wakajua namna ya kuwajibika ,walifika mbali sana .Je ,watu hawa waliofika mbali hawakuwa na madhaifu ?  Jibu ni Hapana walichokiangalia ni uwezo ambao walikuwa nao kuliko madhaifu yao .

Uwezo ulionao hauzuiliwi na jambo lolote.Haijalishi umezaliwa wapi na unaishi wapi uwezo wako ukiamua kuutumia utaonekana tu.Kama unaweza kucheza mpira vizuri  hakikisha unacheza mpira kwa nguvu na akili yako yote maana hapa ndipo mafanikio yako yaliko .Kama unaweza kuchekesha watu fanya hivyo ukielewa kabisa wapo watu ambao wamefanikiwa kupitia uchekeshaji .

Watu hawa walivyoelewa uwezo walionao maisha yao leo yamebadilika.

Nick Vujic
Nick ni mlemavu asiyekuwa na miguu wala mikono ambaye mbali na kuwa alizaliwa mlemavu hivyo alielewa eneo lake ambalo alikuwa na uwezo nalo .Nick baada ya kuona hawezi kazi za kutumia mikono au miguu alianza kufikiri nini ana uwezo nacho na akagundua anaweza kuhamasisha watu na watu wakahamasika .Nick bila kuchelewa alianzisha taasisi yake ambaye yeye aliiita  taasisi ya maisha bila miguu (life without limbs) na akaanza kuzunguka dunia nzima kuhamasisha watu hasa walemavu .Leo Nick Dunia nzima inamfahamu.

Mwalimu Julius Nyerere
Mwalimu Nyerere ni ni mtu  ambaye alifahamu kuwa alikuwa na uwezo wa kuongoza watu na akatumia uwezo wake kwa viwango vikubwa sana leo Mwalimu Nyerere Dunia nzima inamkumbuka kwa kuwa alitumia uwezo wake aliokuwa nao.

Mbwana Sammatta
Mbwana Samatta baada ya kufahamu kuwa Mungu ameweka uwezo wa kucheza mpira vizuri ndani yake alianza mara moja kucheza mpira .Samatta hakuwa anacheza kama wachezaji wengine wanaofikiria kucheza mpira Simba na Yanga maisha yao yaishie hapo lakini yeye alicheza huku akijua siku moja dunia itakuwa ikimsikia na kufuatilia uwezo wake .Mtazamo wake ulikuwa mtazamo mpana wa kuhakisha uwezo wake unamtangaza Duniani .Leo Mbwana Sammatta Dunia inamjua na hakika mafanikio yake si haba.

MC PILIPILI
MC Pilipili alivyogundua kuwa ana uwezo wa kupangilia maneno na kuongea mbele za watu aliamua kuwa mshereheshaji (Master of Ceremony) .Leo Mc Pilipili amefika mbali sana kwa kuwa siku moja aliamua kutumia kile kilichoko ndani yake

Ni lazima ujue wewe ni mzuri na kufanya katika viwango vikubwa sana bila kuangalia mwenzako anafanya nini .Lazima ufike mahali uorodheshe vitu unavyofanya kwa uzuri na hivyo ndivyo vitakutoa katika maisha .Acha kuamini kuwa vyeti vyako ndivyo pekee vitakufanikisha utachelewa sana .Inuka anza kuangalia nini unaweza kufanya ili maisha yako yabadilike .

Unajua nini ? Unaweza kufanya nini ? unaweza kufanya nini kwa uzuri ? .Amsha uwezo wako leo

Itaendelea.

Friday, October 5, 2018

MANENO YA DIAMOND KATIKA SAFARI YA MAISHA YAKE

MAMBO MACHACHE AMBAYO NI MUHIMU KUJIFUNZA KUTOKA KWA KIJANA MWENZETU DIAMOND ALIYOYASEMA KWENYE SIKU YA KUZALIWA KWAKE

Tahere 2/10/2018 ilikuwa ni siku maalumu sana ya Nasibu Abdul alimaarufu diamond ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake

Kuna mambo mengi sana alizungumza Diamond kuhusu maisha yake ya muziki hata maisha kabla ya mziki yani alikotoka hadi hapa alipo.
Yako mambo mazuri sana ya kujifunza kutoka  kwa Diamond  kwa kijana anayetaka kutoka kimaisha sio tu kwa njia ya muziki lakini katika kila jambo unalofanya.

Nimefurahia sana kusikia yeye mwenyewe akizungumza na kuelezea alikopita na mambo aliyofanya hapo kabla hajawa DIAMOND mpaka alipokuja kuwa DIAMOND offcourse amezungumzia mambo mengi mazuri kama ifuatavyo

Hakuchagua kazi diamond alifanya kila kazi iliyokuwa mbele yake ambayo haikuvunja sheria au kwa lugha nyepesi kazi haramu.......Diamonda
1.aliuza mchanga
2.Alifanya kazi petrol station
3.Aliuza nguo
4.Alipiga picha mfumo wa zamani
Then diamond alisema ili uweze kufanikiwa Pamoja na kufanya kazi kwa bidii mambo yafuatayo lazima yachukue nafasi kwenye harakati zako
a. Ubunifu katika kila kazi unafanya
B. Bidii na maarifa ujuzi pia ni lazima
C. Uaminifu katika kazi yako na kazi za watu hii itakusaidia kujenga brand yako ya kuaminika kwa watu na siku nyingine watu watatamani kufanya kazi na wewe.
d. Kutokukata tamaa...kuna wakati unahitaji mtu fulani awe daraja lako kufikia ndoto zako lakini ni ngumu kumpata lakini unachopaswa kufanya pambana hakikisha adhima yako inatimia
e. Mwombe Mungu sana kwa kila jambo
f. Weka nia ya dhati toka moyoni dhamiria kufikia matamanio yako.


Alisema tena kumbuka kutengeneza mazingira ya watu kukupa kazi ajira na mambo mingine
Hapa akasema kuwa smart kuanzia nje hadi namna ya kufikiri jiupushe na mihadarati haisaidii kabisa.


Katika safari ya mafaniko mambo ya kukatisha tamaa ni mengi lakini usikubali yakushinde bali pambana kuyashinda. Wapo watu wengi sana amabao wanakatisha vijana tamaa kuwa wewe huwezi jambo fulani labda jambo fulani ndo unaweza hapana hilo unaloamini unaliweza na linamanufaaa kwako fanya  pambana mpaka mwisho utafanikiwa.

Tumia kila nafasi unayopata ukijua nafasi nyeti huja mara moja tu kwenye maisha.
MWISHO
Kile Mungu anakupa baada ya kupambana kumbuka haya
Rudisha kwa jamii hata kama ni kidogo watu watakuombea na Mungu atakuinua zaidi ya mahali utakapokuwa
Aliyofanya diamond leo Tarehe 5/10/2018
Kawapa vijana wenzake wa tandale pikipiki 20
Watu 1000 kuwapa bima
Wakina mama 100 amewapa mtaji
Kuna mama mlemavu amempatia bajaji
Katoa Gari kwa mpiga picha wake
Mengi amefanya hakika sadaka humwinua zaidi mtu
Prepared by Moses Mgema
Source Diamond plutnum
Contacts: 0755632375/0678355394
Facebook Moses zephania
Instagram & Twitter moses mgema

NA MAONO YA MAYLES MUNROE

MISINGI NA NGUVU: Dr. Myles Munroe alikuwa raia wa Bahama, aliyezaliwa tar 20/04/1954 na kufariki 09/11/2014.(64) kwa ajali ya ndege Binafsi aliyokuwa akitumia akienda kwenye moja ya mikutano yake akiwa na mke wake na wengine nane walipoteza maisha katika ajali hiyo moja.

Shughuli zake
Alikuwa mhubiri wa kimataifa, mwandishi, mwanzilishi wa huduma ya BFMI (Bahamas Faith Ministry International). mwalimu wa masomo ya uongozi, uchumi, kiroho na maisha ya mafanikio.

Pamoja na kuwa Dr. Myles Munroe ni hayati lakini bado mpaka sasa anaishi kufuatana na kazi yake aliyofanya katika kugusa maisha ya vizazi vyake na kwa kauli yake *nitakufa mtupu* nafikiri ilitimia japo ukianza kufuatilia masomo yake mbalimbali unaweza kuona aliwahi kufa.

Kwa nini Nimekuletea hiki kitabu

Maono ni kitu muhimu sana na kama mtu yeyote anataka mafanikio makubwa sana ya kifedha, kiroho, kiafya, kielimu, kimahusiano na kiakili basi cha kwanza kabisa ni kuwa na maono, na hiki ni moja ya vitabu ambavyo vinaeleza vizuri sana kuhusu MAONO, yani kinaeleza kwa lugha rahisi sana, nini maana ya maono, misingi na nguvu yake katika maisha ya kila mtu

Binafsi nilikuwa nafuatilia namna watu wanavyofundisha kuhusu maono, ndoto na kusudi ila waliyo wengi wameshindwa kuelezea kiusahihi eneo hili, kwani kila mtu amekuwa na uwelewa tofauti lakini nilipo pata kitabu hiki niliona suluhisho kwa kila mtu endapo atapata nafasi ya ya kukisoma kitabu hiki cha Maisha bila maono

Maisha mazuri ni yale ambayo yanatokana na mtu kuwa na picha ya baadae yake, kujua unaenda kufanya nini miaka michache ijayo, kuishi maisha ya namna gani, kukaa na watu gani, na kugusa watu wa aina gani.

Mungu aliweka kusudi ndani ya kila mmoja ndani yake na hiyo ndio thamani yako katika Dunia hii, ndani yako kuna dhahabu ila haiwezi kuchimbwa na mtu yoyote ila wewe mwenyewe hivyo lazima uamue mwenyewe kuishi maono yako, kuwa na maana harisi ya maisha yako.

Pasipo maono huwezi kuona Mbali zaidi ya hapo ulipo leo, kuwa na maono ni sawa na kwenda kukaa kilele cha mlima na muono wako unaongezeka.

Hivyo kama umeishi muda mrefu bila maono ,Myles anatuonyesha kitu ambacho wachache wamekuwa wakiishi na kufanikiwa.

Wednesday, October 3, 2018

JIFUNZE USIIGE MAISHA YA MWINGINE

OHabari za muda huu
Napenda kushare nanyi jambo muhimu sana kwa muda huu inaweza kuwa faida kwako leo hata kesho

Duniani kuna watu ambao wamekuwa wakiishi maisha ya ku copy na ku paste.......Yaani mtu anamuiga mtu fulani kwa kila kitu anachofanya wakati mwingine bila hata kujiuliza kwa nini mtu huyu amefanya jambo hili mwisho wa siku wamejikuta wakiangamia na kupotea kabisa lakini pia kupoteza ndoto na uwezo wao kwa sababu tu waliamua kuishi Maisha fulani ya kukopi.
Kuiga sio jambo baya lakini pia kumbuka kuwa kila mtu ameumbwa kwa kusudi na kazi yake hapa duniani hivyo unapoondoka kwenye kusudi au kazi ambayo Mungu alikupa mwisho wa siku maisha yako yatakoma duniani hapa hakuna ulichokifanya maana uliamua kuishi nje ya kusudi la Mungu

Kumbuka kuwa maisha ni mtihani ambao kila mtu amepewa mtihani wenye maswali tofaut na mwingine.
Kumbuka Maisha ni moja ya mtihani mgumu sana na watu wengi wanafeli kwa sababu ya kukopi Maisha ya wengine pasipo kufahamu kwamba kila Mtu ana maswali yake katika katika chumba cha mtihani.

Hivyo Kijana jaribu sana kukaa chini jikague jitathimini ili kuweza kujipambanua kuwa wewe ulizaliwa na lengo gani
Fanya kazi kwa bidii kuwa mbunifu ongeza maarifa katika kila jambo unalofanya.
Note
Sijasema kuwa usiwe na watu unaopenda kuwa kama wao hapana jifunze kwao njia na kanuni walizopitia kufika mahali walipo then baada ya hapo kaa chini chukua jema tupa kule lisilo faa
Halafu anza kufanya kile moyo na akili yako inakuambia kuwa ukifanya hiki utafanya katika ubora kwa kiwango cha juu na kwa ubora mkubwa zaidi.
Life is too short try to utilize every single second effectively through the natural gift or talent that God created with
Be blessed and have a very good moment 
By Moses

Tuesday, September 25, 2018

WAZAZI NA WAZAZI MNAOKUJA AMKENI SIKU ZIMEBADILIKA

PARENTS AND UPCOMING PARENTS WAKE UP DAYS HAVE CHANGED:
Nimshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuwa mzima na mwenye afya tele kufikia sasa.
Nitoe pole kwa ndugu jamaa marafiki na wanamwanza na Tanzania kwa ujumla kwa msiba mkubwa ambao umelikumba Taifa letu siku ya Alhamis Tarehe 20/09/2018 kwa Meri ya Mv nyerere kuzama katika ziwa victoria.
Yote kwa Yote mola anapo ruhusu haku na wa kupinga. Zaidi ya yote Tumshukuru Mungu.

Leo napenda sana tujifunze mambo machache ambayo kwa hakika ni muhimu sana kuyajua.
Dunia tunayoishi inakwenda kwa speed sana na hakika mambo yamebadilika sana katika karne hii tuliyo nayo
ongezeko la maendeleo ya Teknolojia na utandawazi umechukua hatamu kwa wingi.
Maendeleo haya ya sayansi na Teknolojia yameweza kurahisisha sana njia za mawasiliano na utendaji kazi pia ukilinganisha na huko tulikotoka.
mambo ambayo yangeweza faywa na watu kumi leo watu watatu wanaweza kuhatekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu sana na wakati sahihi.

Mahali ambapo ilitupasa kusafiri kupeleka mizigo au kupeleka habari fulani leo hatufanyi tena.
umekaa kwenye kiti unaratibu kila kitu hapo hapo na kila kitu kinafanikiwa kwa ufanisi ule ule ulioutaka
Express=Digital Age period ni muda ambao tunaishi.
Maendeleo haya yamekuja na matokeo Yote yaani
matokeo chanya  (positive results)
Matokeo hasi  (Negative results)
Tumeona kwa uchache matokeo chanya hapo juu japo sio yote ila tunaweza ongeza zaidi na zaidi

MATOKEO HASI  (NEGATIVE RESULTS)
Baada ya maendeleo haya kuchukua nafasi watu wengi wamekosa ajira
Idadi ya watu ambao wangehitajika kuajiliwa mahali fulani kama ni 10 sasa wanahitajika wawili au watu wakati mwingine mmoja tu.
Jiulize swali hawa wengine tisa nane na saba wako wapi?
posta ilikuwa na madereva lundo na posta ilikuwa active. Jiulize baada ya simu na matumizi ya scanning, Email simu calling sms nk. kuchukua hatamu wako wapi waliokuwa waajiliwa posta na maeneo mengine.
Baada ya hapo dunia imejikita katika ujasiriamali  (Entrepreneurship) kila mmoja barabarani na maeneo mengi watu wanafanya business.
Lakini bado sijajua kama watu wanachukua tahadhali ya kuwa kama ajira zilikuwa nyingi enzi hizo na leo ni changamoto je mambo ya ujasiriamali hayatafika mahali yabane iwe ilimradi watu wanafanya business.
Kiufupi ni kwamba biashara hazitakoma hata kama watu watakuwa wanaigana lakini bado watu wataendelea kufanya biashara.
Faida Je hilo ni swala lingine la kusubiri.

Kuna jambo muhimu sana kizazi cha leo lazima tuyajue lakini pia kuyafanyia kazi kwa haraka na kuwekeza nguvu kwa nguvu zote kuanzia rasilimal nafasi tulizo nazo ushauri nk kwa watoto wetu.
Mungu atabaki kuwa Mungu kabla ya misingi ya dunia aliyajua yote haya ndiyo maana akamwezesha kila mtu kitu cha pekee sana ndani yake.
Kipaji ni zawadi na hii zawadi ni zawadi ambayo hakuna anaweza kuigawa mzazi anaweza mpa mtoto wake kila kitu elimu fedha na mahitaji yote lakini kipaji ni Mungu pekee.
Dunia ya kwanza yaani nchi zilizoendelea Nchi za ulaya Kama England, German France nk. zinafurahia faida kubwa kutokana na vipaji vya watoto wao kuanzia kwenye soka mziki, Kikapu wasemaji wa hadhara  (Public speakers) waandishi wasimuliaji washauri wa masuala ya biashara, saikolojia, kudansi kupiga mziki, kuchora, kuchekesha na kila aina ya vipaji.
wenzetu walishituka mapema wakawekeza sana kwenye kile mtoto anakipenda lakini pia alicho na uwezo nacho.
Wanachofanya wanatoa elimu ili kumwezesha mtoto kujua Thamani ya kile kitu alicho nacho na namna ya kukitumia na kumletea manufaa.

kupitia njia hizo hakika dunia imeweza kushuhudia burudani mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali ambao waliweza na wanaoendelea kutumia vipaji vyao.
Mfano dunia ya soka imeshuhudia watu wengi waliozaliwa kwenye familia masikini na fukara wakibadilisha sura na maisha ya familia zao.
Iko mifano mingi ya vijana kutoka Amerika ya kusini kwenye nchi kama
Argentina, Brazil chile Uruguay peru Ambao  ni kina Alexes Sanchez, Ronaldo, Leo Messi, Ronaldinho Gaucho, Angel Di maria na wengine wengi  na baadhi ya nchi za Afrika magharibi  amabao ni Nwango kanu Didie Drogba Samwel Eto'o na Afrika mashariki kidogo Mbwana Ally  Samatta, Donald mariga na ndugu yake Victor wanyama toka nchini kenya kwa hakika wengi na baadhi yao walizaliwa kwenye kaya fukara sana lakini leo ni mamilionea na mabilionea wa kutupwa sababu kubwa ni vipaji.

Vile vile kwenye music,waigizaji iko mifano hai ya watu wanaovuna pesa kwa sababu ya music na uigizaji na uchekeshaji mifano hai:Mr Bin waimbaji Boyce Michael Jackson na wengine wengi hata hapa nyumban kidogo kina diamond Ali kiba kwa uchache angalau mifano ipo.
Wazazi wengi tunajaribu kukariri maisha sana Kitabu cha Rich dad and poor dad kinagusia sana kwa habari ya kijana ambae aliona elimu ya darasani kwake haikuwa much paid kwa sababu ni kama aliona wazazi wake wanafanyia kazi maisha ya kulipa kodi na mafao ya uzeeni ndipo mama ake alipogundua kuwa wao kama wazazi walikuwa wamekariri mfumo wa maisha ambao wazazi wao waliutumia hapo awali na hakujua kuwa dunia tayar ilikuwa nje ya kile alikuwa akikisshi.
Ndiyo wazazi wengi tulivyo hata sio kwamba tunasema watoto wasiende shule hapana lazima watoto waende shule lakini lazima tuwe namna nzuri ya kufanya vipaji vya watoto vinakuwa na manufaa kwao sana
Ajira kwa sasa hakuna lakini pia mtu anaetumia kipaji chake vema hakika hakuna mfanya kazi anaweza mgusa kiuchumi na kifedha mifano angalia diamond Ali kiba  lady Jdee Harmonize  Mbwana Samatta kwa hapa nyumban na wengine wengi
Majuu
Cristiano Ronaldo Leo Messi David Beckham Ronaldo delima LeBron James nk  ni watu matajiri wa kupindukia kwa sababu ya vipaji vyao
Lazima wazazi tushituke tuache kuishi kwa mazoea tusitumie nafasi zetu za uzazi kudidimiza na kuua vipaji vya watoto
wewe kama mzazi onya elekeza shauri na tekeleza hitaji la mtoto ili afanye jambo anapenda kwa uhakika kwa moyo na kwa upendo na kwa manufaa yake na kwako pia.
kwa leo tuishie hapo itaendelea......next time
Moses zephania Mgema
mwandishi
mgemamoses@gmail.com
0755632375/ 0678355394

Friday, September 14, 2018

Brand yourself

*CHAGUA UNATAKA KUWA BORA KWENYE NINI?*

Kila jambo lina bingwa wake, kama unakumbuka Michael Jackson alikuwa Bingwa wa Muziki wa Pop Duniani, Michael Jordan alikuwa ni bingwa wa mchezo wa kikapu.

Vivyo hivyo Pelle, Mike Tyson, Diana King na wengine kibao. Ukija Bongo kwenye Muziki wa Taarab, Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa anakaa, Mfalme Mzee Yusuph anachukua kwa wanaume, Kina  diamond Ali kiba  na wengine wengi na ndivyo ilivyo kwa wengine na wengine.

Nimetolea mfano vitu hivyo vichache lakini kuna vitu vingi sana vinahitaji bingwa au bora wa kuviongoza au kuvifanya. Je, leo hii wakiita bingwa wa jambo fulani mtaani kwako utatoka au na penyewe hautaweza kuonesha uwezo au ubora wako?
Kuna watu wao huwa nyuma kwa kila jambo yaani ile kujifanya nyuma nyuma kwa kila kitu na hii imechangia watu wengi sana kupoteza karama vipaji vyao kwa sababu ya kuwa nyuma nyuma kwa kila jambo.
Jiulize una uwezo gani wewe kama wewe au wakati Mungu anakuumba kitu gani aliweka ndani yako na ili iweje aweke kwako na sio kwangu au kwa yule kiufupi unagundua kuwa
Mungu alikuamini
alijua wewe pekee ndo unaweza kukitendea haki kitu hicho
hivyo basi jaribu kukitumia kwa ajili yako na kikutambulishe kuwa mtu akihitajika kwa jambo fulani basi iwe ni wewe
Leo dunia ina mfahamu Tyson Diamond,Eric Shigongo, c.Ronaldo, Leo Messi.
Jay z Beyonce, Bob Marley na wengine wengi ambao walijipambanua na kutumia vipawa vyao mpaka leo hata kama wengine wamekufa lakini bado kazi zao zinaishi
Jiulize Mimi nitakumbukwa na nini  ?

Jifunze au jitengeneze kuwa bigwa wa Jambo Fulani kama Mungu alikuamini na kukuumba na akakupa uwezo fulani tumia nafasi ya uwezo huo au kipaji hicho kujitanbulisha na kutambulika kwenye jamii kwa manufaa yako au manufaa ya kazazi chako ninacho
Muda wa kuwaandalia watoto wako maisha mazuri ni leo kwa kutumia kile ulicho nacho kama ni kipaji au kazi na biashara uliyo nayo
work hard

MUANDALIE  MAZINGIRA MWANAO  ULIYENAYE AUAJAYE.

0719110760
Email mgemamoses@gmail.com
Moses zephania Mgema.
Instagram: Mo_mgema

Thursday, August 2, 2018

Madhara ya kufikiri muda mrefu

Kiumbe binadamu ni kiumbe  aliyeumbwa  kipekee sana ukilinganisha na viumbe wengine kama mimea wadudu na wanyama wa aina zote.
Binadamu amepewa uwezo na utashi unaomfanya kuwa na uwezo wa kufanya mambo yake kwa weledi na kwa ufanisi na kujisimamia.
Amepewa utashi wa kutambua jema na baya kama vitabu vya dini vinavyotuambia.
Binadamu huyu tangu aumbwe amekuwa na maisha yenye mchanganyiko Fulani ambao unamfanya wakati mwingine atenge muda wake kwa ajiri ya kufikiri ili mambo yake yakae sawa.
Hebu tutazame mambo machache ambayo mtu anaefikiri sana yaweza kumpata ( matokeo hasi)
1. Kuchelewa kuchukua maamzi na wakati mwingine kusababisha madhara
2. Huwa ni ngumu sana kufikia malengo yao hasa kibiashara na kimahusiano kwa sababu muda wote anaofikiri
  . huona changamoto nyingi kuliko njia za kutatulia hizo changamoto hasa kwa suala zima la biashara na kazi
. wakati mwingine hupata msongo wa mawazo kwa sababu anaweza akachukua muda mwingi kufikiri jambo Fulani na akaona matokeo makubwa kabla hajaweka utekelezaji anapokuja kufanya kwa vitendo na isifikie mahali alitazamia basi kwake huwa anaumia sana
.Huzeeka kabla ya umri wao
. Hukosa fursa
. Huwa sio rahisi kukubali kama wanaweza kukosea.
Note
Hujashauriwa kuacha kufikiri ila jaribu kuwa na kiasi