*CHAGUA UNATAKA KUWA BORA KWENYE NINI?*
Kila jambo lina bingwa wake, kama unakumbuka Michael Jackson alikuwa Bingwa wa Muziki wa Pop Duniani, Michael Jordan alikuwa ni bingwa wa mchezo wa kikapu.
Vivyo hivyo Pelle, Mike Tyson, Diana King na wengine kibao. Ukija Bongo kwenye Muziki wa Taarab, Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa anakaa, Mfalme Mzee Yusuph anachukua kwa wanaume, Kina diamond Ali kiba na wengine wengi na ndivyo ilivyo kwa wengine na wengine.
Nimetolea mfano vitu hivyo vichache lakini kuna vitu vingi sana vinahitaji bingwa au bora wa kuviongoza au kuvifanya. Je, leo hii wakiita bingwa wa jambo fulani mtaani kwako utatoka au na penyewe hautaweza kuonesha uwezo au ubora wako?
Kuna watu wao huwa nyuma kwa kila jambo yaani ile kujifanya nyuma nyuma kwa kila kitu na hii imechangia watu wengi sana kupoteza karama vipaji vyao kwa sababu ya kuwa nyuma nyuma kwa kila jambo.
Jiulize una uwezo gani wewe kama wewe au wakati Mungu anakuumba kitu gani aliweka ndani yako na ili iweje aweke kwako na sio kwangu au kwa yule kiufupi unagundua kuwa
Mungu alikuamini
alijua wewe pekee ndo unaweza kukitendea haki kitu hicho
hivyo basi jaribu kukitumia kwa ajili yako na kikutambulishe kuwa mtu akihitajika kwa jambo fulani basi iwe ni wewe
Leo dunia ina mfahamu Tyson Diamond,Eric Shigongo, c.Ronaldo, Leo Messi.
Jay z Beyonce, Bob Marley na wengine wengi ambao walijipambanua na kutumia vipawa vyao mpaka leo hata kama wengine wamekufa lakini bado kazi zao zinaishi
Jiulize Mimi nitakumbukwa na nini ?
Jifunze au jitengeneze kuwa bigwa wa Jambo Fulani kama Mungu alikuamini na kukuumba na akakupa uwezo fulani tumia nafasi ya uwezo huo au kipaji hicho kujitanbulisha na kutambulika kwenye jamii kwa manufaa yako au manufaa ya kazazi chako ninacho
Muda wa kuwaandalia watoto wako maisha mazuri ni leo kwa kutumia kile ulicho nacho kama ni kipaji au kazi na biashara uliyo nayo
work hard
MUANDALIE MAZINGIRA MWANAO ULIYENAYE AUAJAYE.
0719110760
Email mgemamoses@gmail.com
Moses zephania Mgema.
Instagram: Mo_mgema
No comments:
Post a Comment