Sunday, February 19, 2023

Teknolojia na sayansi umeturahisishia sana maisha katika karne hii ya 21, kila kitu kinapatikana kwa urahisi zaidi hasa kwenye eneo la kupata maarifa na ujuzi mpya muda wowote ambao utataka kupata maarifa na ujuzi huo...
Elimu ya maisha, elimu ya biashara, afya, siasa na kila eneo maarifa na ujuzi unafundishwa kupitia platforms mbalimbali za mitandaoni, tofauti na miaka ya nyumba ambapo watu wenye maarifa ni wale tu ambao walikuwa na bidii ya kwenda maktaba kusoma vitabu, kusoma magazeti nk....

Katika kupanuka kwa vyanzo vya habari duniani umechangia sana kuyafanya maisha kuwa ya ushindani katika biashara, siasa, dini na kwenye maeneo mengine ya maisha, hii ninkwa sababu watu wamekuwa wakijifunza kwa mifano na kuona kumbwa, utajiri na kuwa na mali ni haki ya kila mtu hapa duniani.

Kupata maarifa ni pesa, kupata ujuzi ni hela lakini maarifa haya yanapatikana kwa njia ambayo wakati mwinginr unaweza kuwa unalipa gharama pasipokupata maumivu sana lakini ndiyo unajikuta unalipia gharama za kujifunza na wewe kupata maarofa, mfano unaweza usitoe pesa kwa ajili ya kujifunza 

Friday, February 10, 2023

Neno

How youth ministry in Church shaped 

Proverbs 22:6 (KJV) Train up a child in the way he should go: and when he is old, he will not depart

Proverbs 22:6 is dear to me because it genuinely reflects the effect the youth ministry had on me. When I immigrated to the United States, I was uprooted from the Church I knew all my life. So, I struggled initially. I can say that the teachings and the word of God that was planted firmly in my heart helped me find my way back ♥️.

1 Timothy 4:12 (NIV) Don’t let anyone look down on you because you are young, but set an example for the believers in speech, in conduct, in love, in faith , and in purity.

This is absolutely true. Youth ministry sets an example for believers. For example, in terms of purity, I will discuss more of this later in the post.

7 BENEFITS OF YOUTH MINISTRY IN THE CHURCH

Here are the benefits of youth ministry!

1. Role Models and Mentors

When I turned 13 years old, I joined Youth Church, and I was super super excited to see older youth who had graduated from youth church and came to speak to us. They were on fire for God, and they would often accompany us in our church camps. One, in particular, was called Seth! He was really outgoing and would fearlessly share his testimonies which were relatable.

I found that at this age, youth relate more to their peers than their parents. That is why they need to be around positive role models and mentors who will plant good seed into their lives!

2. Teachings and support on purity and courtship

I totally had to put this down because our Church was big on this. In Youth Church, we were taught a lot about purity and courtship.

When I was around youth church members, it felt like a safe place for me. I didn’t feel judged for my decision to abstain, and we would openly talk about it.

Much later, we started to talk about courtship.

Some of the members of my youth church got married to each other and I smile every time when I see them flourishing in their marriages.

The Church really invested in lessons and bible studies on courtship! I felt sad when I left Kenya at this time because I missed these key lessons that came with it.

3. Engagement, Fun, and travel opportunities.

Youth Ministry in Church Activities

Some people think Church is low energy and boring and that perhaps leads them to look to the world for its idea of fun.

However, let me tell you……Youth Church is so much fun! Whether it’s youth church in Kenya or U.S.A, this rings 100% true! I can tell you that you will have many fun options when it comes to travelling, fun and engagement in general.

I remember we used to have other churches from other countries visit us and vice versa, and every youth member would fit in so well. We all wanted the same thing- engagement and fun.

The most important thing about this is the fact that we are in a safe space.

4. Critical Thinking Skills

In church camps, I remember we used to have numerous activities that would challenge us to think critically.

Our church leaders were very creative in organizing games and studies to allow us to apply biblical principles.

5. Healthy friendships

Being surrounded by other people with the same goals allowed me to be surrounded by healthy friendships. My church friends and I have been able to maintain a strong bond. This is because the love of God backs the friendship.

When I was in Church, I remember visiting friends who had lost loved ones, and we would collectively work with our church leaders to organize how we would adequately support them. This sets precedence on how we should treat friendships even as adults.

6. Responsibility and service!

Every church member can attest that there are opportunities to serve in Church. People can serve as youth ushers, camp leaders, choir members, etc.

Often, church leaders would ask for volunteers or even approach someone if they weren’t aware of their gifts.

So for sure, numerous church activities promote youth involvement.

7. Identity & Identifying gifts

Youth Church can be a great place to find one’s identity in Christ and identify their gifts too!

Over the course of a couple of years, I know we noticed people identify gifts of singing, leadership, organizing, etc. This is because we were constantly exposed to different opportunities that we could explore.

Sunday, January 1, 2023

HERI YA MWAKA MPYA RAFIKI YANGU

Heri ya mwaka mpya rafiki yangu, ndugu na jamaa yangu wa karibu. Ni siku 366 zimekatika tangu mwaka ulipoanza 2022, ndani ya siku hizi yapo mengi ambayo yametokea, mazuri, magumu yenye kuumiza, kufurahisha lakini yote kwa yote Mungu ni mwema kwa sababu hata katika nyakati zote Mungu bado anabaki kuwa nguzo na dereva wa maisha yetu hivyo tumshukuru Mungu kwa hali zote...

▪︎Mwaka ni zawadi kubwa sana ambayo Mungu humpa mwanadamu kwa lengo moja tu kuyakamilisha yale ambayo alikupangia kuyafanya hapa duniani, hivyo basi ukiona bado unapata nafasi ya kuingia mwaka mpya fahamu kuwa kuna jambo unapaswa kulifanya hapa duniani kwa ajili yako, familia, Taifa na jamii inayokuzunguka na ukamilifu wa hayo yote ni ukamilifu wa kusudi la Mungu ndani yako....
▪︎Hivyo mshukuru sana Mungu kwa neema hii kubwa lakini pia fahamu kubwa bado unadeni kubwa duniani ndiyo maana bado unaishi, pengine unaweza kujiuliza ni mara ngapi umesafiri lakini hata harufu ya ajali hukupata ni mara ngapi umeugua lakini ukapona,
▪︎ je ni mara ngapi umekosea lakini bado upo huru ?. Katika hayo yote kuna watu walisafiri lakini walirudi wakiwa kwenye masanduku, wapo waliougua hawakupona kabisa lakini wapo waliofanya kosa dogo lakini wapo gerezani au hata kuondolewa kazini au kupata adhabu kubwa ambayo imewaumiza sana.....

▪︎Cha msingi ni kutambua kuwa Mungu anapokuepusha na majanga au changamoto yeyote ile bado anakusudi na wewe hapa chini ya jua na mbingu.
▪︎ Fahamu kuwa una kusudi maalumu ambalo unapaswa kulitimiza kwa nguvu zote na Mungu atakusaidia sana...
▪︎Mwaka unapoanza ni vyema sana kupanga mipango na malengo yako kwa kuzingatia uwezo wa utekelezaji wake, hapa angalia je malengo haya ninayo panga ndani ya mwaka huu nitaweza kuyatimiza au nitajipa mzigo ambao siwezi kuufikisha hata robo ya malengo yenyewe.....
▪︎Kuweka mipango na malengo ni jambo rahisi sana lakini changamoto kubwa sana ni namna ya utekelezaji wa malengo na mipango hiyo. Unapozungumzia malengo au mipango ili itimie inahitaji sana viwezeshi ndiyo uone matokeo ya malengo hayo..
Mfano....
▪︎Ukipanga kujenga nyumba basi unahitaji kitu cha kwanza kabisa ni kuwa na fedha ambayo itaweza kusaidia wewe kuanza hatua ya pili baada ya kupanga malengo yako, kuamua pekee halitosis kama huna fedha za kulifanya lengo hilo kufanyika...
▪︎Malengo mengine hayahitaji fedha ila yanahitaji uelewa, utayari wa kutoka ndani mwako sio kwa sababu kuna mtu alikusukuma kuanza jambo hilo, kwa kufanya hivyo ni rahisi sana kutenda kwa ukamilifu na kwa kujitoa zaidi maana utafahamu nini ambacho unakifanya kwa sababu utakuwa umefanya utafiti wa kutosha na umejiridhisha kuwa jambo hili naweza kulibeba na kulifikisha kwa wakati na kwa ufanisi na ubora....
▪︎Mwanzo wa mwaka mara zote kila mtu huwa na hamasa, shauku na nguvu ya kupanga malengo na pengine kuanza kwa nguvu mno lakini baada ya miezi mitatu tu watu wengi huachana na malengo na mipango yao na kushika njia zingine kabisa ambazo hata hazikuwa kwenye mipango wala mlengo ya mwaka kabisa....

Hii inachangiwa sana na mambo kadhaa ambayo yamekuwa na athali hasi kwa watu wengi....

1. KUKOPI MIPANGO NA MALENGO.
▪︎Watu wengi hawana malengo ila wengi tunakopi mipango na malengo kutoka kwa watu wengine, umemsikia rafiki yako, mhamasishaji Fulani, umesoma kitabu Fulani ukaona malengo Fulani basi unapita nayo kama mwewe kaona kifaranga.
▪︎Malengo haya hayawezi kutimia kwa sababu hujui kwa kina juu ya malengo na mipango hiyo hivyo kama njia uiendayo hujui basi ni rahisi zaidi kupotea na kutokifika mahali unapokwenda maana pia hujui hata uendako....

2. KUHAMASIKA NA MWAKA MPYA...
▪︎Mwaka ni mabadiliko ya majira ambayo hubadilika kila baada ya miezi 12 lakini uhalisia wa maisha unabaki kuwa ni uleule tu kwamba maisha yanaendelea, mwaka mpya unapoanza wengi huhamasika sna kwamba nilikosea mwaka uliopita sasa naanza mwaka mpya ngoja nianze upya lakini wakati mwingine tunapoteza malengo endelevu kwa kigezo cha mwaka mpya hivyo kupoteza focus, hatupaswi kupanga mipango na malengo kwa hamasa ya mwaka mpya bali tupange malengo na mipango ya mwaka kwa nguvu ya kiuchumi, uwezo binafsi wa kibailojia na mazingirq ambayo unaishi.....

3. MIPANGO NA MALENGO YA KUWAFURAHISHA MARAFIKI ZETU...

▪︎Watu wanaweka malengo kwa lengo la kuwafurahisha ndugu, jamaa na marafiki, tusionekane watu tusio na malengo, hivyo mtu anaweka malengo ili akiulizwa na marafiki zake awe na neno la kusema nao ili asionekane ni mtu asiye na mipango wa dira ya mwaka.
NB....

Zipo sababu zingine nyingi ambazo zinapelekea kufeli kwa mipango na malengo ya watu wengi baada ya miezi mitatu au miezi sita tabgu mwaka kuanza.
▪︎Ushauri wangu kwa mwaka huu basi ni vyema sana kujitambua binafsi, kutambua uwezo wako wa kifedha, akili, nguvu ya utendaji na maarifa ya utekelezaji wa kila malengo unayopanga kila mwanzo wa mwaka.
▪︎Kuwa na malengo mazuri bila utekelezaji ndugu zangu ni kuichosha akili na nafsi bila sababu za msingi. Fanya malengo na mipango kwa urefu wa kamba yako, hakuna malengo bora kuliko malengo yako, ubora wa malengo ni matokeo ya mipango na malengo yako mwenyewe....
▪︎Usipange malengo kwa kufurahisha umma, panga malengo kwa kuzingatia uwezo, nguvu, eneo ulilopo, ujuzi maarifa na nafasi ya utekelezaji wa malengo hayo....

▪︎Kuna wakati unaweza kuwa na nguvu ya kifedha, mazingira lakini ukakosa muda wa kufuatilia malengo yako kwa sababu muda wako unaamuliwa na wajiri wako, hivyo set malengo na mipango kwa kuzingatia sana factors zote kwa maana ya Internal and external factors......
Panga malengo kwa kuzingatia sababu nyingi ambazo zinaleta ukamilifu wa kile unachotaka kukifanya kila mwaka....
▪︎Sio kila mwaka uweke malengo kuna mwaka unapaswa kukamilisha malengo yaliyosalia ya mwaka unaopinduka na hapo utajiona bora na mwenye manufaa hapa duniani....
Kumbuka...
Hakuna Malengo bora yasiyokuwa na matokeo chanya....
Heri ya mwaka mpya
Musa Zephania Mgema 
0755632375

Friday, October 28, 2022

It is an incredible opportunity to use our children, childhood stage  to lay the strongest foundations where we can start putting our blocks, kujenga ndoto na maono yao kwenye lile kusudi kubwa la Mungu.....
Maono ni mpango wa Mungu toka mwanzo, ndiyo maana ili kuyakamilisha maono hayo alitoa mtaji unaoitwa kipaji. Kipaji ni moja kati ya mtaji wenye thamani kubwa ulimwenguni, namna ya kutambua na kukipa thamani kipaji, ni rahisi zaidi kugeuza jangwa na kutoa maji na watu sio tu wakaanza kunywa bali wakaanza kuogelea na kufurahia, the treasure of wealth on this earth....
White people have discovered this very beautiful mining thus ndiyo maana wanatumia nguvu na fedha nyingi kuwekeza kwenye vipaji kwa kuhakikisha wanavipa thamani ambayo uwekezaji huo umekuwa na returns nzuri kuanzia kwa mtu mmoja hadi taifa kwa ujumla.....
Familia nyingi zimeondoka na umasikini kwa sababu ya kipaji kimoja ambacho waliamua kwa nia na dhati ya moyo kuwekeza na kujenga misuri ya malezi yenye tija kwa watoto na sasa wanakula matunda ya uwekezaji wao bila kutumia nguvu.....
The world 🌎 is a better place for dynamic people and is an he'll for those people who don't copy with the speed of the World. Myles Munroe hakukosea kusema familia nyingi zinateseka katika giza nene la umasikini kwa sababu ya kushindwa kutambua kuwa yard chache kutoka kwenye milango ya familia zao kuna utajiri mkubwa umerudi bila kutumika kwa kukosa mtu mwenye jicho la tatu la kubaini na kutoa sapoti ya kuvitambulisha katika dunia nankuvipa thamani.
Ufukara na umasikini wa kwanza kwenye maisha ya mtu haupo kwenye ukosefu wa pesa, mali bali  upo kwenye fikra na mtazamo wa mtu husika.. 
Ni rahisi zaidi mtu kukubali samaki mmoja mkononi ili kutibu tatizo la  njaa ya masaa machache kuliko kujifunza namna ya kusuka nyavu zitakazomfanya kuingia mwenyewe ziwani na kuvua samaki na kuondokana na ukosefu wa chakula kila siku....
Malezi bora ya mtoto ni kuwekeza kwenye jambo litakalokuwa na tija zaidi kwenye maisha yake na familia yake. Dunia ya sayansi na teknolojia imebadilika sana, na inahitaji value na Uniqueness ili kuweza kuifanya kuwa sehemu salama na bora ya kuishi  kizazi cha leo na kesho.....
Mifano michache ambayo inaweza kufungua fahamu za watu wengi ni kwa watu wachache ambao kupitia mapambano yao na kujua thamani ya vipaji vyao leo wanaishi katika level ambayo pengine pasikutambua thamani ya vipaji vyao leo hii wangekuwa watu wa kawaida au watu wenye dhiki na taabu duniani.
Kipaji ni zaidi ya kazi, kipaji ni zaidi ya kuingiza kipato, tunapozungumzia kipaji tunazungumzia FULL PACKAGE (KIFURUSHI KAMILI) ambapo ndani ya kifurushi hicho kuna vifurushi vingi vidogo vidogo vye thamani kubwa ambavyo kifurushi kimoja pekee kikitumika vizuri kinaweza kumfanya mtu kuishi maisha bora kwa zaidi ya miaka Mia moja. Mfano
Kama mwanangu ana kipaji cha kucheza mpira wa miguu na nimekilea katika makuzi na 
misingi bora ya soka basi kuna matokeo makubwa yafuatayo.... 

THE DIFFERENCE IS THE ONE NEEDED
Ulimwengu umebadilika sana, scarcity of products is no longer there, available of products have created a huge of supply in the marketplace while demand is going proportional with the supply, so people in the market has a wide range of options to buy whatever they need, so ili mtu uuze the same products katikati ya watu wanaofanya same business na wewe, bidhaa yako lazima iwe na kitu Fulani cha tofauti ambacho kitawafanya watu kukimbilia kwako na kuwaacha wenegine wenye same products 

Saturday, October 22, 2022

Siku moja nilimwona Baba yangu akilia kwa uchungu sana, halafu amechoka kwa kiwango cha kutia simanzi, moyo uliumia sana, nikashindwa kujizuia kulia. Ilikuwa ni kati ya nyakati ngumu sana kwangu kwa sababu sikutegemea kama kuna siku ningeweza kushuhudia machozi ya Baba yangu na huzuni na uchovu uliokamata mwili mzima...

Niliamini Baba yangu ni shujaa, mtu mwenye nguvu na uwezo wa kuhimili milima na mabonde ya maisha, mbele yake sikuona wasiwasi wala mashaka kwa sababu nilijua kuwa nae basi niko salama mno. Sikuwahi kuhisi unyonge, wala mnyong'onyeo wa kutisha kiasi kile kutoka kwa Baba yangu lakini ndiyo ilikuwa imeshakuwa, Baba yangu machozi mengi na unyonge mkubwa mno.

Ikipita siku kadhaa mbele yetu, nikiwa nimetoka shule  nikamkuta Baba yangu amekaa chini ya mti pale kwenye uwa wetu. Baba alikuwa amerejesha tabasamu, nia na shauku kubwa usoni pale, nikaijua kweli ndani yake na furaha njema usoni pake. Kwangu mimi ilikuwa ni nafasi muhimu na nyeti sana kuitumia kumuuliza Baba yangu kwa nini siku ile alikuwa analia kwa uchungu, mateso na maumivu makali kiasi kile....
Baba, samahani sana kama nitakuudhi,!
Bila samahani mwanangu na kijana wangu...
Kwa nini siku ile ulikuwa unalia sana, wakati sijawahi kukuzoea katika hali hiyo na wewe mara zote husema mtoto wa kiume ni shujaa na sipaswi kulia kwa sababu ya changamoto zozote zile.....
Mwanangu Joseph, kuwa uyaone, na ukiona mtu mzima analia basi jua jambo linalomsibu ni zito na amekosa ufumbuzi nalo.....
Kijana....kwa hiyo Baba siku ile ulikuwa unapitia jambo ambalo hukuwa na majawabu nalo...Baba, ukikuwa mwanangu utaielewa hii sentensi na utayakumbuka maneno yangu haya siku hii hapa chini ya mwembe wetu.....
Ni stori ya kija a mmoja kutoka kusini mwa Tanzania aliyoisema wakati akielezea maisha ya familia yake, hasa Baada ya Baba yake kupoteza mwelekeo wa maisha kwa kupoteza mali na utajiri ambao alikuwa amejikusanyia kwa muda mrefu....anasema zilikuwa ni nyakati ngumu kuwahi kuzishuhudia katika familia yetu pasina kutegemea kama maisha hayo yangekuwa sehemu ya maisha yetu.....
Nilizoea maisha mazuri mno, nilimzoea Baba kama mbeba majukumu, nilizoea kumwona Baba akiwa mwenye ujasiri, nguvu, mpanaji na mwenye kuiona nuru ya familia yake muda wote kwa sababu aliamini katika nguvu, uwezo na nafasi aliyokuwa nayo.......
Kijana anasema, machozi ya Baba ndiyo yalikuwa sababu ya mimi kuacha shule na kuingia mitaani kwenye manispaa ya Mtwara kuhakikisha, napambania familia yetu, Baba aliniambia nimefanya kila kitu kwa juhudi, ubunifu, kujitoa na kuongeza masaa ya kufanya kazi lakini kila kukicha afadhali ya jana, nimetoa sadaka, nimetoa muda wangu kwa mambo ya Mungu lakini ni kama nafukia mali zangu, nimefika mahali nimenyoosha mikono juu, sina namna nyingine inaweza kuwa jawabu la maswali magumu kichwani mwangu.....
Haya maneno ndiyo yalinifanya mimi Joseph kuacha shule nikiwa kidato cha pili nakuingia mtaani kwa sababu Baba yangu alikuwa ana elekea kuchanganyikiwa kwa sababu ya mapito magumu na maumivu ya moyo ambayo alikuwa akiyapitia kwa wakati huo.
Ni ngumu sana kunielewa kupitia maandishi haya leo lakini ni maumivu makali mno ambayo yaliingia kwenye moyo wangu wakati wakati mzee ananisimulia hali ya familia yetu ilivyokuwa kwa wakati huo. 
Mwanzo Baba aliuza gari akasema nataka kununua gari nyingine nzuri zaidi ya hii, baadae akauza baadhi ya viwanja na mashamba na kigezo anataka kufanya makubwa zaidi ya vile alivyokuwa. Kumbe wakati huo Baba alikuwa anapambana sana kulinda hadhi na nafasi aliyokuwa nayo katika jamii. Wakati anafanya yote hayo alikuwa katika hali nje ya ufahamu wake wa kawaida, na aliamini katika kila uwekezaji na fedha mkononi.....
Wakati anaendelea kufanya hivyo, alijikuta akipoteza mali, fedha na assets zote za familia akizani anarejesha utajiri na hadhi ya familia kumbe anapoteza vyote. It so sad. Baada ya stori nyingi zenye Simanzi na uchungu mwingi kutoka kwa Baba yangu. Giza lilitanda mbele yangu, njia ilikuwa ni giza nene, kwenye ule mkeka sikuiona kesho yangu kupitia shule, kwa sababu pia nilikuja kubaini kuwa muda si mrefu ningesitishiwa masomo kwa sababu ya kutokulipa ada.....
Maumivu ya Baba yangu alikuwa ndani ya moyo wangu na haya yote yakitokea nilikuwa na umri wa miaka 15 tu. Umri mdogo ambao sikupaswa kuyasikia kabisa, yalikuwa ni maumivu yenye mchanganyiko wa moto, misumari, na nyembe nyingi ndani ya moyo wangu.....
Usiku huo sikuwa na hata Lepe la usingizi kila nikilala, usingizi hakuna, ndipo nikajipa ujasiri wa kuacha shule immediately ili kuipambania familia yangu. Kesho mapema mno nikaingia mtaani, kuanza kutafuta pesa kwenye vijiwe mbalimbali, nia na lengo kuu kumwokoa, Baba yangu kutoka kwenye umasikini.......



Friday, September 23, 2022

(Wakolosai 1:13)


NYUMBANI

NAMNA YA KUUTAMBUA WITO WAKO
NAMNA YA KUUTAMBUA WITO WAKO
Wito ni nafasi anayopewa mtu na Mungu kwa ajili ya kutimiza kusudi fulani, kama vile Uinjilisti, Utume, Unabii, Ualimu, uchungaji, nje ya hao kuna kama Udaktari, Udereva, Uraisi, Ushonaji, Ufundi wa aina yoyote ile n.k. (Efeso 4:11-12)

- Kila mtu aliyezaliwa hapa duniani anawito wake maalumu ambao Mungu amemwitia.
- Mungu anaangalia kutimiza kusudi lake alilomwitia mwanadamu hapa duniani.(Yeremia 1:12)
- Ukifanya kitu nje ya wito wako huwa Mungu anakuwa hawezi kuwa sambamba nawe maana hajakuitia hicho.
- Watu wengi maisha yao ni magumu kwa sababu hawajajua wito waao maalumu hapa duniani.

Mojawapo ya Mambo yatakayokutambulisha Wito ulionao.

Kuungwa mkono na watu kwa kile unachokifanya. "Tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo na Kefa na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara" (Wagalatia 2:9)

            Unapofanya jambo halafu watu hawakuelewi elewi jaribu kujiuliza mara mbilimbili, maana mara nyingi udhaifu wako siyo rahisi kuutambua wewe mwenyewe huwa watu wa pembeni ndiyo wanaweza kuutambua. huwezi kufanya jambo lolote halaffu asiwepo mtu wa kusema hapa uko sawa au hapa hauko sawa. ni lazima wawepo wenye kukutia moyo tu! kama ni cha Mungu.

            kama wewe ni mshonaji au unafanya biashara, utaona wateja ni wengi sana kwako na bidhaa yako inapendwa kuliko sehemu zingine.


Kusikia amani na Furaha unapokuwa unafanya hiyo kazi au huduma.
"Kwa sababu Karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake" Rumi 11:29
"Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi na huzuni nayo" Mith 10:22
         haijarishi umeingia hasara kwa kutumia pesa yako kwenye hilo jambo au kama ni biashara, au ni huduma ya kiroho, mara nyingi hutaumia sana hata kama umepitishwa pagumu na ukatumia pesa yako.

Kuto kukata tamaa.
Mara nyingi hutajisikia kufedheka hata ukikutana na upinzani au vita, hutasikia kukata tamaa na kila ukijaribu kukata tamaa huwa unakosa amani kabisa ndani ya Moyo wako. kama unafanya biashara na ukaibiwa mtaji lakini ndani yako unasikia kuendelea tu kufanya hivyo, ujue huo ndiyo wito wako, usije ukajaribu kuingia kwenye ufundi au kufungua kanisa au kitu chochote nje na kile ulichosikia kukifanya. Wito wa daudi ilikuwa ni awe Mfalme, angalia vita iliyokuwepo kati yake yeye na Sauli lakini hakukata tamaa.
       Ukikata tamaa sehemu ambayo Mungu amekuweka makusudi na ukaenda sehemu nyingine huwezi kufanikiwa baraka za kimungu na Mungu hatakuwa upande wako katika kukutetea na kukupigania. si kwamba Mungu atakapokuweka hakutakuwa na vita, ila watakaopigana nawe watakuwa wanapigana na Mungu aliyekuweka hapo na uwe na uhakika watashindwa tu! lakini ukienda sehemu ambayo Mungu hajakuweka ujue watakaopigana nawe watakashunda kwani Mungu hayupo nawe.
        Fikiria sehemu ambayo wenzio wanasema ni ngumu sana kibiashara Mungu ndo anakwambia uende wewe, kama Isaka alivyoambiwa usiondoke hapa kwenda Misri baada yanjaa kutokea. Mwanzo 26.

Kukutukuza na kuinuliwa kupitia wito huo.
"Zawadi ya mtu humpatia nafasi; humleta mbele ya watu wakuu"
Kipaji au wito ulionao utakufanya upate marafiki wengi sana na wengine mpaka kwenda mpaka nchi za nje huko kwa ajili ya kile anachokifanya. kumbuka Suleiman hekima yake ilimfanya afahamike sana mpaka kwa mataifa jirani, Hivyo hata mkondo wa baraka unapitia kwenye wito wako. kama wewe ni muhubiri basi utaendelea kukaa karibu sana na wahubiri au watumishi mbalimbali, kama ni mwimbaji utajikuta unafahamika sana kwa watu.

Kufanikiwa vizuri kwa jambo hilo.
Mara nyingi huwa hutumii akili sana mpaka ukafanikisha vizuri jambomulitendalo, kwa mfano, mcheji mpira, fundi wa aina yoyote ile kama Mjenzi, fundi fenicha, n.k. unajikuta ukiifanya kazi yako inapendeza sana na kila mtu anaipenda sana.
        Kunawengine wanashona nguo kwa cherehani, wengine viatu, lakini katika ubora sana, huo ndio wito wako. upande wa huduma za kiroho ukakuta ukihubiri watu wengi wanaokoka, wanabarikiwa, wanaelewa, wanatamani uendelee kuongea tu, ujue huo ndiyo wito wako. yaani watu wasikwazike kwa kazi yako au waionekane hawajapenda. (Mkumbuke Dorkasi,