Friday, September 23, 2022

(Wakolosai 1:13)


NYUMBANI

NAMNA YA KUUTAMBUA WITO WAKO
NAMNA YA KUUTAMBUA WITO WAKO
Wito ni nafasi anayopewa mtu na Mungu kwa ajili ya kutimiza kusudi fulani, kama vile Uinjilisti, Utume, Unabii, Ualimu, uchungaji, nje ya hao kuna kama Udaktari, Udereva, Uraisi, Ushonaji, Ufundi wa aina yoyote ile n.k. (Efeso 4:11-12)

- Kila mtu aliyezaliwa hapa duniani anawito wake maalumu ambao Mungu amemwitia.
- Mungu anaangalia kutimiza kusudi lake alilomwitia mwanadamu hapa duniani.(Yeremia 1:12)
- Ukifanya kitu nje ya wito wako huwa Mungu anakuwa hawezi kuwa sambamba nawe maana hajakuitia hicho.
- Watu wengi maisha yao ni magumu kwa sababu hawajajua wito waao maalumu hapa duniani.

Mojawapo ya Mambo yatakayokutambulisha Wito ulionao.

Kuungwa mkono na watu kwa kile unachokifanya. "Tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo na Kefa na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara" (Wagalatia 2:9)

            Unapofanya jambo halafu watu hawakuelewi elewi jaribu kujiuliza mara mbilimbili, maana mara nyingi udhaifu wako siyo rahisi kuutambua wewe mwenyewe huwa watu wa pembeni ndiyo wanaweza kuutambua. huwezi kufanya jambo lolote halaffu asiwepo mtu wa kusema hapa uko sawa au hapa hauko sawa. ni lazima wawepo wenye kukutia moyo tu! kama ni cha Mungu.

            kama wewe ni mshonaji au unafanya biashara, utaona wateja ni wengi sana kwako na bidhaa yako inapendwa kuliko sehemu zingine.


Kusikia amani na Furaha unapokuwa unafanya hiyo kazi au huduma.
"Kwa sababu Karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake" Rumi 11:29
"Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi na huzuni nayo" Mith 10:22
         haijarishi umeingia hasara kwa kutumia pesa yako kwenye hilo jambo au kama ni biashara, au ni huduma ya kiroho, mara nyingi hutaumia sana hata kama umepitishwa pagumu na ukatumia pesa yako.

Kuto kukata tamaa.
Mara nyingi hutajisikia kufedheka hata ukikutana na upinzani au vita, hutasikia kukata tamaa na kila ukijaribu kukata tamaa huwa unakosa amani kabisa ndani ya Moyo wako. kama unafanya biashara na ukaibiwa mtaji lakini ndani yako unasikia kuendelea tu kufanya hivyo, ujue huo ndiyo wito wako, usije ukajaribu kuingia kwenye ufundi au kufungua kanisa au kitu chochote nje na kile ulichosikia kukifanya. Wito wa daudi ilikuwa ni awe Mfalme, angalia vita iliyokuwepo kati yake yeye na Sauli lakini hakukata tamaa.
       Ukikata tamaa sehemu ambayo Mungu amekuweka makusudi na ukaenda sehemu nyingine huwezi kufanikiwa baraka za kimungu na Mungu hatakuwa upande wako katika kukutetea na kukupigania. si kwamba Mungu atakapokuweka hakutakuwa na vita, ila watakaopigana nawe watakuwa wanapigana na Mungu aliyekuweka hapo na uwe na uhakika watashindwa tu! lakini ukienda sehemu ambayo Mungu hajakuweka ujue watakaopigana nawe watakashunda kwani Mungu hayupo nawe.
        Fikiria sehemu ambayo wenzio wanasema ni ngumu sana kibiashara Mungu ndo anakwambia uende wewe, kama Isaka alivyoambiwa usiondoke hapa kwenda Misri baada yanjaa kutokea. Mwanzo 26.

Kukutukuza na kuinuliwa kupitia wito huo.
"Zawadi ya mtu humpatia nafasi; humleta mbele ya watu wakuu"
Kipaji au wito ulionao utakufanya upate marafiki wengi sana na wengine mpaka kwenda mpaka nchi za nje huko kwa ajili ya kile anachokifanya. kumbuka Suleiman hekima yake ilimfanya afahamike sana mpaka kwa mataifa jirani, Hivyo hata mkondo wa baraka unapitia kwenye wito wako. kama wewe ni muhubiri basi utaendelea kukaa karibu sana na wahubiri au watumishi mbalimbali, kama ni mwimbaji utajikuta unafahamika sana kwa watu.

Kufanikiwa vizuri kwa jambo hilo.
Mara nyingi huwa hutumii akili sana mpaka ukafanikisha vizuri jambomulitendalo, kwa mfano, mcheji mpira, fundi wa aina yoyote ile kama Mjenzi, fundi fenicha, n.k. unajikuta ukiifanya kazi yako inapendeza sana na kila mtu anaipenda sana.
        Kunawengine wanashona nguo kwa cherehani, wengine viatu, lakini katika ubora sana, huo ndio wito wako. upande wa huduma za kiroho ukakuta ukihubiri watu wengi wanaokoka, wanabarikiwa, wanaelewa, wanatamani uendelee kuongea tu, ujue huo ndiyo wito wako. yaani watu wasikwazike kwa kazi yako au waionekane hawajapenda. (Mkumbuke Dorkasi, 

No comments:

Post a Comment