Wednesday, September 7, 2022

SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ULIMWENGU WA MASOKO NA MAHUSIANO KATIKA BIASHARA 1.

Miaka ya nyuma, Tanzania na ulimwengu mzima, uliwekeza sana nguvu kwenye vitengo vya umma, kwa maana ya ofsi za serikali na wakati mwingine taasisi binafsi ambazo hazikuwa na mlengo wa kibiashara. Vijana wengi walikwenda shule kwa lengo la kuajiriwa kwenye ofsi za serikali na taasisi mbalimbali ambazo zilikuwa zikijihusisha sana na masuala ya kusaidia jamii....

Lakini katika utandawazi na ukuaji wa teknolojia umekuja kubadilisha, mitazamo, mifumo ya maisha kwa namna ambayo dunia ilikuwa hajazoea hasa katika dunia ya tatu ambayo inabeba asilimia kubwa ya nchi masikini na duni kwa kiwango cha juu sana....

Mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamekuja wakati ambao, hakuna maandalizi wala mapokeo ya mfumo mpya wa maisha ambayo ndiyo yameshika hatamu na kuiendesha dunia kwa namna nyingine kabisa....

Wakati mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wanaipokea nchi hii kutoka kwa mwingereza mwaka 1961, asilimia kubwa ya watu katika Tanganyika walikuwa hawana elimu zaidi ya elimu ya ujuzi katika uchongaji vifaa mbalimbali kwa kutumia mikono yao na vifaa vichache ambavyo walivigundua. Hii ni kwa sababu katika kipindi cha ukoloni elimu ilitolewa kwa uchache saba hasa kwa watoto wa machifu na baadhi ya watu ambao walikuwa wakisaidia mawasiliano kati ya mkoloni na mtu mweusi......

Hivyo hata baada ya uhuru mfumo wa elimu, uliendelea kutolewa kwa mlengo wa kwenda kutumikia taasisi na serikali, watu walifundishwa elimu kwa lengo la kutumikia serikali na sivyo ilivyo leo ambapo duniani inamwitaji msomi kwenda kupngeza thamani kwenye kile ambacho tayari wengine wameshakifanya au kugundua kitu kipya  tofauti na miaka hiyo ambayo mwajiriwa alikwenda kufanya kazi ambayo tayari inafahamika inapaswa kufanywa kwa namna gani ili kufikia malengo...

Miaka imesogea, ujamaa ambao mwalimu Nyerere aliuhubiri na kuusisitiza kwa nguvu nyingi kwa miaka mingi umekosa nguvu mbele ya mfumo wa kikeptalisti, ambao unarahisishwa sana na kuongezeka kwa matumizi ya sayansi na vifaa vya kisasa ambavyo vinaifanya dunia kukimbia kwa kasi na kila mtu akiwa na shauku ya kutaka kuwa juu ya mwingine ukilinganisha na mfumo wa ujamaa ambao ulimwezesha kila mtu kupata sawa na mwingine hata kama hakustahili kupata jambo fulani.....

Ukuaji wa elimu nchini na ulimwengu mzima, unakuja na nguvu kubwa ya ufinyu wa ajira kwenye maofsi mengi, kuongezeka kwa matumizi ya mashine imekuwa miongoni mwa sababu kubwa ya wasomi wengi kukosa ajira kwenye mashirika ya serikali na mashirika binafsi, kwa sababu tu kazi za wengi zinamalizwa na matumizi ya mshine yenye uwezo wa kufanya majukumu ya watu wengi.
Wasomi kuongezeka, watu kuongezeka na mahitaji ya ajira kuwa juu yamepunguza sana ukamilifu wa mahitaji ya watu kwenye sokonla ajira, hivyo imepelekea watu wengi kubadili mwelekeo na mitazamo kwa moyo wa kupenda au wa kulazimishwa maana hakuna jinsi....

Mfumo wa kikeptalisti umejikita zaidi katika uzalishaji kwa maana ya biashara na uwekezaji kwenye viwanda vya manual na viwanda vya software na kila mtu anashauku ya kuwa juu kuliko mwingine. Sasa kutoka na mabadiliko hayo makubwa, watu wengi wamelazimika kuingia kwenye ujasirimali, biashara na kazi zingine nyingi nje ya ajira zinazoitwa rasmi, hii inakuja kwa watu wa kama zote, wasomi, wasio wasomi, walioajiriwa na wasioajiriwa. Hii ni mifumo ambayo inamlazimisha kila mtu kuishi kwenye nini duniani inataka sio wewe unataka nini....

Kutoka na hali hii kushamiri kwa nguvu, baadhi ya watu imewalazisha kuanza ujasirimali, biashara bila kujua ni kwa namna gani biashara inaendeshwa, ufanye nini ili kwenye ile biashara yako iweze kustawi na kudumu kwa muda mrefu na kuleta manufaa kwenye maisha....
Biashara nyingi zinaanzishwa lakini mwisho wa siku zinakufa au kukosa ustawi ambao ulitegemewa. Zipo sababu nyingi sana ambazo zinapelekea hali hiyo kuwa kubwa kiasi cha kutishia maisha ya watu kuwa kwenye umasikini wa kuogelea..

Baadhi ya sababu hizo ni....
1. Sababu za kimasoko..
2. Mitaji..
3. Uwekezaji usiokuwa na ufahamu ndani yake
Na mambo mengine mengi. Sasa ndugu Musa Zephania Mgema, msomi wa chuo kikuu kwenye masuala Mahusiano ya Umma na Masoko amekuandalia darasa huru ambalo kwa hakika litakupa jicho la tatu kwenye eneo la masoko kabla na baada ya kuanzisha baishara yako, unapaswa kufanya nini na ili kuifanya biashara yako ikuwe na kuongezeka kwa kiwango kikubwa na kukupa matokeo unayoyataka....

Kupitia 
Instagram ya @amaris_media1, 
Facebook page ya @Amaris Media 
Kwenye blog ya mosesmgema.blogspot.com na baadae tutakuwa na magroup ya WhatsApp, na twitter, LinkedIn na YouTube account basi tutakuwa na darasa huru lenye manufaa makubwa kwako wewe mfanyabiashara na mjasirimali...
Mgemamoses@gmail.com 
0755632375
0745311928
Karibu sana

No comments:

Post a Comment