Saturday, October 22, 2022

Siku moja nilimwona Baba yangu akilia kwa uchungu sana, halafu amechoka kwa kiwango cha kutia simanzi, moyo uliumia sana, nikashindwa kujizuia kulia. Ilikuwa ni kati ya nyakati ngumu sana kwangu kwa sababu sikutegemea kama kuna siku ningeweza kushuhudia machozi ya Baba yangu na huzuni na uchovu uliokamata mwili mzima...

Niliamini Baba yangu ni shujaa, mtu mwenye nguvu na uwezo wa kuhimili milima na mabonde ya maisha, mbele yake sikuona wasiwasi wala mashaka kwa sababu nilijua kuwa nae basi niko salama mno. Sikuwahi kuhisi unyonge, wala mnyong'onyeo wa kutisha kiasi kile kutoka kwa Baba yangu lakini ndiyo ilikuwa imeshakuwa, Baba yangu machozi mengi na unyonge mkubwa mno.

Ikipita siku kadhaa mbele yetu, nikiwa nimetoka shule  nikamkuta Baba yangu amekaa chini ya mti pale kwenye uwa wetu. Baba alikuwa amerejesha tabasamu, nia na shauku kubwa usoni pale, nikaijua kweli ndani yake na furaha njema usoni pake. Kwangu mimi ilikuwa ni nafasi muhimu na nyeti sana kuitumia kumuuliza Baba yangu kwa nini siku ile alikuwa analia kwa uchungu, mateso na maumivu makali kiasi kile....
Baba, samahani sana kama nitakuudhi,!
Bila samahani mwanangu na kijana wangu...
Kwa nini siku ile ulikuwa unalia sana, wakati sijawahi kukuzoea katika hali hiyo na wewe mara zote husema mtoto wa kiume ni shujaa na sipaswi kulia kwa sababu ya changamoto zozote zile.....
Mwanangu Joseph, kuwa uyaone, na ukiona mtu mzima analia basi jua jambo linalomsibu ni zito na amekosa ufumbuzi nalo.....
Kijana....kwa hiyo Baba siku ile ulikuwa unapitia jambo ambalo hukuwa na majawabu nalo...Baba, ukikuwa mwanangu utaielewa hii sentensi na utayakumbuka maneno yangu haya siku hii hapa chini ya mwembe wetu.....
Ni stori ya kija a mmoja kutoka kusini mwa Tanzania aliyoisema wakati akielezea maisha ya familia yake, hasa Baada ya Baba yake kupoteza mwelekeo wa maisha kwa kupoteza mali na utajiri ambao alikuwa amejikusanyia kwa muda mrefu....anasema zilikuwa ni nyakati ngumu kuwahi kuzishuhudia katika familia yetu pasina kutegemea kama maisha hayo yangekuwa sehemu ya maisha yetu.....
Nilizoea maisha mazuri mno, nilimzoea Baba kama mbeba majukumu, nilizoea kumwona Baba akiwa mwenye ujasiri, nguvu, mpanaji na mwenye kuiona nuru ya familia yake muda wote kwa sababu aliamini katika nguvu, uwezo na nafasi aliyokuwa nayo.......
Kijana anasema, machozi ya Baba ndiyo yalikuwa sababu ya mimi kuacha shule na kuingia mitaani kwenye manispaa ya Mtwara kuhakikisha, napambania familia yetu, Baba aliniambia nimefanya kila kitu kwa juhudi, ubunifu, kujitoa na kuongeza masaa ya kufanya kazi lakini kila kukicha afadhali ya jana, nimetoa sadaka, nimetoa muda wangu kwa mambo ya Mungu lakini ni kama nafukia mali zangu, nimefika mahali nimenyoosha mikono juu, sina namna nyingine inaweza kuwa jawabu la maswali magumu kichwani mwangu.....
Haya maneno ndiyo yalinifanya mimi Joseph kuacha shule nikiwa kidato cha pili nakuingia mtaani kwa sababu Baba yangu alikuwa ana elekea kuchanganyikiwa kwa sababu ya mapito magumu na maumivu ya moyo ambayo alikuwa akiyapitia kwa wakati huo.
Ni ngumu sana kunielewa kupitia maandishi haya leo lakini ni maumivu makali mno ambayo yaliingia kwenye moyo wangu wakati wakati mzee ananisimulia hali ya familia yetu ilivyokuwa kwa wakati huo. 
Mwanzo Baba aliuza gari akasema nataka kununua gari nyingine nzuri zaidi ya hii, baadae akauza baadhi ya viwanja na mashamba na kigezo anataka kufanya makubwa zaidi ya vile alivyokuwa. Kumbe wakati huo Baba alikuwa anapambana sana kulinda hadhi na nafasi aliyokuwa nayo katika jamii. Wakati anafanya yote hayo alikuwa katika hali nje ya ufahamu wake wa kawaida, na aliamini katika kila uwekezaji na fedha mkononi.....
Wakati anaendelea kufanya hivyo, alijikuta akipoteza mali, fedha na assets zote za familia akizani anarejesha utajiri na hadhi ya familia kumbe anapoteza vyote. It so sad. Baada ya stori nyingi zenye Simanzi na uchungu mwingi kutoka kwa Baba yangu. Giza lilitanda mbele yangu, njia ilikuwa ni giza nene, kwenye ule mkeka sikuiona kesho yangu kupitia shule, kwa sababu pia nilikuja kubaini kuwa muda si mrefu ningesitishiwa masomo kwa sababu ya kutokulipa ada.....
Maumivu ya Baba yangu alikuwa ndani ya moyo wangu na haya yote yakitokea nilikuwa na umri wa miaka 15 tu. Umri mdogo ambao sikupaswa kuyasikia kabisa, yalikuwa ni maumivu yenye mchanganyiko wa moto, misumari, na nyembe nyingi ndani ya moyo wangu.....
Usiku huo sikuwa na hata Lepe la usingizi kila nikilala, usingizi hakuna, ndipo nikajipa ujasiri wa kuacha shule immediately ili kuipambania familia yangu. Kesho mapema mno nikaingia mtaani, kuanza kutafuta pesa kwenye vijiwe mbalimbali, nia na lengo kuu kumwokoa, Baba yangu kutoka kwenye umasikini.......



No comments:

Post a Comment