Sunday, August 28, 2022

ROHO YA MATENGANO

Katika ulimwengu tulio nao leo, umekuwa ni ulimwengu wenye mkanganyiko na wenye taarifa nyingi zenye uhalisia na upotoshaji mwingi sana. Kuenea kwa maarifa kumeongeza uhalalishaji wa mambo mengi mabaya wenye lengo la kuhakikisha kuwa kila mtu anajitengenezea mazingira yakujinufaisha na kuishibisha nafsi yake....

Kutokana na kuongezeka kwa maarifa mengi duniani, mifumo mingi imeathiriwa na mabadiliko hayo kwa namna chanya na kwa namna hasi. Mfano kwenye upande chanya, watu wamerahisishiwa namna bora na nzuri ya kupata maarifa, ujuzi, na kuziona fursa, kujifunza maneno ya Mungu na kupata mafundisho kwa urahisi zaidi kutoka kwa watumishi wengi wa Mungu  kuliko kipindi cha nyuma kilichokuwa na ufinyu wa vyanzo vya maarifa....

Lakini pamoja na kuona manufaa mema ya kuongezeka kwa vyanzo vya maarifa, lakini kwenye upande wa mambo ya kiroho, kumekuwa na ongezeko kubwa sana la uasi, ujuaji, na watu kubeba maarifa machache yenye kujihalalishia baadhi ya mambo ambayo kiuhalisia ni chukizo na uasi mbele za Mungu...

Sio ajabu leo kumkuta mtumishi wa Mungu akiwa ameshikiria mstari toka kwenye Biblia ambao anautumia kama silaha ya kulinda maslahi yake binafsi. Ndiyo maana leo makanisani imekuwa ni jambo la kawaida kwa watu kufanya dhambi lakini hakuna mtu ambae anashughulika nao kama sehemu ya maonyo, kurejeshana, na kukumbushana kuwa baadhi ya mambo kama mkristo/wakristo hatupaswi kufanya kwa sababu ya kutunza moto katika madhabahu ya Mungu wetu...

Na kama ikitokea mtumishi wa Mungu akasimamia misingi ya kikristo basi anaonekana ni mtu mwenye ukengeufu, mtu mshamba, anajifanya yeye mtakatifu, anajiona, hajui kama ni kipindi cha neema, yeye ni adhabu tu, mtu asiye na huruma wala kuchukuliana na madhaifu ya watu. Na watu wamekuwa na baadhi yakujitetea na kujilinda kwa mlengo wa kuhalalisha yale wanayoyafanya mfano wa maandiko hayo ni......
Kutoka na ulimwengu kuzalisha watu wenye maarifa mengi, imechangaia kwa kiwango kikubwa sana, mioyo ya watu kuwa magumu, kiburi, hawapendi kuonywa, wanajiona wao ni bora wenye kujua na hawapaswi kuguswa wala kuelekezwa, ukiwagusa, wanajikunja, ukiwaonya hawaji kanisani au wanahama....

Nguvu hii yote inakuja kwa sababu ya kupngezeka kwa maarifa 

Tuesday, August 23, 2022

MWANAUME V MWANAMKE

Tangu misingi ya ulimwengu kuumbwa na Mungu alipofanya maamzi ya kumfanya mtu kwa mfano wake, imani ya kwanza kabisa aliiweka kwa mwanaume. Imani hiyo ilijengewa msingi imara sana ambao huwa sio rahisi kuyumbishwa kwa namna yoyote ile kwa sababu ya ile nguvu ya kuaminiwa na Mungu na kushirikishwa hata katika uumbaji.

Wakati Mungu anafanya uumbaji wa vitu mbalimbali duniani, mwisho kabisa alimuumba mtu, (mwanaume) na baada ya kumuumba alimpa mamlaka na uwezo wa kuumba pia na kwa kulidhibitisha hilo, Mungu alimpa Adamu nafasi yakuwaita wanyama na vitu vyote majina kwa niaba yake....
Kwa maana hiyo basi, mamlaka na nafasi ya kwanza ya Mungu kwa mwanadamu aliweka kwa mwanaume, wakati huo mwanamke hayupo kabisa na wala wazo la yeye kuwepo duniani halikuwepo. Mwanamke amekuja duniani kwa sababu ya hitaji la Adamu ambae ni mwanaume, upweke katika ile bustani, Mungu akaona vyema ampe mtu ambae wanaweza kuishi pamoja na kushirikiana..

Kwa kifupi ni kwamba, Mwanamke asingeweza kuwepo kama either kungekuwa na njia mbili ambazo angepewa Adamu kama machaguo ya kuondoa Upweke wake pale bustanini, labda Angelina maamzi ya kuchagua kile kitu cha pili badala ya mwanamke.
Lakini kwa sababu Mungu alitoa chaguo moja na kulifanya chaguo hilo kuwa hitaji la mwanaume, basi mwanamke akawa ametoka na kuwa sehemu ya maisha ya mwanaume hata sasa...
Ndiyo maana leo ni rahisi zaidi mwanamke kuishi pekee yake baada ya mume wake wa kwanza kuondoka kuliko mwanaume na hata huyu mwanaume akiamua kuishi pekee yake baada ya mke kuondoka, jamiii na viongozi wa dini wanaweza kuwa sehemu ya kumshawishi ili kufanya maamzi ya kuoa tena kwa sababu si tu kuoa na kuzaa bali mwanaume kuishi na mwanamke ni hitaji maalumu sana...

Maaana yake ni kwamba mwanaume alitengenezewa uhitaji na uhitaji huo ukawa kwenye eneo la kutatuliwa na mwanamke. Na kwa sababu hiyo basi ili kuongeza thamani ya mwanamke kwa mwanaume, Mungu aliweka nguvu na mamlaka, utulivu na kiwango kikubwa cha kufikiri ndani ya mwanaume kuliko mwanamke....
Kwa point hiyo ni rahisi zaidi mwanaume kulaumiwa kwa sababu ya jambo fulani kuharibika wakati yeye yupo, kuliko mwanamke mwenye nafasi, uwezo na nguvu ya kutatua jambo hilo kwa sababu tu, mwanamke ni kwa ajili yake lakini mwanaume ni kwa ajili ya familia na jamii.
Mwimbaji mmoja akasema, ukiona jambo linayumba mahali fahamu mwanaume hajatimiza wajibu wake sawasawa. Uwezo wa mwanaume kufikiri ni mkubwa mno ukilinganisha na uwezo wa mwanamke katika kufikiri. 
Watu wengi husema kuwa mwanamke ana kiwango na uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko mwanaume na akili nyingi sana lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanawake huwa hawafikiri bali huwa wanawaza. Na hapa ndipo kuna tofauti kati ya kuwaza na kufikiri na hapa hapa ndiyo njia panda ambayo inawatofautisha wanawake na wanaume...
Mfano, tatizo likitokea kwenye familia, mtoto ameungua maji ya moto wakati wazazi wako kazini, mfanyakazi wa ndani akapiga simu kwa Baba, Baba atasema mwandae umlete mjini utanikuta hapa hospital na fanya haraka, na kama huna hela ya nauli chukua bajaji au tax, utanikuta hapa nitalipa. Same scenario akifikishiwa mwanamke, jambo la kwanza atapaniki, hisia zitatangulia, atalia, atataka kujua ilikuwaje mpaka amwagikiwe maji, hapo hapo atakuwa anapanda bodaboda kwenda nyumbani umbali wa kilometa kadhaa, huku akigombeza mfanyakazi na kumlaumu, atapaniki, na akifika huko atafanya anachokijuq yeye, wakati huo akili yake ikiwa ina waza lile tatizo zaidi kuliko kufikiri namna ya kuondoa tatizo hilo...
Mwanamke anatawaliwa na hisia sana, anahamasika (Easy to be motivated) wakati mwanaume huwa anataka kulielewa jambo kwa undani na kufanya mchakato ndani ya akili yake, halafu baada ya kulipa hilo jambo kwa mapana na marefu huwa anakuwa Inspired kulifanya jambo hilo kwa ubora na kwa uhakika zaidi maana anakuwa amejipima na kujitathimini kuwa jambo hili liko ndani ya uwezo wangu au hapana...




Monday, August 22, 2022

THAMANI YA MWONEKANO...

Miaka ya nyuma kidogo, sikuwa najua sana thamani ya mtu hujengwa kwenye maeneo gani, nilifahamu kuwa ukiwa  na 

Tuesday, August 9, 2022

MALEZI, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA

Malezi ya watoto na vijana katika ulimwengu wa sasa imekuwa ni changamoto kubwa sana katika nchi yetu na bara zima la Afrika, hii inachangiwa na kiwango kikubwa cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambayo yanapelekea mwingiliano wa tamaduni kutoka taifa moja kwenda taifa jingine na bara moja na bara jingine...

Mwingiliano huu umekuwa ukichagizwa sana na dunia kuwa karibu sana na maisha ya watu kuliko namna ambavyo watu wa dunia ya tatu tulitegemea kwa kipindi kifupi namna hii, ndiyo maana kumekuwa na mapokeo tofauti tofauti na mitazamo tofauti tofauti juu ya uwepo huu wa mwingiliano wa kitamaduni na mila kutoka maeneo tofauti ya dunia yetu.

Mwingiliano huu wa kitamuduni na mila haujaletwa tu na kuhama hama  kwa watu kutoka eneo moja kwenda eneo jingine, njia ambayo kwa miaka mingi ndiyo ilikuwa inaleta mwingiliano wa watu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na lengo kuu lilikuwa ni kutafuta fursa za kibiashara zaidi kuliko miaka hii ya karne tuliyo nayo...

Mwingiliano umekuwa mkubwa kwa sababu ya sayansi na teknolojia ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa watu kupata taarifa kwa ukaribu na uharaka zaidi kupitia viganja vya mikono yao, mfano leo tuna Television na radio za mikononi, YouTube, mitandao ya kijamii ambayo imerahisisha watu kujifunza na kuona mambo mengi kupitia njia rahisi kabisa za upatikanaji wa taarifa zote ambazo mtu anahitaji kwa muda anao taka.

Kuwepo kwa mwingiliano huu wa tamaduni, desturi na mila, haujaanza leo, haujaanza leo kwa sababu mabadiliko ya duniani yamekuwa yakitokea tangu karne ya kwanza, hata leo, dunia ikipewa vifaa rahisishi zaidi ambavyo vinampa mwanadamu nafasi ya kurahisisha majukumu yake na kuyafanya kwa ufanisi zaidi ukilinganisha na enzi za kale.

Katika bara la Afrika malalamiko yamekuwa mengi zaidi hasa kutoka kwa wazazi na walezi, ambao kwa asilimia kubwa ni kama hawakujiandaa kuyapokea matokeo haya makubwa ya teknolojia, wengi wakisema kuwa mila, desturi na tamaduni za mwafrika zinaharibiwa na utamaduni wa kimagharibi, hii ni kutokana na tamaduni hizi kuwa na nguvu zaidi ukilinganisha na utamaduni wa mwafrika.

Wakati sisi tunapokea utamaduni wa kimagharibi, hatukujua kuwa tunaupokea, tulijua ni misaada na usaidizi wa kimaisha kumbe ndiyo tulikuwa tunatengeneza mazingira ya kukubali kuwa wanyonge, na daraja la mtawala na mtawaliwa lilikuwa linajengeka katika fikra ambazo kwetu hazikuwa tunduizi bali tulitazama misaada kwa wakati huo.

Miaka mingi nyuma kabla ya ukoloni, historia inaonyesha kuwa Waafrika walikuwa tayari wameshasogea katika ugunduzi wa vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumika katika kuwarahisishia utimizaji wa majukumu yao kwa kipindi hicho, tunaona ugunduzi wa moto, ugunduzi wa vifaa vya kilimo na Silaha na nyenzo nyingine nyingi ambazo zilikuwa zikitumika katika kuwarahisishia mambo yao..

Kuja kwa ukoloni ndipo changamoto ya kuruhusu mwingiliano wa kitamaduni ulipoanzia rasmi, na katika kipindi hicho utamaduni kutoka mabara mengine ulianza kuwa na nguvu zaidi kwa sababu tuliaminishwa kuwa tamaduni zetu zilikuwa na mahusiano ya kichawi na uabuduji wa mizimu isiyo na tija, hivyo walituletea utamaduni mpya ili kutustarabisha, kutokomboa na kutupa maisha mapya ambayo sio ya gizani kw akifupi walikuja kuleta mwanga katika giza...

Kwa hiyo tunachokiona leo ni matokeo ya michakato mingi ambayo ilianza karne nyingi nyuma mpaka kufika leo. Sasa kutokana na kukuwa kwa sayansi na teknolojia umekuja kukamilisha kazi ambayo ilikwisha kuanza siku nyingi na kwa sababu kama bara la Afrika tumeshindwa kujisimamia wenyewe kuanzia ngazi za utawala, biashara, matibabu na kiimani kwa muda mrefu ni vyema sasa kutambua kuwa sio rahisi kupingana na mabadiliko makubwa ambayo kwa asilimia kubwa sana yanachagizwa na ukuaji wa teknolojia...

Kupiga na kuona utamaduni wa kimagharibi kuwa ni mbaya leo sio sawa kwa sababu udhibiti wake ni mgumu sana, tunachopaswa kufanya sasa ni kuhakikisha kama nchi au bara linasimama kwa kujitegemea katika mambo ya uendeshaji wa mambo yake. Lakini je tuna hiyo nguvu ya kujitegemea kwa sasa au tutasubiri kwa miaka mingi zaidi ya hii tuliyoishi baada ya uhuru ?...

Mambo haya yanatokea leo kwa sababu ya kuongezeka kwa kitu kinaitwa mmomonyoko wa maadili hasa kwa watoto na vijana ambao wamekuwa wahanga zaidi wa mwingiliano wa tamaduni hizi kwa njia ya teknolojia. Kwangu mimi hii sio hoja kubwa sana kwa sasa, kwa sababu tumeshachelewa na udhibiti wake ni unategemea zaidi katika udhibiti wa mifumo ya kimitandao ambayo haitawapa watu access ya kupata taarifa wanazotaka kwa wakati wao bali iwe katika utaratibu wa kiinchi kama ambavyo baadhi ya nchi za kiarabu na baadhi ya nchi za Asia kuwa na mifumo yao inayojitegemea hivyo kuwa na uwezo wa udhibiti katika kuperuzi katika mitandao ya kijamii.

Lakini lazima tutambue kuwa kuishi kwenye utamaduni wa mwafrika pekee sio tija wala hakuna manufaa yeyote katika ulimwengu ambao tuko nao leo, leo nchi haiko katika uendeshaji wa mambo kwa mfumo wa kijamaa, kila mtu yupo na uhuru wa kufanya mambo yake mwenyewe, utamaduni huu wa kimagharibi hautulazimishi kuishi wao wanavyotaka bali sisi wenyewe tumeupokea na tunaufurahia sana kuliko hata wao kwa upande mmoja...

Lakini bado wanatuonyesha madhaifu mengi sana katika matumizi ya teknolojia, wenzetu wakitumia kwa manufaa makubwa ya kibiashara, na kazi sisi tumezigeuza platform hizi kuwa sehemu za kupeana mipasho na kuwekana wazi mambo yetu kwa maana ya taarifa za udaku..

Tutakuwa na mwendelezo wa kuelezea zaidi kiini cha lengo la makala hii katika toleo lijalo...
Moses Zephania Mgema 
0719110760, 0755632375
mgemamoses@gmail.com 
mosesmgema12.blogspot.com
moses_mgema on Instagram, twitter and Facebook 

Tuesday, August 2, 2022

Cover book/ Kava la kitabu

Dunia ya leo, inaishi kwenye aina Fulani ya mitazamo na kuthaminishana kutokana na kile mtu ambacho anaweza kuwa anakisikia zaidi kuliko kukaa chini na kufikiri kabla ya kusambaza habari, au kukijaji kitu. Nje ya kava la kitabu watu wamejikuta wakijipa majibu ambayo sio sahihi..

Story ya kichaa mmoja kwenye stand ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani, kando ya dambo la stand, mama mmoja aliyoenekana akiwa chakavu na mwenye kuishi maisha ya kuokota makopo na kula vyakula vya majalalani, kuvaa nguo chakavu na nywele ndefu zilizojaa uchafu mwingi...

Wengi kwa kumtazama walimwona ni kichaa, walimpita na kumsemea maneno mabovu, walimtazama kama mtu asie na thamani, mtu aliyepoteza dira ya maisha, value yake kama binadamu haikuwepo tena, lakini kumbe alikuwa ni mtu mwenye kazi yake kubwa na alikuwa kwenye kazi maalumu ambayo ilimlazimu kuishi katika hali hiyo, binadamu wasio jipa nafasi ya kufikiri walijipa majibu yao ambayo yalikuwa tofauti kabisa..

Ndivyo ilivyo kwetu, tumekuwa watu wepesi kuhukumu, kudharau watu, kuwaona watu hawana thamani, hawana tena mwelekeo wa maisha kwa sababu ya hali ya sasa kwa sababu mwonekano wao...

Wengine ni vijana wadogo tumeshindwa kuwaheshimu, tumeowaona ombaomba, watu wasio na maana dunia kwa sababu ya mwonekano wao, wengine wanatokeo familia duni, wengine wamekimbia familia zao kutokana na shida mbalimbali za kimaisha, wengine ni yatima hakuna aweza kuwashika mkono, wote hawa tunawaona watu wasio na malengo, watu wenye chembe chembe za wizi na udokozi...

Mitazamo yetu kwao ni mibaya, bahati mbaya hata tulio kulia mazingira kama hayo na leo Mungu ametupa nafasi, tumesahau kuwa hata sisi kuwa tulitokea huko, we don't value dhahabu chakavu kwa sababu haijapita kwenye moto bado.

Vijana wengi walio maliza vyuo, wapo wengi mitaani wakitafuta ajira, sio kwa sababu hawana mawazo mazuri ya biashara hapana ni kwa sababu mitaji ni changamoto kwao, ni sababu inawalazimisha kutafuta walau kazi ambayo itampa mshahara mzuri ambao utamwezesha yeye pamoja na familia yake, wadogo zake wanamwangalia kama kijana aliyetoka shule, kama kijana mwenye elimu, wazazi wametua mzigo kwake maana walimsomesha ili awasaidia, vijana hawa wanatafuta ajira ili kutatua changamoto za mapema sana...

Lakini kwa sababu ya kutembea mwonekano wa nje umechakaa sana, maisha ni magumu mno, maisha yamewapiga hawana tena mwonekano mzuri, yawezekana hata fedha ya kununulia walau mafuta mazuri hawana, kila kitu kwao ni kigumu ni matatizo juu ya matatizo.

Waungwana tunawaona hawafai tena kwa sababu ya mwonekano wao. Ukweli ni kwamba sio kila mtu anavyoonekana ndivyo alivyo, tusiwe wepesi kuwachukulia watu kwenye mitazamo yetu, we have to take time to study people so that we can know them in out by doing that ni rahisi zaidi kupata the best of a person....

Ni rahisi kumkuta mtu Ana mwongelewa mtu vibaya lakini ana ujasiri kana kwamba anamjua, wengine wanachukia watu bila sababu ya msingi, wengine wakisema huyu anatabia Fulani bila kuwa na uhakika na maneno hayo ila tu kwa sababu amesikia watu wakisema na yeye anabeba maneno hayo..

Watu wengi tumewavisha watu tabia ambazo sio zao, wapo wameitwa malaya, wengine wanaviburi wengine wachoyo, wabinafsi, wanajidai kwa sababu ya kutokupata nafasi ya kuwajua zaidi....

Sio rahisi kumfahamu mtu kwa kumwagilia, au kukutna nae kwa muda mchache, you need time, mtu hahitaji kuzungumzwa kwa kusikia story mtaani, hupaswa kumhukumu mtu kwa kusikia watu wanasema nini juu yake ni vyema kujiaminisha pia wewe kama wewe...

Ndiyo wengi wamejikuta wakipoteza watu wa muhimi zaidi kwa sababu ya mwonekano, na wamejikuta wakiingia kwenye mikono ya watu malaghai kwa sababu ya kutokujua na wengine kuvutiwa ba mwonekano wa nje...

Take time to know a person 
Usiishi kwa story za kusikia invest your time to know someone