Monday, February 7, 2022

Joel Nanauka, moja kati ya waandishi na wazungumzaji bora kabisa katika hadhara amewahi kusema kwamba " katika ulimwengu tulio nao, ulimwengu wa mitandao ya kijamii, watu wengi wanakuonyesha jambo/kitu wanachotka wao ukione sio kile unachotaka wewe kukiona 

Na mara nyingi tunachokiona katika social media ni matokeo ya michakato ya muda mrefu ambayo katu mtu huyo hawezi kushare na wewechakato mpaka kufikia level aliyofikia kwa wakati anaamua kushare matokeo ya alichokifanya.

Hali ya namna hii imekuwa chanzo kubwa sana kwa vijana wa leo ambao wamekuwa na shauku ya kumiliki vitu vyenye thamani kwa sababu tu wamemwona kijana mwenye rika Lao anamiliki baadhi ya vitu vyenye thamani kubwa...

Matokeo yake tumeishi kwa kupoteza focus na malengo ambayo tumekuwa tukijiwekea sisi, wenyewe kwa sababu tu kuna rafiki amekuwa akionyesha utajiri na thamani ya Mali zake ambazo wakati mwingine hatuna uhakika Mali hizo Americana kwa namna gani...

Changamoto hiyo imewafanya vijana wengi kupambania maisha kwa lengo la kuwa kama Fulani au kumiliki Mali Fulani ili aonekane ni.kijana mwelevu na mwenye akili ya maisha. Changamoto hii imegeuka kuwa sababu ya vijana wengi kupoteza maadili yao katika kazi walizoajiliwa, wamekuwa wakitumia nafasi zao vibaya kuiba Mali ya ofsi au ambayo ilipaswa kuwafikia watu.

Watu wamekuwa wakijiuza miili yao, kuuza madawa ya kulevya na kuiba lengo ikiwa ni kutengeneza hadhi (status) katika macho ya wengi wakodoleao mitandao  ya kijamii. Ndio maana leo ufasinisi wa kazi ni mdogo, heshimu ya nafasi zao ni ndogo.
Ni vyema vijana wenzangu tukasimama katika misingi ya uadilifu na kuacha kuishi ya kukopi katika mitandao ya kijamii, maisha ambayo sio halisi ni.maisha ya show off....

Ukitaka kuwa mkubwa ni vyema sana kuishi kwenye malengo yako.na kuhakikisha kuwa unayasimamia kwa asilimia kubwa, maana hapa.duniani we have an equal chance to make our life better 

No comments:

Post a Comment