Saturday, February 19, 2022

Akili ya mtu mweusi ambayo imeshindwa kujitegemea kwa miaka yote, akili ya mtu mweusi ambae reference  yake ni kwa mtu mweupe. Mtu mweusi yuko tayari kuwa mbwa katika nchi ya mtu mweupe, yuko kuwa mfungwa katika Geneva moja katika nchi ya mtu mweupe, kuliko kuwa mtu huru katika ardhi mama katika bara la Afrika...

Akili ya mtu mweusi ambae anaweza kucheka katika uso na meno 32 yote nje huku katikati ya moyo na roho yake vikipingana na kicheko chake mwenyewe. Ni ajabu sana

Ni miaka zaidi ya hamsini mataifa ya Afrika tangu yalipo dai uhuru wake kutoka kwa mtu mweupe. Waasisi na viongozi wa awali ambao waliona mwanadamu hakuumbwa ili kutawaliwa na kuamliwa mambo yake, kwa jambo na damu bila elimu, bila silaha, bila kuwa na minutes kubwa za kivita waliweza kumwondoa mkoloni nakuweza kuicha Afrika huru yenye kujitegemea nakufanya maamzi juu ya mali zake yenyewe 

Nyerere akiwa na fimbo yake, Nkwame Nkurumah kutoka nchi ya Ghana 🇬🇭, Jommo kenyatta pale kenya 🇰🇪, Milliton Obote pale nchi ya 🇺🇬 mpaka miaka ya kuelekea mwisho mwa 1990s alipokuja mzee mwenye busara hekima na maarifa mengi Nelson Mandela alimaarufu Madiba....

Wakatengeneza bara jipya nje ya ukoloni walijua maumivu yakutawaliwa na watu wa nje, walijua maendeleo ya Afrika yataletwa na waafrika wenyewe, walijua jirani hawezi kujenga kwa jirani yake hata akijenga atajengq either kwa kiwango cha chini au kwa lengo Fulani, walijua jirani anaweza kuwahudumia watoto wa mwafrika lakini hawezi kufanya kama ambavyo mama au Baba halisi atakavyofanya....

Baada ya uhuru, nchi nyingi katika bara la Afrika zimerudi kwenye ukoloni mambo leo, asilimia kubwa tunaamini cha mzungu au mchina ni bora kuliko check ndio maana leo sio ajabu kumkuta kijana akitamani kuwa mbwa katika bara ulaya, kutamani kuwa mfungwa katika magereza ya watu weupe pale London, Washington Dc, Berlin, Paris pale Milan au hata pale Amsterdam nchini uholanzi kuliko kuwa mtu huru katika ardhi ya muasisi Nyerere mwana wa kambarage....

Fikra mfu, fikra finyu, fikra mgando usioweza  kuona thamani yakuishi katika ardhi ya nyumbani kwa uhuru na kwa amani. Nakwenda ulaya kwa sababu nyumbani hakuna fursa za ajira, nakwenda ulaya kwa viongozi wa Afrika ni watu wa made all sana watu wanasahau kuwa kwa njama ya mtu mweupe Muamar Gaddafi alipoteza uhai, kwa njama za mtu mweupe, Robert Mugabe alionekana kituko mbele ya Waafrika wenzake kisa alikataa kuishi kwenye fikra za mtu mweupe....

Naikumbuka hadithi ya kijana wa kisukuma kutoka wilayani chato, kando ya ziwa Victoria aliyeamini kuwa sisi ni nchi tajiri, aliamini bila fedha za Mzungu Tanzania inaweza kusimama yenyewe, aliamini kama taifa na bara zima la Afrika hatustahili kuwa hapa tulips kwa sababu  ya Mali zenye thamani  kubwa duniani zimelala Afrika, aliamini utajiri katika bara ulaya, America na kwingineko ni kwa sababu ya Afrika....

Naitazama Tanzania yangu ambayo watu wake wamechagua aina Fulani ya maisha, nchi ya Nyerere imebaki kuwa nchi ya made madeal kwa viongozi, wanachi wake kuwa chawa wa viongozi, aina ya maisha tumechagua ni kuwaumiza wengi ili mimi binafsi nite mbele kwenye hama iliyotokana na kuwa chawa wa mtu Fulani....

Tumechagua kuwa chawa na watu wa vijiweni huku tukitoa lawama kwa watawala wa nchi, wabunge hawatimizi wajibu wao, viongozi wanakula nchi huku tukisahau kuwa hao hao tumewafanya kuwa miungu watu kwa kuwa machawa wao.....wakitupatia lak moja, mbili, tatu nk tunaona maisha tumeyawini na kuwa ni wajanja sana kuliko kawaida....

Sisi hao hao ndio wa kwanza kulaumu kuwa hospitality hakuna dawa, hakuna walimu katika mashule yetu na tunakuwa tuko seriously kama tuna pointi vile kumbe ugoro tupu.... tumechagua aina Fulani ya maisha ambayo hayana afya kwetu sisi na kwa kizazi kijacho....
Itaendelea...

No comments:

Post a Comment