Wednesday, February 9, 2022

AKILI SMART NI URITHI BORA

Urithi bora katika maisha ya mtu sio Mali, fedha, elimu. Nimejaribu kutafakari, kujifunza na kusoma watu wengi katika vipengere vingi kama kipengere cha kurithishwa au kupata mtaji wa fedha, wengine wamepata urithi bora wa elimu  na wana GPA kubwa, wengine wameachiwa biashara nzuri na kubwa, wengine wamepata kazi za kuajiriwa nzuri na zenye hadhi, wengine wameachiwa majumba na magari mengi nk..

Lakini watu wamezaliwa katika mazingira yenye giza nene na dim-witted kubwa la umasikini, walala njaa, nguo kwao ilikuwa ni urithi bora sana tena nguo zenye uchakavu wa kiwango cha kutisha, wengine hawakubahatika hata kupata malezi bora ya wazazi, elimu haikuwa sehemu yao sio kwa sababu waliamua kama wale vijana kutoka familia tajiri walioamua kwa matakwa yao kuchagua kutokwenda shule....

Aina na makundi yote haya mawili, nimegundua kuwa kutoka katika familia yenye uwezo, familia yenye kila kitu, sio sababu ya mtu kutoboa tundu la mafanikio. Ingekuwa hivyo wale manikins, kizazi chose katika mstari wa ukoo wao wangeusikia utajiri katika majirani zao, wangeona katika Television na kusikiliza kwa majirani zao....

Urithi bora hata kama umezaliwa nyikani, tamani kuwa na akili yenye akili sawa, akili yenye uwezo wa kuamua kwenda mabli, akili ambayo haisikitishwi na mahali ambapo umezaliwa, akili yenye kuona kuwa hata kama leo niko hapa kesho yangu yaweza kuwa bora sana kwa sababu nilizawaliwa kwa kusudi la Mungu....

Urithi bora wa mtoto sio elimu kwa sababu wapo watu wengi wenye elimu kwa viwango vya degree,  masters, PhD, wengine hata degree 100 lakini wayatendayo hayaendani na viwango vya elimu yao, wengi elimu imewafanya kuwa wa hovyo kuliko hata ya kabla yakuwa na elimu kubwa...

Wengi wameachiwa Mali nyingi za urithi lakini ziliwafanya kuwa watu wa hovyo. Baadhi yao walikuwa wacha Mungu kabla ya kupata urithi lakini Mali zemewabadilisha na kuwa watu wapumbavu na wasio faaa kwenye jamii hata kwenye familia zao....

Watu wengine wamepata fedha nyingi kwa mkupuo either kwa njia ya urithi, kwenye madini, kwenye ubashiri wa michezo ya kubashiri, wengine wana bidii ya kufanya kazi, wamepata fursa zenye hela nyingi katika biashara au katika kazi za kuajiliwa lakini zimewafanya kuwa watu wa hovyo na hofu ya Mungu sio sehemu yao tena....

Changamoto kubwa ambayo imekuwa ikitupata na watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa elimu ndio urithi bora, ni kweli lakini elimu hata ingekuwa bora kiasi gani lakini kama inaenda mahali sio sahihi ni sawa na ile habari ya kwenye Biblia ambayo Yesu aliitoa wakati akiwafundisha wanafunzi wake.

Kwamba kulikuwa na mpanzi ambaye alikuwa na mbegu zake, kwa mfano huo Yesu anasema kuwa mbegu zingine zilianguka njiani mahali penye wapita njia wengi, nyingine katika miamba hakuna rutuba, zingine kwenye miba zilisongwa na miiba, zingine kwenye udongo mzuri zikastawi vyema kabisa.....

Mbegu ni elimu na mtaji ni mzazi au mlezi na shamba ni mtoto anaepswa kupata elimu hiyo, lakini Changamoto kubwa inatokea pale shamba(mtoto)anakuwa ni ardhi ya Barabarani au akawa ni shamba lenye mwamba  mkubwa na mgumu....

Hapa hata kama mtaji mzazi/mlezi + mbolea ambayo ni mahitaji muhimu yakuwezesha elimu yawepo yote lakini kama hiyo mbolea na matunzo yanafanyika juu ya ardhi yenye mwamba au kando ya njia basi usitegemee matokeo bora kutoka kwenye ardhi ya namna hiyo....

Lakini kama elimu hiyo hiyo ikiienda kwa mtu sahihi yaani mtu mwenye ufahamu bora na mwenye kujua thamani ya kile mzazi anafanya basi huu ndio udongo mzuri ambao utaleta matokeo mazuri kuanzia kwa mtu husika, wazazi hata kwa taifa kutakuwa na manufaa na hatua nyingine kubwa ya maendeleo  kabisa....

Vivyo hivyo hata kwenye urithi wa Mali zingine, urithi ukienda kwa mtu smart mwenye ufahamu bora na mpana basi ni rahisi kuona hatua ya maendeleo katika zile Mali zinaongezeka. Ipo mifano hai ya kina Muhammed Dewji na wengine ambao walipata urithi na kuzitoa Mali zile kwenye kiwango walichopewa na kwenda hatua ya juu zaidi....

Smartness is the key of success 
Education is the factor to support and expose a personal to see opportunity in a third 👁 

Smartness can turned unproductive land to produce, take an example of John, who were taken to the desert 🏜  

Smartness is everything 

Moses_mgema 
0755632375
0719110760



No comments:

Post a Comment