Tuesday, January 8, 2019

KWA KILA JAMBO ANZA, TEMBEA NA MALIZA NA MUNGU.

Pamoja na maarifa, ujuzi, elimu, shauku, uwezo mkubwa wa kufanya kazi, bidii ya kufanya kazi bila kuchoka.

Haitoshi kwenda pekee yako na kujitegemea mwenyewe au watu wanaokuzunguka.

Fedha na kila aina ya rasimali ulizonazo haziwezi kukubeba katika kila jambo.

Ufanyaje sasa ?
Kwa kila jambo tembea na Mungu, mshirikishe Mungu, mwache Mungu awe kiongozi kwa kila kazi yako.

Ukitembea na Mungu hakika huwezi kuona unaanguka kibiashara au katika kazi zako kwa sababu yeye atasimama na kupigana  na maadui wa kazi zako.

Ukiwa Mwaminifu kwa Mungu kwa kutoa fungu la kumi, hakika Mungu ataibariki kazi ya mikono yako.

Ukiwa mwaminifu kwa Mungu, Mungu atakutetea wakati wa ukame wako.

Kumbuka Biblia inasema yeye alikujua kabla ya misingi ya dunia kuumbwa, kwa hiyo hatima ya maisha yako iko mikononi mwake.

Kwa hiyo hata alipokuumba aliweka kusudi na maono yake ndani yako ili uyatimize kwa utukufu wake.

Kwa hiyo unapaswa kufahamu kuwa mafanikio yote, maarifa yote, ujuzi wote na utajiri ulio nao ni kwa sababu Mungu alipanga maono yake kupitia wewe, na amekupa uwezo wa kujua na kutambua uwezo wako na wewe kufanyia kazi, fahamu huyo ni Mungu.

Usikubali kutembea pekee yako mwaka huu tembea na Mungu hakika utaona matunda mazuri kwa sababu Mungu atakuwa na wewe.
Wakati mwingine biashara, kazi zetu hazisimami kisawasawa kwa sababu tujiona kuwa tunaweza bila Mungu.

Tumejitegemea sana sisi pasipokujua kuwa wakutegemewa pekee ni Mungu

Jiepushe na watu ambao wanaushauri mbaya kuhusu Mungu, acha kutegemea mwadamu, mfano kwenda kwa waganga, maana Biblia inasema kwamba amtegemeae mwanadam amelaaniwa kabisa.
Kwa hiyo kila mmoja lazima amtegemee Mungu kwa akili yake yote.
Pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni zote zinazotakiwa kwenye kanuni za kazi bado kanuni kubwa na yenye nguvu basi ni kumtegemea Mungu
Yeye ndiye anajua hatima ya maisha yako.
Msingi wa mambo yote mema ni Mungu tu.

Barikiwa kwa kusoma ujumbe huu mwanzoni kabisa kwa mwaka huu
Mwaka huu tembea Na Mungu
Acha kutembea pekee yako.

Moses zephania Mgema
0755632375.
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam Tanzania

*-2019 Is the year of achievements-*

Sunday, January 6, 2019

MAISHA YA YESU DUNIANI NI PAKITI KAMILI YA MAISHA HAPA DUNIANI.

Habari,
Natumaini kila mmoja watu amepata neema nyingine ya upendeleo kuifikia siku ya leo akiwa mzima wa afya.

Nitoe pole kwa yeyote ambae anapitia changamoto yoyote ambayo inamnyima furaha yake ya kila siku.

Niende moja kwa moja kwenye somo la kwanza la mwaka huu tangu kuanza, naamini utakuwa msingi mzuri wa kuunza mwaka huu baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Somo letu kama linaposomeka katika kichwa cha habari, basi tuambane ili kuweza kufahamu nini hasa tunajifunza, lengo na nini matokeo yake baada ya kujifunza.

Yesu au Mesia sio jina geni kwa watu wote, ni mtu ambae alikuwepo duniani kwa hali ya mwili na aliishi kati ya maisha ya kwaida kabisa. Yesu alizaliwa kwa hali ya kawaida na akaishi kwa uhalisia wote wa dunia.

Na ndiyo sababu iliyonifanya kuja na somo hili kama msingi wa kila mtu ambae, ana shauku ya kuona ndoto, malengo, nia na matamanio yake yanatimia siku moja.

Yesu alikuwa na malengo ya yeye kuwepo duniani, na lengo kuu lilikuwa kuleta ukombozi wa maisha ya kiroho lakini hata katika mwili, lakini lengo kuu ilikuwa kukomboa watu waliokuwa wamepotea.
Hiyo ndiyo ilikuwa main purpose ya Yesu kuwepo duniani.
Pamoja na yote hayo, mimi nimejaribu kutafuta na kufikiri zaidi juu ya ujio wa Yesu duniani.

kusudi kuu la yeye kuja duniani linafahamika kwa kila mtu, lakini je ni hilo pekee ? hilo ni swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza zaidi.

Naufahamu uwezo wake, nguvu zake, mamlaka yake, uwezo wa kuona kesho kabla ya siku kufika lakini kwa nini alikubali kuja kufa huku duniani, je hapakuwa na njia nyingine ya ukombozi?.
Jibu hapana Yesu anajia nyingi ambazo zingemfanya kuikomboa dunia bila yeye kupata maumivu na mateso.
Kuna zaidi ya shughuli za kiroho zilizomfanya yesu kuja duniani. Na kama dunia ingemwelewa vizuri au ingeelewa vyema sababu zingine  zilizomlazimu yesu kuja duniani basi huyu pekee ndo angekuwa Role model wa wote.

Yesu ni pakiti kamili (Full package) ameenea kila kona ya maisha ya binadamu, anaemkubali na hata asiemkubali ila kiuhalisia Yesu anagusa kila kona na pembe ya maisha yetu.

Yesu ni mwalimu, na alikuja kufundisha uhalisia wa maisha ya duniani.

NAMNA GANI TUNAJIFUNZA KWAKE.
Lesson 1.
Yesu aliamini katika kufanya kazi kwa  bidii sana na kwa muda mrefu sana huku akiwa na focus na nia ya kufikia kile ambacho amedhamilia kukitimiza kwa siku. Ndiyo maana unaweza kuona kwenye mkusanyiko wa wanaume 500 na wanawake na watoto alilazimika kufanya muujiza watu wapate msosi palepale ili ratiba yake ya siku itimie hata kama ni usiku wa manane.
 
> Hapa tunajifunza kufanya kazi kwa bidii sana lakini kuhakikisha kila ratiba unapopanga mambo ya kufanya kwa siku, wiki, mwezi na hata mwaka lazima uhakikishe unapambana kutimiza ratiba ili kuepuka viporo, bora kuchelewa kurudi nyumbani lakini ukiwa umetimiza majukumu ya ratiba yako.
Lesson 2
Alipata habari ya kuumwa kwa lazaro rafiki yake, lakini tayari alikuwa kwenye ratiba ya mambo mengine aliyokuwa anayatimiza, kwa hiyo alilazimika kumaliza kwanza kazi zilizokuwa ndani ya ratiba yake ndo akaenda alikokuwa ameitwa.
Jiulize swali.
Je ni mara ngapi rafiki yako amekuondoa kwenye ratiba yako ?
    Majibu unayo wewe

>Hapa anatufundisha kuwa usikubali mtu awae yeyote kukuharibia au kuingilia ratiba yako pasipo sababu, hata kama kuna sababu ipime uzito wake kama unaona unaweza kuisolve hata kwa wakati mwingine basi timiza kwanza ratiba uliyonayo ili kuondoa uwezekano wa kuloose focus na concentration.
Ukikubali kila mtu aingilie ratiba yako na wewe umtimizie haja yake, basi wewe ni ngumu sana kufikia malengo kwa wakati ambao ulitazamia kutimiza. Maana mtu asiyekwenda na ratiba huyo ni kama bendera.
Kuna wakati unapokea taarifa ngumu ni vyema kutulia na kuonesha ukomavu, ukifanya hivyo basi utaipa akili kupumua vyema, hata unapoamua kufanya maamzi basi unatakuwa na asilimia kubwa ya kuamua vyema.
Lesson 3
Kutimiza malengo yako kwa wakati sio rahisi usipokuwa, mkomavu na mwenye nia ya dhati.
> pamoja na uwezo alokuwa nao lakini kuna wakati alikiri wazi kwamba yasingekuwa mapenzi ya Mungu basi yeye angeomba kikombe kimwepuke.

Maana yake nini kwenye maisha yetu ya kupambania ndoto zetu, kuna wakati unaona mlima mkubwa, huoni kama utaweza, kila unalofanya ni gumu lakini bado unapaswa kusimama kupambana ili kuvuka hapo

Hakuna mafanikio au kutimiza ndoto kirahisi lazima utoke jasho kweli kweli, no way ya kuepuka jambo hili.

4. Yesu anatufundisha kuvumilia sana kuna wakati mambo hayaendi, changamoto, unajisikia kuchoka, kukata tamaa lakini  bado hata kama hayo yanakuja bado unapaswa kupambana hata mwisho utakapoona umetoboa.

5.katika kila jambo unalofanya, watu watakudhihaki, kukusaliti, majungu, kukusengengenya, utaanguka au kutaitiwa mahali basi utasikia hata marafiki zako wakisema anajifanya eti mpambanaji basi ajitoe hapo alipokwama, wengine utasikia wanasema si alijifanya ana hela kwa sababu yeye ni mjasiriamali mbona siku hizi.....maneno mengi yote hayo yaache yapite ni upepo tu.

Mfano wa maisha ya Yesu
Wakati anachapwa mijeledi alithihakiwa, alitukanwa na kuambiwa kama yeye ni Mwana wa Mungu basi ajiokoe lakini hakutaka kuluzi focus kwa kuwajibu watu.

Lesson 6
Kupenda kile unachokifanya hata kama ni cha muda, maana yake nini hicho unachofanya ndiyo daraja la wewe kuifikia ile ndoto kubwa ya maisha yako.
Yesu alikubali kuja duniani lakini alikuwa anafahamu lengo ni nini. Alijua maisha ya duniani ni ya muda, pamoja na hayo aliithamini sana kazi yake hapa duniani, ndiyo maana leo tunamwita Mfalme wa wafalme.
Lesson 7.
Sio kila unachoombwa basi utoe, kuna wakati unapaswa kuwafundisha watu wanaokuomba namna yakufanya ili kuondoa jamu njiani wakati mwingine.

Yesu akawachia mwanafunzi wake kutoa pepo yeye akiwa hayupo, alitaka wajue na wawe na uwezo wa kujitegemea hata kama yeye hayupo. Hii ina jikita zaidi pale unapokuwa umefanikiwa, wengi hasa ndugu watakuja kukuomba fedha, wafundishe namna fedha inatafutwa.

Lesson 8.
Yesu ni mtoto wa tajiri ambae alikuja kuwafundisha masikini namna njema ya kuishi, hakuna lawama bali ni kufanya kazi bila kujali mazingira gani yanakukabili.

Alikuwa ni Mungu aliye uvaa utu ili kutufanya tujifunze kwa vitendo
Alifundisha pia yafuatayo
Kuwa na nia ya dhati.

General Lesson kwa mwaka huu 2019
Jitahidi sana kuwa wewe.
Fanya kazi zako bila kujali hali.
Focus kwenye malengo yako usipeperushwe na kelele za watu.
Fanya kwa bidii sana kila unapopata nafasi ya kufanya.
Simamia malengo yako.
Simamia ratiba zako.
Toa muda wa kujifunza na kuongeza maarifa ujuzi na taaluma mpya.
Fanya kazi kwa malengo na bidii
Baada ya yote.......
Kwa kila jambo Mungu ni wa kwanza.
Omba soma neno tafakari mtolee mungu kile kidogo anachokupa Mungu

Mwisho.
Yesu alikuja duniani kubadilisha fikra za watu kutoka mtazamo hasi mwenda Mtazamo chanya.
Mageuzi ya fikra yalianzia kwake.
Uaminifu na utii ndo yalikuwa maisha yake, hivyo yakupasa kuwa hivyo pia.
Kuthubutu hata kama huelewi, hata kama upo katika nchi ya ugeni mazingira   ni magumu
Yesu alikuja kukomboa
Roho
Fikra
Na ukombozi ulifanya katika aspects zote za maisha ya binadamu.
Mwaka huu ukawe mwaka wa mageuzi
Ya fikra, mitazamo na tuishi kwa malengo na targets huku tukimtumaini Mungu.

Mungu akubariki sana mwaka huu 2019 hasawewe uliemua kufanya kazi kwa bidii maarifa na ujuzi mwingi
Kwa utukufu wa Mungu utafanikiwa.

Prepared by:
Moses zephania Mgema
0755632375.
Mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam Tanzania

Wednesday, January 2, 2019

THAMANI YA WAZO LAKO.

Mungu amenissaidia, nmeamka salama kabisa. Nitoe pole kwa ndugu jamaa na marafiki ambao wanapitia changamoto mbalimbali, kwamba Mungu yupo atarejesha neema ya uzima au kuiondoa changamoto yoyote unayopitia sasa.
Mungu ni yule yule aliyemtendea Ayubu, lazaro na wengine, hata sisi pia lakini jambo jema ni kuendelea kumtumaini Mungu siku zote.

Leo ningependa tujifunze tena kitu muhimu na cha msingi sana hasa tunapoendelea na mchaka mchaka wa maisha ya kila siku.

Leo tutajifunza kitu kinaitwa        

*-THAMINI YA WAZO LAKO-*

Mungu wetu ni Mungu wa maarifa na maajabu mengi ambayo kiufupi tu hakuna mtu anaweza kuyaelewa zaidi ya kukiri tu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha yetu.

Mungu alituumba akatupa uwezo na akili yakuweza kutumia ili kuzitambua fursa na kuzitumia vyema kwa manufaa binafsi, familia, jamii lakini kwa ajili ya utukufu wake yeye Mungu.

Wazo  (Idea) ni moja ya silaha kubwa ambayo Mungu alimpatia mtu, na akampa uwezo wa kulinyumbua wazo hilo na kuwa faida kwake. Hapa ndipo tunaona watu wanagundua fursa mbalimbali zinazoendesha maisha yao.

Wazo (idea) ilimwijia Biligate, Wallace Wattle, mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg, wamiliki wa Twitter, whatsup, na mitaondao mingine ya kijamii hatimae leo tunatumia vitu hiv, Microsoft, Fb nk.  ni kati ya viungo vya mawasiliano ambavyo vimerahisisha sana njia za mawasiliano ukilinganisha na zama za kale.

Wazo la wagunduzi wa baiskel, pikipiki, gari, treni, meli na ndege, liligeuka kuwa fursa ambayo imeleta mageuzi makubwa sana kwenye nyanja za usafiri na usafirishaji.
Wazo ni kitu cha Thamani sana kama kikiheshimiwa na kupewa heshima yake, wazo hugeuza umasiki kuwa utajiri, wazo hugeuza woga kuwa ujasili, hapo ndipo tunapata watu waliojitoa muhanga bila kujal hadhi zao na leo ni watu wa mfano na matajiri duniani kote.

Kila jambo huanza kama wazo, liwe jambo baya au zuri lakini asili yake ni wazo moyoni na kwenye ufahamu wa mtu kabla halijaja katika ubayana wake.
Mpira wa miguu ulianzia nchini England kama wazo la wafanyakazi kujiburudisha baada ya kazi, lakini leo ni kati ya sekta inayozalisha ajira na utajiri mwingi kwa vijana na jamii kwa ujumla hapa (IDEA WAS IMPLEMENTED)

Mifano ni mingi mno ambayo tunaweza kuitumia, *-WALLACE WATTLE-* moja ya matajiri waliotokea kwenye familia masikini huko nchini marekani mwishoni mwa miaka ya 1880s hadi alipofariki dunia miaka ya 1900s aliwahi kusema, kila mtu ana wazo jema lakini namna ya kulitekeleza hilo wazo.

Watu duniani wana Mawazo mazuri sana na baadhi ya Mawazo ya watu masiki leo, yaliwahi kuwa ngazi ya watu matajiri duniani.
Kupitia vijiwe vya kawaha na vijiwe vya stori mawazo mengi huzalishwa na ni mawazo kuntu sana, shida iliyopo wale wanao zalisha mawazo hayo wengi wao hufanya ivo ili kunogesha vijiwe na kufanya siku iende wakalale.

Wachache sana wanaokuwa ndani ya vijiwe hivyo hung'amua mawazo hayo na kuyakusanya na kuyafanyia kazi na leo hawa matajiri tulio nao duniani na hapa Tanzania.
Hujawahi kupita mitaa ya jiji la Dar es salaam ukawasikia wazee wakisema huyu Bakhresa tulikuwaga tuko hapa anatuuzia kashata na kawa na wana feel proud kabisa kusema ivo, yawezekana ndani ya stori hizo kuna Mawazo bora kabisa Bakhresa aliyapata na kuyaboresha na leo yamemfanya kuwa  moja ya matajiri Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Nimekutana na mawakala na watu wengi wanaosema tulimpokea Shigongo alipotoka kwao Mwanza, na baadhi yao wanamwelezea kama mtu aliyekuwa duni sana lakini mwenye focus na malengo kwenye Idea yake.

Wengine wanasema waliuza naye magazeti,hata alipokuwa anaanzisha gazeti la uwazi akiwa hana kitu wengi wao walikuwa wanamtazama wanasema, wakati mwingine aliwaomba pesa ili kuzalishia gazeti la siku inayofuata na mengine mengi, lakini  leo Ndugu Shigongo ameajili zaidi ya watu mia kuanzia kwenye hotel zake, Global publishers, Global online Tv na vitega uchumi vyake vingine kama, Dar live mbagala ukumbi maarufu kabisa wa burudani.

Wazo ni kito cha Thamani sana, Je ni namna gani unaitumia, hakuna masikini duniani maana kila mtu ana wazo, wakati mwingine mawazo yetu ni bora kuliko waliofanikiwa, lakini hayaonekani bora kwa sababu hatujayaweka katika utekelezaji kwa kumaanisha toka ndani.

Wazo bila kuamua kulitekeleza ni sawa na midori ya wauza nguo sokoni kariakoo.
Amua leo bila kujali mazingira ya kiuchumi, kimaisha, nk. Amua kutoka moyoni.
Kufeli na kufaulu huwa ni maamzi ya mtu binafsi, ukiamua kufeli ni rahisi, ila ukiamua kufaulu au kufanikiwa ni maamzi magumu ya kutamani kutoka hapo ulipo kwenda eneo lingine.
Wazo ni jema pale tu unapolifanyia kazi kwa uaminifu, na kumaanisha, maisha yamekuwa na changamoto nyingi sana lakini hatuwez kuacha kupambana.
Kila mtu huwa na wazo, hivyo hakikisha unapopata wazo hilo lifanyie kazi immediately, bila kuchelewa, unapochelewa wengine wataliona na kulifanyia kazi.
Epuka kushirikisha ideas zako kama unaona kwamba bado huna uwezo wa kutekeleza kwa wakati huo, maana ukishare tu na watu, watu wenye nafasi zao watalitumia na wewe kubaki kwenye kushangaa.
Tumia wazo lako vyema, kuna wakati kama utakuwa na mawazo mazuri na huyatendei kazi basi kuna hatariya wewe kuumia kila siku kwa kuona watu wengine wakiyatumia mawazo yako
Heri ya mwaka mpya.
Moses zephania Mgema
0755632375
mgemamoses@gmail.com

ASANTE 2018, KARIBU SANA 2019

Mwaka 2018 umepita, tuna sababu ya kumshukuru Mungu sana kwa mengi mazuri aliyotutendea, mengi magumu aliyotuvusha, haikuwa rahisi hata kidogo maana ndugu jamaa, marafiki, majirani wameshindwa kuambatana nasi kwa kuunza mwaka huu.

Wengi wamefariki na wengine wameingia wakiwa wagonjwa na wengine wanapitia changamoto mbalimbali, lakini yote juu ya yote ni vyema kumshukuru Mungu tu.

Ni kwa neema wala sio kwa welevu, ujanja, ubora na utakatifu mwingi uliotufanya kuwa hai, is by Grace tu ndiyo maana tuko ndani ya mwaka huu tena, hakika ni kwa neema tu.

2019 tumeuanza kwa amani na furaha kubwa, wengi tukiwa na matumaini makubwa kwa kuset, mipango, malengo, shauku na hamasa ya kwamba mwaka huu basi ni mwaka ambao ni mwaka wa taofauti kabisa.

Kiuhalisia imekaaje, kiuhalisia kabisa kugeuza mwaka ni kama kulala na kuamka siku mpya, au kutoka mwezi mmoja kwenda mwezi mwingine in short ni mwendelezo wa maisha yaleyale tu.

Kwa kweli ndugu yangu tufanye kazi zaidi kuliko kuongea, mipango bila utekelezaji wa majukumu au wa mipango hiyo, kikawaida imekuwa ni mazoea ya kila unapoanza mwaka watu kupanga mipango na malengo, lakini kadri siku zikiwa zinasonga basi watu wanafunika diary zao na kusahau zile hamasa za mwanzo wa mwaka kabisa.

Kuanza mwaka sio kigezo cha wewe kubadilika kitabia na kimtazamo bali, maamzi ya dhati ya kuacha tabia za mazoea ndiyo kitu kinaweza kukufanya kufikia malengo ya kile ulichokifanya.

Pasipo Kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kuongea bila kutekeleza unachozungumza tutakuwa tunaanza na kumaliza miaka na miaka tukiwa kwenye tabia zilezile.

Lazima mabadiliko yaanzie kwenye fikra na maamzi ya dhati toka moyoni hapo ndipo unaweza kuona kweli mwaka umebadilika na uko tofauti na mwaka uliopita.

Katika kila jambo unalofanya mshirikishe Mungu, maana Mungu ndiyo  mwamzi na maratibu wa kila jambo tunalofanya, ni signatory wa kila jambo kwenye maisha yetu hakuna sababu ya kuishi bila kumtegemea Mungu.

Kufanya mambo ambayo yanamsikitisha mzazi wako basi jua Mungu anasikitika zaidi na hapo unajichumia laana utakuwa ukifanya mambo lakini hufanikiwi kumbe umeishi maisha yenye kumchukiza muumba wako.

God ni kila kitu fanya kila jambo kwa kumshirikisha Mungu, toa sadaka, fanya ibada, achana na waganga, na kuwategemea viumbe ambao pia kesho na kesho kutwa watakufa, na Biblia inasema amtegemeae mwanadam amelaaniwa achana na kuwategemea viumbe kama wewe.

Jifunze mara kwa mara ili kuujengea ubongo wako maarifa mengi kwa ajili ya matumizi yako binafsi na jamii.

Epuka mogogoro isiyo ya Lazima, hata kama ni ya lazima basi jitahidi kuepukana nayo kwa kila hali.

Samehe kwa kadili uwezavyo, ni afya ya akili nafsi na moyo, ukiombwa msamaha samehe, ukijua kuwa kila mtu anakosea, waweza kukosewa kama binadamu samehe maana hujui kesho yako wewe

Usiwe mtu wa kubeba mambo yasiyokuwa na faidia hata kidogo, kumbuka jambo likitokea limetokea huwezi kulifuta zaidi ya kusamehe tu.

Ushirika na wenzako liwe ni jambo la lazima kwa mwaka huu, baraka zingine za mafaniko zimefungwa kwenye ushirikiano na watu, kupitia ushirika mzuri na watu hapo ndipo unajenga connection na channels zingine ambazo huwezi zipata ukiwa pekee yako kama mkiwa jangwani.

Hekima, Busara  ni jambo jema kwa mwelekeo mzuri wa maisha yetu.

Nikutakie baraka za Bwana kwa mwaka huu, ukawe mwaka wa ushindi na utajiri kwa kila nyanja ya Maisha yako.

Kumbuka mkono mlegevu huleta umasikini bali mkono wenye bidii hutajilisha.
2019 Is the year of achievements
By
Moses zephania Mgema
0755632375