Sunday, November 18, 2018

MAISHA YA MAFANIKO HAYAHITAJI UDHURU.

Kuna wakati na nyakati unaweza ukawa unazipitia mpaka ukahisi hakika duniani kuna watu wamepangiwa kuwa na maisha mazuri na wengine maisha mabaya.

Maana kila jambo ambalo unakuwa unafanya ni kama haliendi kabisa daa....una kaa chini unawaza, unapanga mambo mengi lakini mwisho wa siku unaona ugumu kabla hata hujajaribu kufanya jambo lenyewe.

Ingawa kuna wakati unajitahidi  kufanya baadhi ya mambo lakini bado naamini hujajitoa kwa asilimia mia moja kabisa kufanya jambo hilo either kazini au kwenye biashara zako binafsi

Kitabu  kimoja niliwahi kukisoma kilichoandikwa na Brian aliandika mambo mengi sana ambayo kwa kweli binafsi yamenifikisha hapa nilipo leo japo bado sijafika ila kuna vitu tayari vimeanza kuthihirika kwangu baada ya kuanza kujitoa

Mwandishi Brian mwandishi wa Kitabu alielezea mambo mengi kwenye maeneo kama haya,  tabia za mtu ambazo zinamrudisha nyuma kufanya makubwa, ambazo kama tukikubali kuziacha leo na kuanza tabia mpya itaenda kutupelekea  Brian Amegusa umuhimu wa NIDHAMU BINAFSI na mambo ya kufanya ili uwe na hiyo nidhamu binafsi.

Kuna vitu au mambo kadha wa kadha ambayo ukiyafanya au ukiyabadilisha yawe katika mwelekeo chanya hakika kuna mwelekeo mwema utashika kwenye njia na mwelekeo wako wa mafanikio.

Unajua kuna vitu huanzia ndani namna unawaza, unafikiri na unavyotazama na kujigrede wewe kama wewe kule ndani. Yaani unajionaje, shauku ya moyo wako nini basi yote hayo yanaweza kuathiri matokeo ya nje either chanya au hasi.

Tutazame mambo haya kama yanaweza kuwa na manufaa kwako kama ambavyo yamefanikiwa kuwa na matokeo chanya kwa upande wangu.

Mafanikio yoyote yale ukiacha mitazamo, juhudi, maarifa na channel mbalimbali ambazo unazo basi ambatanisha na mambo yafuatayo kama ambavyo mwandishi amejaribu kuelezea kwa ufasaha.

1. Kiwango cha nidhamu kuanzia ndani inavyoweza kuathili hadi tabia yako ya maisha ya kila siku.

Nidhamu ni hali ya kuheshimu na kufuata ratiba, mipango na malengo yako ambayo umepanga kufanya kwa kipind fulani bila kujali changamoto yoyote ambayo unaweza kuwa inakukabili wakati unatekeleza mambo yaliyo ndani ya ratiba yako.

Katika mfumo wa maisha tulio nao kwenye karne hii, ili upate mafanikio lazima ujijengee nidhamu ya hali ya juu sana katika kutekeleza kila unalopanga, na lazima nidhamu uifanye kuwa msingi wako.

2. Tabia.
Nidhamu hujenga tabia, hivyo kama huna nidhamu utakuwa na tabia mbaya zisizo eleweka na ukiwa na nidhamu basi hakika utafikia malengo na ndoto zako.

Ukiona, huna ujasiri katika maisha yako, hujiamini katika kila unachokifanya basi jua wewe bado  ni mtu dhaifu sana, huwezi kuongea mbele za watu ukasikilizwa na kila unalofanya unaona unakosea, rudi nyuma ujitathimini upya. Jiulize je, ni mtu mwenye NIDHAMU katika mambo yangu ya kila siku ?

Tabia, ni kitu gani?
Ni mwenendo wa maisha yako, ni mjumuisho wa unachokisema na kukitenda kuanzia kwako binafsi hata mbele za watu tofauti tofauti bila kujali hadhi zao.

Mtu mwenye tabia bora, ni yule anae kiishi kile anacho kisema. Mfano kama unasema kesho nitaanza kutekeleza majukumu yangu saa moja asubui lazima kweli muda huo unapofika unapaswa kuwa kwenye eneo la kazi ili kwendana na muda ulio panga jana nje na hapo nidhamu yako itakuwa ya hovyo maana umeenda nje na mapatano yako mwenyewe.

Vile vile itamaanisha kuwa huwezi kuishi unachosema, na hiyo tabia ni mbaya na haitakufikisha kwenye mafanikio makubwa unayoyatamani

Njia pekee ya kujitengenezea sifa bora, ni kuwa na tabia bora lakini tabia bora msingi wake ni Nidhamu binafsi.

Nidhamu binafsi, Tabia bora, sifa njema, bidii, maarifa na ujuzi  hekima na busara maombi kwa Mungu wa kweli na Imani basi jawabu lake  ni mafanikio na matokeo makubwa.

Ukifanya yote hayo basi  hakuna wa kuzuia kufanikiwa kwako katika maisha. Lakini pia fahamu kuwa ukifanya bidii ofsini au kazini  kwako lazima upate promotion ya kupandishwa cheo. Kwenye  biashara yako lazima iwe na wateja wakutosha kabisa na utapata faida kubwa maana unatembea kwenye misingi ya nidhamu

3. Tabia njema inapelekea na  Uadilifu(Integrity). Ndugu yangu fahamu tunapozungumzia Nidhamu binafsi, siyo kitu kirahisi sana, ila ni kitu kinachowezekana hasa unapoamua kutoka ndani ya moyo wako kwa dhati.

Ukiweza kuwa na nidhamu binafsi lazima uwe mtu mwenye sifa njema kila unapokanyaga na itakujengea uadilifu wa hali ya juu kuanzia kwako wewe hata kwa watu wengine.

Nidhamu na Uadilifu ni kuwa mtu wa sura moja, yani ukisema hivi basi inakuwa hivi. Watu waone unafanya, ukimwahidi kitu aone unamfanyia kwa uwaminifu.

Mfano ulipoanza biashara, ulikuwaje ? Hebu jaribu kujitathimini, hivi wakati unaanza au kufungua biashara yako ulikuwa unawahi kufungua kauli njema kwa  wateja. Je leo bado uko hivyo?

Leo umebadilika sana umechoka huoni tena Thamani ya mteja umejawa na tamaa ya pesa unachoangalia ni pesa tu hakuna thamani ya mteja tena je utafika kwa mwenendo huo?

Nidhamu yako haipaswa kuwa ya muda wa uhitaji tu bali inapaswa kuwa mfumo wako wa maisha ya kila siku kwa kufanya hivyo basi hata misimgi ya biashara yako itaimarika sana. Lakini leo umekwisha sahau yote uliyokuwa unafanya mwanzo  unachelewa kufungua na wakwanza kufunga, unahifadhi bizaa zako ili mradi, hakuna mpangilio, umechoka umezoea kazi hakuna tena nidhamu.

4. Kipimo cha Tabia njema. 

Ili kujua kweli unachokisema ndiyo unachokiishi na ndiyo  tabia yako basi ni pale unapofanya kile unachokipanga kila siku kukufanya lakini pia muda nguvu, maarifa na ujuzi lazima kiendane na uzalishaji bora katika kila unachofanya.

Na kumbuka pia kuwa hata ukipita kwenye changamoto, tabia zako nzuri ziendelee au vilevile.
Swali ?

Je kwa mfano, ukipata hasara kwenye biashara, unaendelea kuwahi unawahudumia wateja vizuri, kuwahi kuamka , na kuiboresha biashara yako kama kipindi cha neema au kwa kuwa biashara imeyumba umeacha iwe hivyo hivyo ?

Mtu mwenye Tabia njema , hata apitie kwenye  changamoto zipi, bado mwenendo na mfumo wake wa maisha na tabia zake huwa hazibadiliki hata kidogo.

  Na mtu wa aina hii, kama leo akipata shida anarudi kwenye hali yake ya kawaida haraka sana na harakati za mafanikio zinaendelea, hivyo hata mafinikio yake ni makubwa sana.

5. Mambo matatu ya kutengeneza Tabia njema na imara.

a). Kujifunza kuishi tabia njema, kama uvumilivu, subira, upendo, kuchukuliana na kuwa mwaminifu. Na zaidi ya yote kuwa mkweli siku zote. Acha uongo, madhara yake ni makubwa na mabaya kuliko.

b).kuchagua watu bora ambao watakuwa kampani yako katika jamii na kuanza kuishi tabia zao.

c).Ishi tabia unazotaka kila siku.

Jambo la mwisho kwa siku ya leo.

Muundo wa utu na mifumo ya maisha ya kila siku.

Kama tulivyo ona mwanzo, Nidhamu binafsi ndio utu wako, sifa yako,na tabia yako pia.

Utu wako ni mjumuisho wa maeneo matatu,katika maeneo matatu.

1 Eneo la mfumo wa akili na mawazo yako.

Ni eneo la akili yako, ambalo limebeba mipango yako ya maisha, tabia bora unazotamani kuishi, thamani ya maisha yako na mambo ambayo unatamani kufanya ili kuwa mtu wa aina fulani unaye hitaji kuwa.

2.Mtazamo binafsi
Hili ni eneo la pili, namna unavyojiona wewe mwenyewe, mitazamo yako, je, unajiona ni mtu bora, mwenye faida kwa jamii, unaona uweza kufanya makubwa na kujiona una vitu vizuri kwajili ya wengine.

Ukisha jiona wewe bora, hakuna wa kukudharau, kila mtu atakuheshimu na utakuwa na ujasiri mkubwa sana mbele za watu, hata ukizungumza utaeleweka kwa urahisi kabisa.
Anza kutengeneza nguvu binafsi ya kuaminika na  wengine watakuona kufuatana na wewe unavyo jiona

3. kiwango cha kujipenda na kujikubali.
Ni kwa kiwango gani unajipenda mwenyewe, unajikubali, na kufanya mambo kwa ubora.

Jinsi gani unajielewa, unaijua mihemuko yako na kuweza kuidhibiti, unajua udhaifu wako, na kuweza kuutumia kwa faida na siyo hasara.

Hii itawafanya hata wengine wakupende na wakukubali sana.

Ila kama mwenyewe ni wa kwanza kujitukana, kujidharau, unajichukia, hakuna mwingine atakaye kupenda.

Maeneo hayo matatu yanatakiwa kutunzwa sana ndio utu wako, na ili kuweza kuyaishi vizuri, nidhamu haipingiki.

Leo, hii anza kujiuliza swali hili , Je je hivi kama kila mtu angekuwa kama mimi, hii dunia ingekuwa wapi ?

Kisha anza kubadilika,kwani kuna tabia unazo usingependa watu wengine wawe nazo, na kama watu wote wangekuwa kama wewe, basi dunia ingekuwa mahali pabaya zaidi mara nyingi  kuliko ilivyo leo.

Nikikukwaza nisamehe..ni hatua za kutaka tuwe bora zaidi.

Imeandikwa na
Moses z. Mgema
P.o.box.......
Dar es salaam Tanzania
mgemamoses@gmail.com
0755632375/0678355395
Kwa hisani ya kusoma vitabu vya kuongeza maarifa na utekelezaji

No comments:

Post a Comment