Friday, November 16, 2018

HAKUNA NAFASI YA UDHURU KAMA UNATAYATAKA MAFANIKIO

HAKUNA UDHURU KAMA UNATAKA KUFANIKIWA

Kuna mambo mengi sana kwenye Maisha yetu yanayoendelea kila mtu akipambana kuhakikisha maisha yake yanakuwa mazuri na yenye maana kubwa hasa kiuchumi, Kielimu, kiroho, eneo la Utawala na matumizi ya vipaji.

Sasa pamoja na mapambano yote hayo lipo daraja ambalo linatenganisha kati ya watu wanaofanikiwa na wasio fanikiwa japo watu wote tunaamka na tuna muda sawa wa kufanya kazi.

Pamoja nakuwa na muda sawa lakini ninachoamini kabisa kitu kinachotutofautisha hapa naamini ni mgawanyo wa muda na namna ambavyo tunaweza kupangilia namna ya utekelezaji wa majukumu yetu.

Mfano ukichukua kundi la watu ambao ndio wanaanza kiuchumi na wanafanana, na ukiwapa muda miaka miwili, utakuta kuna ambao wamepiga hatua zaidi na kubwa sana na wengine, wako palepale, je, unafikiri kuna uchawi hapo? Huwa tunaona kama wanabahati kwa kujitia moyo maisha ni foleni na sisi bahati yetu yaja.

Kila mtu anataka vitu vizuri ila kwa njia rahisi na za mkato, bila kujua maumivu yaliyopo nyuma yake.

Je, unataka kuongeza mauzo kwenye biashara mara dufu zaidi?, unataka kufanya ndoa yako kuwa bora zaidi?, unataka kujenga mahusiano bora zaidi? Unataka kuanza ukulima bora ?uwekezaji bora? , unampango wa kufikia uhuru wa kifedha na kustafu mapema?

Nini kina kuzuia kati ya unachojipanga kufanya na kuanza?

Huu, ndio mtego, anza kuutegua, kuvunja mara moja

Hapo ndipo kwenye shida, kwanza kabisa waafrika wengi tumejicholea mstari wa kutofanikiwa ila ni watu wenye kutamka kuwa  *siku moja, nitaanza* ? alafu pia *kesho nitaanzaa.....*

Utafiti unaonyesha 80% ya watu Duniani wapo kwenye *nitaa*  fanya, nitaanza, n.k.

Na 20% ni wale waliyofanikiwa, sana na wanachukua hatua kwa kila wanachopanga na kujifunza.

Kundi hili ni watu ambao wanapanga na kufanya.

Amua Leo,
  Kuendelea kusingizia, mambo ya nyuma, mazingira, ukosefu wa Elimu ,mara bosi simwelewi, ndoa inasumbua, sina kazi nzuri, sina shamba ila natamani kulima, natamani kufanya mauzo makubwa ila wateja hakuna, napenda kufikia uhuru wa kifedha ila, naona sina biashara kubwa* kama upo kwenye kundi la aina hiyo basi unajichelewesha, wewe ni moja kati ya watu wanaotakiwa kufanikiwa sana Duniani, kwani hata tunaofahamu wamefikia uhuru wa kifedha walikuwa na hizo sababu ila waliamua kuyakataa mazingira hayo na kutokuridhika nayo hata kidogo

   Amua leo  kutoka kwenye *Comfort zone* , kuachana na maisha ya watu wa kawaida, maisha ya mazoea, maisha ya kupanga kufanya, badala yake, *anza kuishi maisha ya kufanya.*  Jua hakuna mtu mbaya Duniani anaye jidanganya.

Amua.
  leo, kuwa chanzo cha mabadiliko kazini kwako, kwenye biashara yako,ndoa yako,familia yako,afya na elimu yako, kwa kuanza kufanya zaidi ya wengine, au kufanya vitu ambavyo wengine hawafanyi, kwa kuingia kwenye kundi la 20%.

  Tuangalie mambo 5 yakujifunza ambayo watu wengi waliofanikiwa waliyagusa ama kuyapitia kutokana na vitabu ambavyo nimekuwa nikisoma ambayo pia ni muhimu ukayajua ili either yakuasaidie kupiga  hatua kwenye safari ya maisha uliyonayo*

Kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kubwa kwenye kufikia mafanikio ni kukosa NIDHAMU BINAFSI.

Mafanikio kiuhalisia  yanaanzia kwenye nidhamu binafsi.

Aristotle aliwahi kusema, *nia kubwa ya maisha ni furaha*
Kama kila mtu ataweza kujiuliza nini afanye ili kuwa na hiyo furaha, hakuna mtu atashindwa kufanikiwa kiroho na kimwili.

1. *Pambanua maisha yako*

Unataka uwe mtu wa aina gani kazini, kwenye biashara, kwenye uongozi wako , ndoa au familia yako? , unataka kufanya kazi kampuni ya aina gani? Biashara yako unataka iweje, ? Je, unataka utengeneze kiasi gani cha pesa kwa sekunde, dakika, saa ,siku, wiki hata mwezi? Unataka kupunguza uzito? Kusafiri kwenda wapi?
  Jiulize maswali kujua nini unataka haswa.

Mfano, kama familia yako, ingekuwa na kila kitu, ungependa uishi wapi leo,? Upumzike hoteli gani? Usaidie watu wa aina gani, utembelee nchi zipi? Uwe na lifestyle ya aina gani?

Jiwazishe leo, kiuchumi,kiroho,kimahusiano,kiafya na kifikra ungependa uwe mtu wa aina gani?

2. Siyo kwamba watu hatujui nini,tufanye ili kuwa matajiri ila kukosa Nidhamu binafsi na kuwa na Excuses nyingi sana ndo sababu ya vile tunaishi leo.

Anza kuishi unachowaza kuanzia sasa, na kuzungukwa na watu unao wahitaji katika mazingira unayotaka.

3.Kanuni kubwa ya ulimwengu.

*Law of Cause and effects* inasema
Kwa kila matokeo kuna kisababishi, mfano kama unataka kufanikiwa katika eneo lolote la maisha yako, jua nini kinahitajika kufanikiwa na fanya hivyo kwa kurudia rudia kila siku.

Kama ni kuchelewa kula kwa sababu maalumu na kuwahi kuamka, basi fanya hivyo mpaka uyaone matokeo.

Jua, mafanikio yanatabilika, na wewe ndio  wa kuyatabili hayo mfanikio kwa tabia zako za kila siku, nini unafanya na nini hufanyi.

4. Siri ya mafanikio.

Lipa gharama, jifunze kwa waliyofanikiwa, anza kuwa yule unayemtaka, ishi tabia za kuwa bora kila siku

Acha maisha ya kawaida na historia, kila mtu anataka kufanikiwa ila siyo wengi wanajua tofauti ya waliyofanikiwa na waliyoshindwa, anza kujitofautisha leo.
Hutakufa kwa kuweka bidii ila utakufa kwa stress usipofikia malengo yako.

5.Jiulize maswali katika kila eneo la maisha yako, unayotaka mafanikio makubwa, *ni kipi ukikifanya kwa nidhamu maisha yako yataanza kubadilika mara moja?*

Ni mimi..
Moses zephania Mgema
0755632375
0678355394
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam,Tanzania

No comments:

Post a Comment