Saturday, November 3, 2018

JUA HAYA MAMBO MANNE ILI UFANYE BIASHARA YAKO KWA UFANISI.

kuna sababu nyingi sana zimekuwa zikichangia kuanguka kwa biashara na watu wengi bado hawajafahamu  sababu critical za wao kuanguka kibiashara hasa kwenye dunia ya tatu ambayo watu wengi ni kama tunaingia kwenye biashara kwa sababu hakuna namna nyingine ya kufanya ili kujiingizia kipato
Pamoja na sababu nyingine nyingi kama ukosefu wa elimu juu ya biashara, ujuzi, maarifa, ukosefu wa mitaji au kuanza na mitaji midogo, ukosefu wa uzoefu nk. Lakini kuna mambo haya muhimu sana kama unataka kufanikiwa kibiashara na ni vema ukazingatia sana.
Kuna kitu kinaitwa 4ps kwenye biashara yoyote ile.
Kwa Lugha ya kigeni zimebebwa kwenye kitu kinaitwa  (Marketing Mix )
Marketing Mix-Ni muunganiko wa sababu au mambo ambayo huwaratibiwa na kampuni au Taasisi ili kuhakikisha inatoa huduma kulingana na mahitaji ya wateja iliyowakusudia 

Tutaangalia mambo makuu manne 4ps ambazo mfanya biashara yoyote lazima uyazingatie ili kuifanya biashara yako idumu kwa kiwango kilekile au ikuwe zaidi.

1. Bidhaa  (products)- hiki ni kitu cha kuzingatia sana unapotaka kuanza kufanya biashara, sio kila bidhaa yafaa kuwa mahali fulani kwa sababu tu ulikuja au ulienda mahali ukakuta watu wanauza sana 

Jiulize je hii bidhaa pamoja nakuwa inauza sana hapa Dar je ni kweli singida kwetu inawatumiaji au inahitajika, Je katikati ya waislam kibanda cha kitimoto kitalipa, je baibui na kanzu katikati ya jamii ya kikiristo kitalipa, senene, michembe na bidhaa fulani inahitajika 

Kwa hiyo unapotaka kufanya biashara lazima uzingatie aina ya biashara unayotaka kuifanya kwenye eneo ambalo umeliona lina manufaa 

Kumbuka si kila fursa yafaa kutekelezeka kila mahali fursa zingine hazilipi kwenye eneo fulani hapa tuanachoangalia ni uhitaji wa kitu sio kila biashara ya dar ifanyike Arusha. Arusha tunaweza uza masweta, blanket lakini dar maji feni kwa sababu ya hali ya hewa.

2. Bei  (price) kitu kingine cha msingi sana kuzingatia unapotaka kufanya biashara. Hapa Lazima uangalie levels ya uchumi ya watu wa eneo husika je wanauwezo wa kumudu bei ya bidhaa yako, ukipeleka IPhone Singida, Manyara kigoma nk. Kwa asilimia ngapi wanamudu kununua IPhone yenye kuhitaji laki tano na kuendelea, ni kwel watu wanaipenda bidhaa lakini je wanaweza kumudu gharama za bidhaa hiyo

Lazima uzingatie kiwango cha uchumi cha eneo husika kabla hujapeleka bidhaa yako.usije anza kusema unalogwa kumbe ni wewe kushindwa kutambua level ya uchumi wa watu wa eneo la biashara yako

3. Eneo  (place)- Hii ni sababu ya msingi kuzingatia sana. mimi ntaanzia mbali kabisa kwamba Lazima eneo la biashara yako liwe karibu na wateja, Mazingira safi ambayo yatawavutia watu kuja, Mazingira Lazima yaweze kuwashawishi yaani eneo limtengenezee mtu sababu yakuja kununua kwako.kuna mambo sana ya kuzingatia kwenye uchaguzi wa eneo wataalamu wa masoko wametaja vitu vichache sana kwenye eneo hili ila Mimi naweza sema 

Eneo lako la biashara Lazima lijumuishe watu wa aina zote yaani wazima walemavu watoto eneo lako lazima liwazingatie sana maana wote ni wateja ukiacha mambo mengi ambayo yamezungumzwa na watu wa masoko 

Mazingira ya soko Lazima uyatengeze kwa namna yakumshawishi mtu kurudi tena na tena.

4. Promosheni (promotion) watu wengi huchanganya na wengi wanahisi ni gharama sana kufanya promotion hapana, promotion zipo za aina nyingi sana free promotion ambayo inaweza kuwa matumizi mazuri ya lugha kwa wateja kuwaja liwateja, kuchangamka kuwa na welcome face.

Kutumia zawadi ndogo ndogo kama pipi kwa watoto, kupitia mazingira safi yaweza kuwa means ya promotion. Achana na kutumia magari, media na vyombo vingine vya gharama ambavyo yawezekana huna mtaji wake.

Ivi sukari kwa sasa kilo unapata faida 1000 kwa mfano, na wengine wanauza bei hiyo hiyo kwa nini wewe usitoe hamsini au mia upate faida ya 900 shida iko wapi.

Lazima utumie akili na maarifa mengi ili kuifanya biashara yako kuwa stable na yenye kukuwa kila siku.

Kuna watu huona ugumu katika kila jambo ila mara nyingi sisi ndo tunatengeneza huo ugumu badilika nenda kisasa utafanikiwa 

Nimejaribu kutumia maelezo fulani ambayo sio kuntu sana ili uelewe vizuri 

MOSES MGEMA

0755632375

No comments:

Post a Comment