Sunday, November 18, 2018

MAISHA YA MAFANIKO HAYAHITAJI UDHURU.

Kuna wakati na nyakati unaweza ukawa unazipitia mpaka ukahisi hakika duniani kuna watu wamepangiwa kuwa na maisha mazuri na wengine maisha mabaya.

Maana kila jambo ambalo unakuwa unafanya ni kama haliendi kabisa daa....una kaa chini unawaza, unapanga mambo mengi lakini mwisho wa siku unaona ugumu kabla hata hujajaribu kufanya jambo lenyewe.

Ingawa kuna wakati unajitahidi  kufanya baadhi ya mambo lakini bado naamini hujajitoa kwa asilimia mia moja kabisa kufanya jambo hilo either kazini au kwenye biashara zako binafsi

Kitabu  kimoja niliwahi kukisoma kilichoandikwa na Brian aliandika mambo mengi sana ambayo kwa kweli binafsi yamenifikisha hapa nilipo leo japo bado sijafika ila kuna vitu tayari vimeanza kuthihirika kwangu baada ya kuanza kujitoa

Mwandishi Brian mwandishi wa Kitabu alielezea mambo mengi kwenye maeneo kama haya,  tabia za mtu ambazo zinamrudisha nyuma kufanya makubwa, ambazo kama tukikubali kuziacha leo na kuanza tabia mpya itaenda kutupelekea  Brian Amegusa umuhimu wa NIDHAMU BINAFSI na mambo ya kufanya ili uwe na hiyo nidhamu binafsi.

Kuna vitu au mambo kadha wa kadha ambayo ukiyafanya au ukiyabadilisha yawe katika mwelekeo chanya hakika kuna mwelekeo mwema utashika kwenye njia na mwelekeo wako wa mafanikio.

Unajua kuna vitu huanzia ndani namna unawaza, unafikiri na unavyotazama na kujigrede wewe kama wewe kule ndani. Yaani unajionaje, shauku ya moyo wako nini basi yote hayo yanaweza kuathiri matokeo ya nje either chanya au hasi.

Tutazame mambo haya kama yanaweza kuwa na manufaa kwako kama ambavyo yamefanikiwa kuwa na matokeo chanya kwa upande wangu.

Mafanikio yoyote yale ukiacha mitazamo, juhudi, maarifa na channel mbalimbali ambazo unazo basi ambatanisha na mambo yafuatayo kama ambavyo mwandishi amejaribu kuelezea kwa ufasaha.

1. Kiwango cha nidhamu kuanzia ndani inavyoweza kuathili hadi tabia yako ya maisha ya kila siku.

Nidhamu ni hali ya kuheshimu na kufuata ratiba, mipango na malengo yako ambayo umepanga kufanya kwa kipind fulani bila kujali changamoto yoyote ambayo unaweza kuwa inakukabili wakati unatekeleza mambo yaliyo ndani ya ratiba yako.

Katika mfumo wa maisha tulio nao kwenye karne hii, ili upate mafanikio lazima ujijengee nidhamu ya hali ya juu sana katika kutekeleza kila unalopanga, na lazima nidhamu uifanye kuwa msingi wako.

2. Tabia.
Nidhamu hujenga tabia, hivyo kama huna nidhamu utakuwa na tabia mbaya zisizo eleweka na ukiwa na nidhamu basi hakika utafikia malengo na ndoto zako.

Ukiona, huna ujasiri katika maisha yako, hujiamini katika kila unachokifanya basi jua wewe bado  ni mtu dhaifu sana, huwezi kuongea mbele za watu ukasikilizwa na kila unalofanya unaona unakosea, rudi nyuma ujitathimini upya. Jiulize je, ni mtu mwenye NIDHAMU katika mambo yangu ya kila siku ?

Tabia, ni kitu gani?
Ni mwenendo wa maisha yako, ni mjumuisho wa unachokisema na kukitenda kuanzia kwako binafsi hata mbele za watu tofauti tofauti bila kujali hadhi zao.

Mtu mwenye tabia bora, ni yule anae kiishi kile anacho kisema. Mfano kama unasema kesho nitaanza kutekeleza majukumu yangu saa moja asubui lazima kweli muda huo unapofika unapaswa kuwa kwenye eneo la kazi ili kwendana na muda ulio panga jana nje na hapo nidhamu yako itakuwa ya hovyo maana umeenda nje na mapatano yako mwenyewe.

Vile vile itamaanisha kuwa huwezi kuishi unachosema, na hiyo tabia ni mbaya na haitakufikisha kwenye mafanikio makubwa unayoyatamani

Njia pekee ya kujitengenezea sifa bora, ni kuwa na tabia bora lakini tabia bora msingi wake ni Nidhamu binafsi.

Nidhamu binafsi, Tabia bora, sifa njema, bidii, maarifa na ujuzi  hekima na busara maombi kwa Mungu wa kweli na Imani basi jawabu lake  ni mafanikio na matokeo makubwa.

Ukifanya yote hayo basi  hakuna wa kuzuia kufanikiwa kwako katika maisha. Lakini pia fahamu kuwa ukifanya bidii ofsini au kazini  kwako lazima upate promotion ya kupandishwa cheo. Kwenye  biashara yako lazima iwe na wateja wakutosha kabisa na utapata faida kubwa maana unatembea kwenye misingi ya nidhamu

3. Tabia njema inapelekea na  Uadilifu(Integrity). Ndugu yangu fahamu tunapozungumzia Nidhamu binafsi, siyo kitu kirahisi sana, ila ni kitu kinachowezekana hasa unapoamua kutoka ndani ya moyo wako kwa dhati.

Ukiweza kuwa na nidhamu binafsi lazima uwe mtu mwenye sifa njema kila unapokanyaga na itakujengea uadilifu wa hali ya juu kuanzia kwako wewe hata kwa watu wengine.

Nidhamu na Uadilifu ni kuwa mtu wa sura moja, yani ukisema hivi basi inakuwa hivi. Watu waone unafanya, ukimwahidi kitu aone unamfanyia kwa uwaminifu.

Mfano ulipoanza biashara, ulikuwaje ? Hebu jaribu kujitathimini, hivi wakati unaanza au kufungua biashara yako ulikuwa unawahi kufungua kauli njema kwa  wateja. Je leo bado uko hivyo?

Leo umebadilika sana umechoka huoni tena Thamani ya mteja umejawa na tamaa ya pesa unachoangalia ni pesa tu hakuna thamani ya mteja tena je utafika kwa mwenendo huo?

Nidhamu yako haipaswa kuwa ya muda wa uhitaji tu bali inapaswa kuwa mfumo wako wa maisha ya kila siku kwa kufanya hivyo basi hata misimgi ya biashara yako itaimarika sana. Lakini leo umekwisha sahau yote uliyokuwa unafanya mwanzo  unachelewa kufungua na wakwanza kufunga, unahifadhi bizaa zako ili mradi, hakuna mpangilio, umechoka umezoea kazi hakuna tena nidhamu.

4. Kipimo cha Tabia njema. 

Ili kujua kweli unachokisema ndiyo unachokiishi na ndiyo  tabia yako basi ni pale unapofanya kile unachokipanga kila siku kukufanya lakini pia muda nguvu, maarifa na ujuzi lazima kiendane na uzalishaji bora katika kila unachofanya.

Na kumbuka pia kuwa hata ukipita kwenye changamoto, tabia zako nzuri ziendelee au vilevile.
Swali ?

Je kwa mfano, ukipata hasara kwenye biashara, unaendelea kuwahi unawahudumia wateja vizuri, kuwahi kuamka , na kuiboresha biashara yako kama kipindi cha neema au kwa kuwa biashara imeyumba umeacha iwe hivyo hivyo ?

Mtu mwenye Tabia njema , hata apitie kwenye  changamoto zipi, bado mwenendo na mfumo wake wa maisha na tabia zake huwa hazibadiliki hata kidogo.

  Na mtu wa aina hii, kama leo akipata shida anarudi kwenye hali yake ya kawaida haraka sana na harakati za mafanikio zinaendelea, hivyo hata mafinikio yake ni makubwa sana.

5. Mambo matatu ya kutengeneza Tabia njema na imara.

a). Kujifunza kuishi tabia njema, kama uvumilivu, subira, upendo, kuchukuliana na kuwa mwaminifu. Na zaidi ya yote kuwa mkweli siku zote. Acha uongo, madhara yake ni makubwa na mabaya kuliko.

b).kuchagua watu bora ambao watakuwa kampani yako katika jamii na kuanza kuishi tabia zao.

c).Ishi tabia unazotaka kila siku.

Jambo la mwisho kwa siku ya leo.

Muundo wa utu na mifumo ya maisha ya kila siku.

Kama tulivyo ona mwanzo, Nidhamu binafsi ndio utu wako, sifa yako,na tabia yako pia.

Utu wako ni mjumuisho wa maeneo matatu,katika maeneo matatu.

1 Eneo la mfumo wa akili na mawazo yako.

Ni eneo la akili yako, ambalo limebeba mipango yako ya maisha, tabia bora unazotamani kuishi, thamani ya maisha yako na mambo ambayo unatamani kufanya ili kuwa mtu wa aina fulani unaye hitaji kuwa.

2.Mtazamo binafsi
Hili ni eneo la pili, namna unavyojiona wewe mwenyewe, mitazamo yako, je, unajiona ni mtu bora, mwenye faida kwa jamii, unaona uweza kufanya makubwa na kujiona una vitu vizuri kwajili ya wengine.

Ukisha jiona wewe bora, hakuna wa kukudharau, kila mtu atakuheshimu na utakuwa na ujasiri mkubwa sana mbele za watu, hata ukizungumza utaeleweka kwa urahisi kabisa.
Anza kutengeneza nguvu binafsi ya kuaminika na  wengine watakuona kufuatana na wewe unavyo jiona

3. kiwango cha kujipenda na kujikubali.
Ni kwa kiwango gani unajipenda mwenyewe, unajikubali, na kufanya mambo kwa ubora.

Jinsi gani unajielewa, unaijua mihemuko yako na kuweza kuidhibiti, unajua udhaifu wako, na kuweza kuutumia kwa faida na siyo hasara.

Hii itawafanya hata wengine wakupende na wakukubali sana.

Ila kama mwenyewe ni wa kwanza kujitukana, kujidharau, unajichukia, hakuna mwingine atakaye kupenda.

Maeneo hayo matatu yanatakiwa kutunzwa sana ndio utu wako, na ili kuweza kuyaishi vizuri, nidhamu haipingiki.

Leo, hii anza kujiuliza swali hili , Je je hivi kama kila mtu angekuwa kama mimi, hii dunia ingekuwa wapi ?

Kisha anza kubadilika,kwani kuna tabia unazo usingependa watu wengine wawe nazo, na kama watu wote wangekuwa kama wewe, basi dunia ingekuwa mahali pabaya zaidi mara nyingi  kuliko ilivyo leo.

Nikikukwaza nisamehe..ni hatua za kutaka tuwe bora zaidi.

Imeandikwa na
Moses z. Mgema
P.o.box.......
Dar es salaam Tanzania
mgemamoses@gmail.com
0755632375/0678355395
Kwa hisani ya kusoma vitabu vya kuongeza maarifa na utekelezaji

Friday, November 16, 2018

HAKUNA NAFASI YA UDHURU KAMA UNATAYATAKA MAFANIKIO

HAKUNA UDHURU KAMA UNATAKA KUFANIKIWA

Kuna mambo mengi sana kwenye Maisha yetu yanayoendelea kila mtu akipambana kuhakikisha maisha yake yanakuwa mazuri na yenye maana kubwa hasa kiuchumi, Kielimu, kiroho, eneo la Utawala na matumizi ya vipaji.

Sasa pamoja na mapambano yote hayo lipo daraja ambalo linatenganisha kati ya watu wanaofanikiwa na wasio fanikiwa japo watu wote tunaamka na tuna muda sawa wa kufanya kazi.

Pamoja nakuwa na muda sawa lakini ninachoamini kabisa kitu kinachotutofautisha hapa naamini ni mgawanyo wa muda na namna ambavyo tunaweza kupangilia namna ya utekelezaji wa majukumu yetu.

Mfano ukichukua kundi la watu ambao ndio wanaanza kiuchumi na wanafanana, na ukiwapa muda miaka miwili, utakuta kuna ambao wamepiga hatua zaidi na kubwa sana na wengine, wako palepale, je, unafikiri kuna uchawi hapo? Huwa tunaona kama wanabahati kwa kujitia moyo maisha ni foleni na sisi bahati yetu yaja.

Kila mtu anataka vitu vizuri ila kwa njia rahisi na za mkato, bila kujua maumivu yaliyopo nyuma yake.

Je, unataka kuongeza mauzo kwenye biashara mara dufu zaidi?, unataka kufanya ndoa yako kuwa bora zaidi?, unataka kujenga mahusiano bora zaidi? Unataka kuanza ukulima bora ?uwekezaji bora? , unampango wa kufikia uhuru wa kifedha na kustafu mapema?

Nini kina kuzuia kati ya unachojipanga kufanya na kuanza?

Huu, ndio mtego, anza kuutegua, kuvunja mara moja

Hapo ndipo kwenye shida, kwanza kabisa waafrika wengi tumejicholea mstari wa kutofanikiwa ila ni watu wenye kutamka kuwa  *siku moja, nitaanza* ? alafu pia *kesho nitaanzaa.....*

Utafiti unaonyesha 80% ya watu Duniani wapo kwenye *nitaa*  fanya, nitaanza, n.k.

Na 20% ni wale waliyofanikiwa, sana na wanachukua hatua kwa kila wanachopanga na kujifunza.

Kundi hili ni watu ambao wanapanga na kufanya.

Amua Leo,
  Kuendelea kusingizia, mambo ya nyuma, mazingira, ukosefu wa Elimu ,mara bosi simwelewi, ndoa inasumbua, sina kazi nzuri, sina shamba ila natamani kulima, natamani kufanya mauzo makubwa ila wateja hakuna, napenda kufikia uhuru wa kifedha ila, naona sina biashara kubwa* kama upo kwenye kundi la aina hiyo basi unajichelewesha, wewe ni moja kati ya watu wanaotakiwa kufanikiwa sana Duniani, kwani hata tunaofahamu wamefikia uhuru wa kifedha walikuwa na hizo sababu ila waliamua kuyakataa mazingira hayo na kutokuridhika nayo hata kidogo

   Amua leo  kutoka kwenye *Comfort zone* , kuachana na maisha ya watu wa kawaida, maisha ya mazoea, maisha ya kupanga kufanya, badala yake, *anza kuishi maisha ya kufanya.*  Jua hakuna mtu mbaya Duniani anaye jidanganya.

Amua.
  leo, kuwa chanzo cha mabadiliko kazini kwako, kwenye biashara yako,ndoa yako,familia yako,afya na elimu yako, kwa kuanza kufanya zaidi ya wengine, au kufanya vitu ambavyo wengine hawafanyi, kwa kuingia kwenye kundi la 20%.

  Tuangalie mambo 5 yakujifunza ambayo watu wengi waliofanikiwa waliyagusa ama kuyapitia kutokana na vitabu ambavyo nimekuwa nikisoma ambayo pia ni muhimu ukayajua ili either yakuasaidie kupiga  hatua kwenye safari ya maisha uliyonayo*

Kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kubwa kwenye kufikia mafanikio ni kukosa NIDHAMU BINAFSI.

Mafanikio kiuhalisia  yanaanzia kwenye nidhamu binafsi.

Aristotle aliwahi kusema, *nia kubwa ya maisha ni furaha*
Kama kila mtu ataweza kujiuliza nini afanye ili kuwa na hiyo furaha, hakuna mtu atashindwa kufanikiwa kiroho na kimwili.

1. *Pambanua maisha yako*

Unataka uwe mtu wa aina gani kazini, kwenye biashara, kwenye uongozi wako , ndoa au familia yako? , unataka kufanya kazi kampuni ya aina gani? Biashara yako unataka iweje, ? Je, unataka utengeneze kiasi gani cha pesa kwa sekunde, dakika, saa ,siku, wiki hata mwezi? Unataka kupunguza uzito? Kusafiri kwenda wapi?
  Jiulize maswali kujua nini unataka haswa.

Mfano, kama familia yako, ingekuwa na kila kitu, ungependa uishi wapi leo,? Upumzike hoteli gani? Usaidie watu wa aina gani, utembelee nchi zipi? Uwe na lifestyle ya aina gani?

Jiwazishe leo, kiuchumi,kiroho,kimahusiano,kiafya na kifikra ungependa uwe mtu wa aina gani?

2. Siyo kwamba watu hatujui nini,tufanye ili kuwa matajiri ila kukosa Nidhamu binafsi na kuwa na Excuses nyingi sana ndo sababu ya vile tunaishi leo.

Anza kuishi unachowaza kuanzia sasa, na kuzungukwa na watu unao wahitaji katika mazingira unayotaka.

3.Kanuni kubwa ya ulimwengu.

*Law of Cause and effects* inasema
Kwa kila matokeo kuna kisababishi, mfano kama unataka kufanikiwa katika eneo lolote la maisha yako, jua nini kinahitajika kufanikiwa na fanya hivyo kwa kurudia rudia kila siku.

Kama ni kuchelewa kula kwa sababu maalumu na kuwahi kuamka, basi fanya hivyo mpaka uyaone matokeo.

Jua, mafanikio yanatabilika, na wewe ndio  wa kuyatabili hayo mfanikio kwa tabia zako za kila siku, nini unafanya na nini hufanyi.

4. Siri ya mafanikio.

Lipa gharama, jifunze kwa waliyofanikiwa, anza kuwa yule unayemtaka, ishi tabia za kuwa bora kila siku

Acha maisha ya kawaida na historia, kila mtu anataka kufanikiwa ila siyo wengi wanajua tofauti ya waliyofanikiwa na waliyoshindwa, anza kujitofautisha leo.
Hutakufa kwa kuweka bidii ila utakufa kwa stress usipofikia malengo yako.

5.Jiulize maswali katika kila eneo la maisha yako, unayotaka mafanikio makubwa, *ni kipi ukikifanya kwa nidhamu maisha yako yataanza kubadilika mara moja?*

Ni mimi..
Moses zephania Mgema
0755632375
0678355394
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam,Tanzania

Sunday, November 4, 2018

MAMBO MUHIMU KUJIFUNZA

Key Skills To hold on
Kama mtu mwingine ambae ana kazi, vilevile mjasiriamali anahitaji ujuzi mkubwa ambao utamfanya aifanye kazi yake vema.
Unapozungumzia neno "UJUZI" ni kitu ambacho kimebeba vitu kama uwezo, utoshelevu,  na  uwezo wakufanya jambo fulani vizuri kabisa.
Ujuzi unafanya kazi na vitu kama, utalamu Fulani, maarifa, uwezo lakini lazima ujuzi usiutenganishe na kitu kinaitwa kipaji, kuna watu wanaujuzi wa jambo fulani kwa sababu ni kipaji chao
Kuna wakati lazima tukubali kwamba japo kwenye mafanikio ya ujasiriamali hakuna formula maalumu ya kutoboa kimaisha lakini kuna baadhi ya skills  (juzi) ambazo zina randana sana na mafanikio ya kijasiriamali na lazima mtu awe nazo au azijue.

Uwiano na mchanganyiko mzuri wa maarifa na juzi mbalimbali inamwezesha mjasiriamali kutegua au kupambanua mambo mbalimbali na kujenga lakini kuja na mawazo mapya ambayo yanamsaidia sana kuinua hali ya biashara na maisha kwa ujumla.

Tunapozungumzia ujuzi tofauti tofauti kwenye issue za ujasiriamali ni kwamba ujuzi una play role kubwa sana ya mjasiriamali kuwa mshindani wa kweli katika biashara, kuwa na akili wazi iliyofunguka na shapu ya kusoma hali ya soko kwa ujumla wake na kuweza kutembea kwenye hali yoyote ya soko
Tunapozungumzia suala la ujuzi maana yake tunazungumzia, ujuzi binafsi ambao ni kipaji, hard skills amabazo ndo ujuzi wa kibiashara. Ukiacha kipaji lakini ujuzi mwingine tunajifunza darasani na maeneo mengine, sasa Lazima Kama mjasiriamali ujue namna ya kutumia ujuzi wako to the maximum lengo ni wewe UNAFIKIA ndoto zako
Swali Je wewe unafikiri nini?

Ujuzi binafsi ni ule utaalamu tulionao ambao tunautumia kwa ajili kujiendesha kimaisha, ujuzi ni kile kitu kinakupa nguvu ya kufanya jambo fulanikwa sababu kiko ndani yako.
Ujuzi unapounganishwa na maarifa inatengeneza bond ambayo inapelekea kuboresha kabisa mfumo mzima wa ujasiriamali maana hapa itakupa nafasi yakuwa mbunifu, kuunda mbinu ndogo ndogo za kuwini washindani wako, kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinapokukabili, kukupa nguvu yakufanya maamzi mahali ambapo ni magumu na uthubutu wa kuanzisha mambo katikati ya woga wa wengine.
Ujuzi + maarifa inakupa nafasi ya kufanya kazi ya aina yoyote maana utakuwa na ujuzi wa kutengeneza mahusiano mazuri na aina za watu wote, hapa utakuwa na ujuzi wa kimawasiliano, nguvu yakufanya kazi kama team na kila mtu ambae analazimika kuwa mbia kwa namna yoyote ile.
Ujuzi unakupa nafasi ya kukufanya uyazoee maisha na hali yoyote kwenye maisha ya kibiashara ambayo unaweza kuyakabiri, uwezo wa mawasiliano mazuri na kila aina ya mteja au mbia.

Lakini pia ukiwa na ujuzi na maarifa itakupa nafasi kubwa mno pale kampuni au biashara yako inapokuwa kubwa namna ya kuunda uongozi na utawala wa usimamizi mzuri na biashara kusonga mbele zaidi kuliko ukiwa huna ujuzi ufahamu na maarifa juu ya ujasiriamali.

Vilevile ujuzi unakupa nafasi na uwezo mkubwa kutekeleza mipango na malengo amabayo ungependa kuyafikia ndani ya muda mfupi kati na mwisho ambao ni muda mrefu.

Ujasiriamali ni uwezo binafsi ambao unalifanya tatizo kuwa ni wazo linalotakiwa kutatuliwa kwa vitendo.

Kuwa mjasiriamali lazima uwe na uthubutu na uwezo  wa kuchukua na kutumia uwezo wa kufikiri, ubunifu na mtu mwenye kuchukua uamzi mgumu lengo kuu ni kutatua changamoto lakini pia kufikia lengo baada ya tatizo kuwa limepatiwa ufumbuzi.
Uwezo wa kujenga wazo, hoja uwezo wa kuwasiliana na namna ya kufanya kazi na watu sahihi ambao wanaweza kufanya nao kazi na kufikia malengo mfano unapokuwa na kampuni basi unapoajiri watu wawe na uwezo unaoutaka na wenye kuleta matokeo ya kile kilipelekea kuwaajiri.

Kumbuka ujasiriamali ni uchaguzi ambao mtu anafanya kwa manufaa yake na jamii, Kwa hiyo Lazima awe na mtazamo chanya endelevu, Thamani, uwezo binafsi, mwonekano na mapenzi binafsi na kazi husika.
Uchaguzi kwenye masuala ya ujasiriamali huzaliwa kwenye fursa amabazo unakuwa umeziona hapo ndipo unalazimika kufanya maamzi yanayowezekana katikati ya mambo ambayo yalionekana hayawezeakani kwa kutumia ujuzi sahihi.
Ujuzi pia unaotumika lazima uwe ujuzi sahihi ambao unaendana sana na hali ya utumiaji wa Teknolojia iliyopo ili kusapo ujuzi wako uwe sahihi zaidi hapa lazima pia utengeneza namnaya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kimasoko ili kuleta matokeo unayoyataka. Hapa pia inaendana sana na uwezo wa kugundua uwezo na udhaifu wa washindani wako hapo utaweza kuwa mjasiriamali bora.

Ni ujuzi upi ambao unakutofautisha na wengine?. Kuwa na uwezo ambao utakupeleka kwenye uzoefu ambayo lazima tabia yako kabisa ambayo imekufanya kuwa hapo ulipo.
Ujuzi unao na uzoefu unao sasa yakupasa kuanza kufanya mambo mbalimbali yaliyo ndani ya uwezo wako lakini kuwafanya watu wakuhitaji zaidi wewe kwa kile unafanya.

Prepared by
Moses zephania Mgema
0755632375

Saturday, November 3, 2018

JUA HAYA MAMBO MANNE ILI UFANYE BIASHARA YAKO KWA UFANISI.

kuna sababu nyingi sana zimekuwa zikichangia kuanguka kwa biashara na watu wengi bado hawajafahamu  sababu critical za wao kuanguka kibiashara hasa kwenye dunia ya tatu ambayo watu wengi ni kama tunaingia kwenye biashara kwa sababu hakuna namna nyingine ya kufanya ili kujiingizia kipato
Pamoja na sababu nyingine nyingi kama ukosefu wa elimu juu ya biashara, ujuzi, maarifa, ukosefu wa mitaji au kuanza na mitaji midogo, ukosefu wa uzoefu nk. Lakini kuna mambo haya muhimu sana kama unataka kufanikiwa kibiashara na ni vema ukazingatia sana.
Kuna kitu kinaitwa 4ps kwenye biashara yoyote ile.
Kwa Lugha ya kigeni zimebebwa kwenye kitu kinaitwa  (Marketing Mix )
Marketing Mix-Ni muunganiko wa sababu au mambo ambayo huwaratibiwa na kampuni au Taasisi ili kuhakikisha inatoa huduma kulingana na mahitaji ya wateja iliyowakusudia 

Tutaangalia mambo makuu manne 4ps ambazo mfanya biashara yoyote lazima uyazingatie ili kuifanya biashara yako idumu kwa kiwango kilekile au ikuwe zaidi.

1. Bidhaa  (products)- hiki ni kitu cha kuzingatia sana unapotaka kuanza kufanya biashara, sio kila bidhaa yafaa kuwa mahali fulani kwa sababu tu ulikuja au ulienda mahali ukakuta watu wanauza sana 

Jiulize je hii bidhaa pamoja nakuwa inauza sana hapa Dar je ni kweli singida kwetu inawatumiaji au inahitajika, Je katikati ya waislam kibanda cha kitimoto kitalipa, je baibui na kanzu katikati ya jamii ya kikiristo kitalipa, senene, michembe na bidhaa fulani inahitajika 

Kwa hiyo unapotaka kufanya biashara lazima uzingatie aina ya biashara unayotaka kuifanya kwenye eneo ambalo umeliona lina manufaa 

Kumbuka si kila fursa yafaa kutekelezeka kila mahali fursa zingine hazilipi kwenye eneo fulani hapa tuanachoangalia ni uhitaji wa kitu sio kila biashara ya dar ifanyike Arusha. Arusha tunaweza uza masweta, blanket lakini dar maji feni kwa sababu ya hali ya hewa.

2. Bei  (price) kitu kingine cha msingi sana kuzingatia unapotaka kufanya biashara. Hapa Lazima uangalie levels ya uchumi ya watu wa eneo husika je wanauwezo wa kumudu bei ya bidhaa yako, ukipeleka IPhone Singida, Manyara kigoma nk. Kwa asilimia ngapi wanamudu kununua IPhone yenye kuhitaji laki tano na kuendelea, ni kwel watu wanaipenda bidhaa lakini je wanaweza kumudu gharama za bidhaa hiyo

Lazima uzingatie kiwango cha uchumi cha eneo husika kabla hujapeleka bidhaa yako.usije anza kusema unalogwa kumbe ni wewe kushindwa kutambua level ya uchumi wa watu wa eneo la biashara yako

3. Eneo  (place)- Hii ni sababu ya msingi kuzingatia sana. mimi ntaanzia mbali kabisa kwamba Lazima eneo la biashara yako liwe karibu na wateja, Mazingira safi ambayo yatawavutia watu kuja, Mazingira Lazima yaweze kuwashawishi yaani eneo limtengenezee mtu sababu yakuja kununua kwako.kuna mambo sana ya kuzingatia kwenye uchaguzi wa eneo wataalamu wa masoko wametaja vitu vichache sana kwenye eneo hili ila Mimi naweza sema 

Eneo lako la biashara Lazima lijumuishe watu wa aina zote yaani wazima walemavu watoto eneo lako lazima liwazingatie sana maana wote ni wateja ukiacha mambo mengi ambayo yamezungumzwa na watu wa masoko 

Mazingira ya soko Lazima uyatengeze kwa namna yakumshawishi mtu kurudi tena na tena.

4. Promosheni (promotion) watu wengi huchanganya na wengi wanahisi ni gharama sana kufanya promotion hapana, promotion zipo za aina nyingi sana free promotion ambayo inaweza kuwa matumizi mazuri ya lugha kwa wateja kuwaja liwateja, kuchangamka kuwa na welcome face.

Kutumia zawadi ndogo ndogo kama pipi kwa watoto, kupitia mazingira safi yaweza kuwa means ya promotion. Achana na kutumia magari, media na vyombo vingine vya gharama ambavyo yawezekana huna mtaji wake.

Ivi sukari kwa sasa kilo unapata faida 1000 kwa mfano, na wengine wanauza bei hiyo hiyo kwa nini wewe usitoe hamsini au mia upate faida ya 900 shida iko wapi.

Lazima utumie akili na maarifa mengi ili kuifanya biashara yako kuwa stable na yenye kukuwa kila siku.

Kuna watu huona ugumu katika kila jambo ila mara nyingi sisi ndo tunatengeneza huo ugumu badilika nenda kisasa utafanikiwa 

Nimejaribu kutumia maelezo fulani ambayo sio kuntu sana ili uelewe vizuri 

MOSES MGEMA

0755632375