Sunday, October 6, 2019

KILE CHA ZIADA NDO DUNIA INAKIHITAJI KUTOKA KWAKO, SIO ELIMU , KIPAJI NK KATIKA KARNE HII.......BALI KILE KINACHOKUFANYA UWE TOFAUTI NA WENGINE.

-Kila kijana anatamani kuwa mtu fulani kwenye maisha yake, leo, kesho hata kesho kutwa
- Ni furaha ya kila mtu kutimiza mambo yafuatayo....
1. Ndoto na malengo.
2. Kuwa na fedha na kazi nzuri.
3. Kufanya kila kitu unachokitaka.
> Pamoja na kutamani yote hayo lazima kama vijana tujikumbushe haya yafuatayo....
1. Dunia ya leo haitafuti mtu wa kusaidia katika eneo lolote la maisha Bali mtu mwenye kuleta na kuongeza ufanisi.
2. Dunia ya leo inahitaji ulicho nacho cha pekee (Your uniqueness) mfano kwa nini tukuajili wewe kati ya maafsa masoko 200 ambao wanataaluma kama yako, nini cha ziada kwako ambacho wengine hawana.
3. Wewe mwimbaji kwa nini uje wewe wakati kuna waimbaji wengi wanaoimba aina ya mziki wako.......nk.

åDunia ya leo ina kila aina ya watu inaowahitaji, wamejaa hawana kazi, wanafanana kwa minajiri ya taaluma, wanavipaji, kila eneo wapo, kitu ambacho kimepelekea kwamba Watu ndo watafute kuliko wao kutafutwa.

å Miaka ya nyuma, mtu angeajiliwa ikiwa hajamaliza darasa la 7, mtu angeenda form one akiwa na kazi lakini leo kila mahali pamejaa na maofsi hayahitaji watu tena Bali watu wanazihitaji nafasi ambazo hazitoshi tena.
√•. Shahada na Masters  sio sababu tena ya mtu kukupa kazi kwa sababu watu wa aina yako ni wengi sana wamejaa kila kona.
å Kumbe nini sasa kinaweza kukupa thamani na kukufanya uhitajike zaidi na hii dunia ni (Utofauti juu ya ubora, maarifa ya ziada, ujuzi na ubunifu wa pekee ambao wengine hawana.
å Leo kuna watu hawana hata elimu ila wapo kwenye nafasi nzuri sana na wanakula maisha kwa sababu tu wameweza kujitofautisha na wengine, wamejiongeza na kujitengenezea thamani na mazingira ya kuhitajika zaidi kuliko watu wengine.
√•  Cha kwako cha ziada ni kipi....tunatafuta MC, msemaji wa makongamano, mwalimu, mwimbaji, Daktar, mshauri wa ndoa na mambo ya kijamii nk. Kipi kinatufanya tumwache wa karibu na mwenye bei ndogo na kukufuta wewe wa mbali.
å kwa nini tukuajili, kwa nini tukupe milioni kumi kwa mwezi, kwa nini uwe mtu Fulani.
å Ni kwa sababu ya kitu kidogo tu kinachokufanya uhitajike *-UWE WEWE-* kile kidogo kinachokutofautisha na wenzako wenye kipaji, elimu, sawa na wewe.
åkwa nini wanunuzi wa mahitaji waje kwako sio kwangu wakati wote tunauza madafutali na kalamu za aina moja, kwa nini nije kushona kwako sio kwa James, kwa nini nije kula kwako sio kwa mama John........?
> Kile kitu cha ziada ulichonacho chenye ubora ndo kinachonifanya nije kwako, Lugha nzuri ya biashara, huduma nzuri ya chakula, usafi na nadhifu, kujali na kuthamani wateja ndiyo sababu inayonifanya kuja kwako.....
Je kama wote tunawahudumia vizuri wateja zetu nifanyaje....
>Mfanye kuwa rafiki wa karibu
> Tumia mapungufu ya mwenzako kuwin.
å Dunia ya leo imejaa changamoto na ushindani wa hali ya juu katika kila jambo so ni vyema kujitofautisha kwa mtazamo chanya kwenye kila kazi unayofanya.......
Dhahabu ni Dhahamu hata kama inaonekana kufifia kwa sasa, ila huwezi kuilinganisha na kioo hata kama kiooo kinang'aaa kiasi gani..
BE YOU
BE UNIQUE
BE DIFFERENT
WALK ON WHAT OTHERS ARE SHOWING WEAKNESSES.
USE EVERY OPPORTUNITY WHICH COMES AHEAD OF YOU EFFECTIVELY.........
MAKE PEOPLE TO NEED YOU TO SATISFY THEIR NEED......

Prepared by
MO_MGEMA........INSTA
Moses Zephania....FB
0715366003.......WHATSUP
Dar ea salaam

1 comment:

  1. Barikiwa sana Mtumishi ni kweli kabisa maneno yaliopo hapa yatanitoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine bora zaidi Barikiwa sana.

    ReplyDelete