Usiruhusu mtu, au kitu chochote, mtu mwenye nguvu lakini hana hekima, busara na utu akuvunje moyo, au aiharibu njia yako kwa maneno ya dharau, kukatisha tamaa, kukwambia hujui wala huwezi.
åKama Mungu aliruhusu uzaliwe, maana yake Mungu alikuamini.
å Mungu amekupa talanta, uwezo wa pekee na sifa ya kwako tu.
åKuna jambo Mungu anatamani litimie kupitia wewe....
>Hivyo basi lazima ufahamu kwamba, njia ya mafanikio sio lelema, ina changamoto nyingi sana ambazo zinakuhitaji wewe kwanza ujijue kuwa wewe ni nani, kwa nini ulizaliwa, kwa nini upo hapo ulipo, unaenda wapi, na unaenda kufanya nini ? Hapo ndipo inaweza kukabiliana na changamoto yoyote njiani.
Kama hujijui basi ni rahisi kuyumbishwa, kukatishwa tamaa, kuhamishwa kwenye lengo na kusudi la kuzaliwa kwako..............
Tuna wazazi, viongozi, walezi, walimu, kaka & Dada, babu & Bibi, shangazi & mjomba hawa wanaweza kuwa wazuri kwako au wabaya kwako pia, hivyo tafuta kujijua kuwa wewe ni nani, hata wakija kwa lengo la kukuhamisha kwenye ndoto yako basi wakukute umekwisha jitambua.
Mafanikio ya mtu yako mikononi mwake yeye mwenyewe, wengine ni washauri wa pembeni lakini "constructor of your life is you".
Wapo watu duniani wanaamini kuwa wao ni sahihi daima, hawaruhusu wengine kuchipua mbele yao, any potential wakiona kwa kijana wanatumia nguvu kubwa kuizima, wanadharau, wajuzi wa kila kitu, wabinafsi, wakosoaji sio wajenzi, maboss sio viongozi, wamelewa madaraka na sifa, kwao miili yao sio chakula cha udogo, wanaishi milele.......hao ni hatari sana watambue na kuwaepuka.
Pamoja na kwamba dhahabu ili ing'ae inahitaji moto, vilevile mmea ukisongwa sana na miba pamoja na magugu hutoa matunda dhaifu na wakati mwingine kutokutoa kabisa jihadhari.
Sio kila jambo gumu ni changamoto bali ni vitu vya kuepuka, daima ukiona mto unaspeed ya maji kubali kusubili upungue au utafute namna nyingine ya kuvuka mto huo.
Njia nzuri ya kufanikiwa ni
1. Kumshukuru Mungu kwa kuwa ulivyo
2. Kujitambua, kujikubali na kujiamini
3. Kuwa na maarifa sahihi na ya wakati.
4. Kuwa wewe kwanza kabla ya kupokea ushauri
5. Epuka majungu,fitina na unafiki
6. Mwombe Mungu akujalie hekima, busara, na namna njema ya kuishi na watu.
> Wewe ni Wewe, Mimi ni Mimi, yule ni yule, pamoja na kwamba tunahitajiana lakini wewe ndiye C.E.O wa maisha yako.
Mfanye Mungu namba moja kwa kila kitu, atakubariki, atakupa maarifa, utulivu ambao utakufanya uamue vyema kwa kila jambo.
I love you brother & sister.
MO_Mgema
mgemamoses@gmail.com
0715366003/0755632375
Dar es salaam, Tanzania.
Facebook Moses Zephania
Twitter Mo Mgema
In stag Mo_Mgema
YouTube; Mo Mgema
No comments:
Post a Comment