*-MFUMO WA MAISHA-*
•Dunia imeubwa kwa mgawanyo sawa wa muda, majira na nyakati, mpangilio wa kizazi kimoja kwenda kizazi kingine.
•Mzazi mmoja kwenda kwa mtoto na mtoto akileta mjukuu, vitukuu mpaka vilembwe, dizaina na mratibu wa mambo yote haya ni Mungu.
•Uwepo wa mtu kwenye kizazi Fulani, kwenye miaka Fulani lilikuwa kusudi, majira na wakati sahihi wa kila mtu kuwa tumboni mwa mama hatimae duniani kwa mwaka, sikunde, dakika saa, Siku, wiki mwezi,mwaka kwa muongo, karne na millennium pia.
• Waliozaliwa miaka ya mwanzoni mwa 1900, hao ndiyo Mungu aliwaamini kuwa hadi kufikia wakati wa Tanzania inataka kuwa nchi huru wataweza kupambana kwa hoja na watu kutoka bara Ulaya na nchi itakuwa huru.
• J.k. Nyerere na wenzake wakazaliwa na hatimae kukuwa, kwa ushirika wao walipambana na watu toka Ulaya, walionekana sokwe, wajinga, wapuuzi, waliumia, walibaguliwa na kuteseka lengo ikiwa ni kuhakikisha nchi yetu inapata uhuru na hatimae baada ya miinuko, miiba, jua, makorongo, milima na changamoto zote toka enzi za kina kinjikitile Ngwale, Mangi sina, na watawala wa kichifu ambao walikutana na ukatili wa kijerumani Leo Tanzania imekuwa nchi ya watu weusi na hata tunaona fursa za kusema na kufurahia kwa sababu ni wakati wetu na sisi.
• Tukiwa na matajiri na watu wa aina mbalimbali hapa nchini Leo kina Nyerere, chief mkwawa, Kijikitile Ngwale na wengine hawapo tena duniani na wakati mwingine uzuri wa Tanzania hawaujui kabisa wamelala na zama zao zimepita.
•√MFUMO WA MAISHA.......
•Mfumo wamaisha umegawanyika katika makundi tofauti tofauti, na mgawanyo huu umekuja ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pakuishi na kufurahia zawadi ya Mungu ambayo ni pumzi ndani yetu.
• Kuna watu wamekuja kama waandaji wa mazingira ili wengine wafurahie ndiyo maana walizaliwa katika kipindi ambacho kila mtu WA kizazi hiki anajiuliza ni kwa namna gani watu waliweza kuishi enzi hizo ?....Je maisha bila simu, internet, lami, ndege nk yaliwezekanaje ?.
• Yaliwezekana kwa sababu kwa majira na nyakati Mungu aligawanya na kila mtu kwa kizazi chake aliaminiwa kuishi kwa miaka na karne yake na waliweza kwa sababu waliumbwa kwa muundo wa kuyaweza na kuyakabili maisha na mazingira ya kizazi chao.
• Wengine wameumbwa kama makatapilla na walishushwa duniani kwenye Yale mazingira magumu ampapo Hummer, Range, Harrier, Scuba, Subaru, Prado, Rav4, nk visingeweza kumudu mazingira hayo...
• katapillar likaja kuyakabili mazingira hayo na kusafisha, kushusha milima, mabonde, kung'oa visiki, kufukia mashimo, makorongo, kupasua miamba, na kuhakikisha kwa kiasi Fulani levo inakuwa sawa kwa ajili ya magari mengine.
• Baadhi ya watu ni makatapilla kwenye maisha, wapo kwa ajili ya kuwatengenezea wengine mazingira na barabara nzuri.
• Katapilla hukutana na visiki, miamba, makorongo, milima na miinuko mingi na kwa sababu hiyo hulazimika kung'oa, kupasua miamba, kukata miti, kufukia mashimo, makorongo na kusawazisha vyema na kisha kuweka jamvi zuri lami nk.
• Hivyo basi kama wewe uliishi maisha ya katapilla au unapitia maisha hayo kwa sasa usipende sana au kulazimisha na wengine kuishi maisha hayo wakati unyoofu na usawa wa barabara upo levo tayari.
• Acha wengine wafurahie ubora na uzuri wa barabara hiyo, wasimulie na kuwambia changamoto ulizopitia ili kuwapa changamoto ya kuilinda na kuitunza barabara hiyo vizuri, usilazimishe na wengine wapitie mapito uliyopitia wewe kwa kuwanyanyasa, kuwa mbabe, na kutumia nafasi ukiyonayo kuwaumiza wengine bila sababu za msingi.
• Kumuumiza, kumnyanyasa, na kutaka afanye matakwa yako hata kama anaona hatari mbele sio sahihi, wala humjengi Bali unajiumiza mwenyewe ukizani unamkoa kumbe unajiumiza wewe mwenyewe.
• Mtu hafundishwi kwa manyanyaso, masimango Bali hufundishwa kwa utaratibu mzuri na kupewa nafasi yakuonyesha ubora wake.......Ubabe, kutumia nafasi za utajiri, uongozi kuwanyanyasa na kuwadidimiza wengineo sio sawa na lazima ukumbuke kuwa maisha ni kama jua tu huanza kwa upole na kufurahiwa na watu lakini saa nane hakuna awezaye kukaa juani, na jioni jua huwa tamu na kila mtu aweza kulifurahia tena.
• Ndiyo maana Yesu alifanyika katapilla kwa niaba yetu, kilichobaki kwetu nikufuata misingi bora ya Imani ambayo aliyeileta aliumizwa nayo na leo tunafurahia.
• Katapilla Yesu alichonga barabara, alichomwa na miiba, walimpiga mijeredi, wakamtemea mate yetu, lakini kumvisha taji ya miiba kichwani ili Mimi na wewe tuwe tulivyo leo.
• Fikiria kama huyu Mungu angetaka kila mtu alipie pumzi yake ingekuwaje nafikiri hakuna angeweza kuishi.
• Kama wewe ni tajiri, kiongozi au mzazi usipende waliokuja na kukuta Mungu ameshakuinua kuwanyanyasa, kuwakandia na wakati kuumiza nafsi zao bila sababu ya msingi.
• Wambie kwamba haikuwa rahisi kuwa hapo ulipo, ulipitia changamoto nyingi, ambazo leo ndiyo zimekufanya ukawa hapo, hivyo kila mtu afanye kazi, asome kwa bidii na kutimiza jukumu lake sawasawa ili kulinda hatua ambayo mmenikuta nayo na ikiwezekana kwa sababu sasa haupo pekee yako, uunganishe nguvu na team yako kufikia malengo makubwa zaidi.
Note.....
Kama wewe ni boss, mzazi, kiongozi tumia changamoto ulizokutana nazo kuwakumbusha tu kwamba kuna milima mirefu, miamba, miiba nk. Mpaka kufikia hapo ulipo.
•Changamoto ni maisha ya mwanadamu ila kwa majira na nyakati zina changamoto zake.
• Kama ulikuja mjini na madaso, usilazimishe na wengine wavae madaso wakati mitumba ya wachina imejaa k/koo.
Katika yote Mungu ndiyo msingi wa yote.
Kama umebarikiwa wewe basi wabariki na wenzako kwa wema na Mungu atakujazia
Prepared by
Moses Zephania Mgema
0755632375/0715366003
mgemamoses@gmail.com
mosesmgema.blogspot.com
No comments:
Post a Comment