Sunday, September 24, 2023
IFANYE NDOTO HALISI YA MTOTO UNAEMLEA IWE KWELI L
Monday, September 4, 2023
Thursday, August 31, 2023
incentives.
• Sixth, all employees must have a path to give feedback on the success of the process.
• Seventh, all employees must actively participate in the procedure.
• Eighth, the change may involve strategically-planned corporate “interventions” such as mergers.
Organizational Leaders
Many business experts believe that this type of leadership should come from the human resources department. An article in Forbes Magazine says the most important factor in organizational change is managing human capital. The article author says that human resource departments should focus more on being “strategic business partners” and less on implementing HR policies. The article goes on to say that the most important components of the development are identifying options for change that are available to the corporation and then to look at employees in terms of management talent and how to recruit, train and keep that talent.
HR also should be responsible for creating a motivational program that would permeate the entire organization. Obviously, the kind of assessment and change discussed here necessitates the leadership of people who understand human and organizational behavior and other components of the challenge of organizational change. Universities offer degree programs for professionals that include undergraduate and graduate degrees as well as doctoral degrees and certifications. Certificates can generally be earned in less than a year and can supplement other business degrees. Students take courses in areas like communications, conflict resolution, staff development, and human resource management.
Sunday, August 20, 2023
Wednesday, August 16, 2023
Monday, August 14, 2023
Mahusiano mazuri ya wazazi ni muhimu katika malezi ya watoto
Watoto hujifunza kutokana na matendo ya wazazi wao, kama watoto wakilelewa kwenye familia yenye mifarakano na kutokuelewana baina ya wazazi wao mara nyingi watarithi tabia hizo. Wakilelewa kwenye familia zenye mahusiano mazuri, majibizano yenye kuheshimiana nao watathamini umuhimu wa mahusiano. Tatizo kubwa linalopelekea mahusiano kuzorota ni mawasiliano dhaifu. Udhaifu wa mawasiliano tunaozungumzia ni pamoja na kukaripiana, kutukanana, kununiana na hata kusonyana mbele za watoto wenu.
Hili laweza kuwa tatizo la mahusiano yenu, lakini kwa nini muwahusishe watoto? Kwani ugomvi lazima ufanyike sebuleni? Hakuna faragha kama chumbani mkakaa na kuzozana?
Kupaziana sauti mbele ya watoto wako inawaletea watoto madhara mbalimbali ikiwemo nidhamu ya uoga na kutojiamini na hivyo kumyima fursa ya kuwa mdadisi na kudhoofisha uwezo wa akili yake kukua kadiri ya umri wake. Kwa maneno mengine, unamdumaza mwanao kwa wewe kutohsiana vyema na mzazi mwenzio. Wewe ni mama au baba kwa mtu na si vinginevyo. Hivyo majina mnayoitana mkiwa na mihasira yenu yanawaondolea uhalisia na heshima mbele za watoto wenu.
Inawezekana kabisa mzazi mwenzako ni mkorofi na hajali kama kuna mahitaji ya watoto na familia kwa ujumla. Ingawa tunatambua umuhimu wa kushirikiana katika kulea watoto, busara inahitajika katika kuhusiana na mwenza mkorofi wa namna hii katika ndoa. Haingii akilini kwa baba au mama kumcharaza mboko mwenza wake wa ndoa/mzazi mwenza kisa kakosea. Sasa unamcharaza viboko ili ajifunze ama unabomoa mahusiano yenu na maisha ya watoto wenu bila ya wewe kujua?
Suala lingine linaloathiri maadili ya watoto amabalo ni la kimahusiano katika familia ni ubinafsi uliokithiri kwa baadhi ya wazazi. Kuna wazazi ambao wanaishi kwa sheria ndani ya nyumba kwa kuwazuia wenzi wao ikiwemo watoto kutotumia baadhi ya miliki zilizomo ndani ya nyumba zao. Kwa mfano, kama baba hayupo TV, Radio, nk. haviwashwi ama akiwepo basi woote mnaangalia anachotaka yeye na hakuna mjadala juu ya hili. Bado yote haya ni kutowaheshimu wezi wao wa maisha. Dharau unazomfanyia mwenzio mbele ya watoto wenu unajenga maisha ya watovu wa nidhamu. Watoto namna hii hawatoweza kuwaheshimu watoto wenzao na hata watu wazima ikiwemo waalimu. Matokeo yake watoto hawa itawawia vigumu kusoma darasani na mara nyingi wataishia mitaani kuhangaikia matumbo kwa kugaagaa kuganga njaa ukubwani.
Ikiwa huna mahusiano mema na mkubwa mwenzio vipi utakuwa na mahusiano wa watoto wenu? Watoto pia wanakumbana na changamoto kama ilivyo kwa watu wazima na wanahitaji mtu wa kuwasikiliza na kuwapa ushauri wa namna ya kuzitatua changamoto hizo. Kutokana na kukosekana kwa mahusiano na mawasilianao mazuri baina ya wazazi na watoto wao, watoto wanapata wakati mgumu kujenga ukaribu na wazazi. Pindi wanapopata changamoto, hasa katika kipindi cha balehe kwa kuogopa kuwahusisha wengi wao hutumbukia katika matatizo makubwa kama kutumia madawa ya kulevya na mimba za utotoni. Kuna wazazi ambao kwao ni mwiko kuongea na watoto wao ana kwa ana na badala yake husikiliza mahitaji ya watoto kupitia mzazi mwenza! Matokeo yake mtoto akipatwa na matatizo wazazi hawa mara nyingi huishia kuwalaumu wenza wao ambao eti wameshindwa kulea. Mmeshirikiana kuzaa. Shirikianeni kulea.
Familia nzuri na yenye amani hujengwa kutokana na uhusiano thabiti wa wanafamilia hasa baba na mama. Familia namna hii inayo mazingira muafaka kwa makuzi ya watoto. Ubora wa mawasiliano, uchaguzi wa maneno ya kusema hasa uwapo na hasira mbele za watoto ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya watoto. Kutofautiana katika mahusiano kupo. Lakini ugomnvi wa maneno kati yenu ufanyeni faraghani, chumbani, n.k. Inawezekana
Prepared by Moses Z. Mgema