Monday, February 26, 2024

PASTOR ELIYA TIMOTHY TOKA DODOMA

1.Mpe Bwana Utukufu
2.Nyenyekea
3.Sikia na kutii maelekezo ya Mungu
4.Tafuta maelekezo ya Mungu na uyafuate
5.Kaa kwenye nafasi yako

Sunday, February 25, 2024

Imenichukua miaka 3 nikiwa nasoma vitabu mbalimbali vya historia za watu ambao wamekuwa ni History makers and History breakers, watu ambao dunia imekuwa ikiwazungumzia kuwa ni ICON people kwa mambo makubwa ambayo wameyafanya na kuacha alama za kukumbukwa hapa Duniani.
■ Asilimia kubwa za hawa watu wanatokea familia duni sana, familia ambazo kuishi kwake ni pale tu unapoamka hai ndo usalama na mtaji wako wa siku.
■Ni watu ambao wamelala njaa, wanajua nini maana ya dhiki, nini maana ya ugumu wa maisha nk.

Katika nyakati ngumu na nyakati zenye giza nene na lisilo na matumaini bado waliamini kuwa hakuna hata mmoja anaweza kubadili historia ya maisha ya mtu isipokuwa mtu mwenyewe.

Katika ulimwengu tulio nao leo, nguvu binafsi, juhudi, kutamani kuwa uliyekusudiwa na Mungu basi jua inakuhitaji wewe uvuje jasho jingi sana ambalo litakutambulisha ulimwenguni.

Hakuna namna rahisi inaweza kukupa nafasi ya kufurahia 

Friday, February 23, 2024

The world  needs very focused, determined and energetic people, watu wasio jenga hoja ya kushindwa kwao kwa sababu ya watu wengine, wanatambua kuwa mwenye wajibu wa maisha yake ni yeye mwenyewe

Thursday, February 22, 2024

Maisha ni safari ambayo mwanadamu huianza pale ambapo mchakato wa kuumbwa kwake unapofanyika na hatimae kuwa mtoto na kuzaliwa.
■Katika safari kuna nyakati zenye kubeba kumbukumbu zenye hisia mchanganyiko kutokana na mapito ya Duniani, zipo nyakati za furaha ambazo hutufanya kufurahia na kuiona dunia ni sehemu yenye utulivu ambapo tunapaswa kuishi na kuzifanya ndoto zetu kuwa kweli ambapo ni kutimiza kusudi la Mungu la uwepo wetu hapa duniani.

■ Pamoja na nyakati njema zenye kutufaraji na kutupa utulivu katika safari ya maisha, hatuwezi kukataa kuwa pia kuna nyakati ngumu zilizobeba hisia zenye machungu na machozi ambazo mara zote huwa hatutamani nyakati hizo zijirudie kwenye maisha yetu.

■ Tumepoteza vingi mno vyenye Thamani, tumepoteza wazazi, ndugu na jamaa zetu wakaribu, tumepoteza marafiki na vito vya Thamani ambavyo pengene tusingetamani viondoke mikononi mwetu lakini bado Mungu aliamini kwa wakati tulio kuwa navyo ndiyo ulikuwa wakati sahihi na muda wakuwa mbali na mikono yetu ulipofika Mungu aliona vyema viwe mbali yetu kwa maslahi yetu binafsi na Mungu pia kwa sababu Yeye Mungu hujua kila jambo huja na kupita kwa utukufu wake.

■Katika ya nyakati hizo zote kuna moja huja kwa sura mbaya lakini ndani yake ndiyo ina heri na nyingine huja kwa sura nzuri mfano wa malaika lakini ndani yake huwa imebeba maumivu na matokeo yenye majuto ndani yake. Nyakati hizi tunamhitaji sana Mungu ili tuamue sahihi kwa manufaa ya kwetu, familia, makusudi yetu Duniani na kwa Mungu pia.

■ Pamoja na nyakati nyingi mchanganyiko ambazo binafsi nimezipitia kwenye maisha yangu kwangu nimekuwa na imani na mtazamo chanya kwa sababu zote zimenifanya kuwa mtu bora kwa kiwango ambacho nipo na zimeendelea kunipa courage na nguvu yakujiboresha na kuwa mtu mwenye tija zaidi duniani.

■Maeneo mengi nimepita na kwa kadri ya nguvu za Mungu imenisaidia sana kuwa a very positive man although si kila kitu napatia kwenye maisha ila i always stand to be corrected ninaposhindwa kufanya vitu vyangu kwa kiwango na ubora unaotarajiwa na mahali nakosea i always admit and  be ready to be helped for the seek of being a person the world need and a man was intended by God from the Begning.

■ Ndoa ni eneo Nyeti sana, ndoa ni taasisi ambayo inatumika kujenga uzao bora, familia bora, ukoo bora, kanisa bora, jamii bora na hata dunia yenye tija na amani. Kila mtu ni matokeo ya familia na malezi ya wazazi, jamii na hata watu wanaomzunguka by the time.

■Wakati mwingine ndoa ni sehemu ambayo inazalisha jamii mbovu kutokana malezi, mazingira, tabia za wazazi na watoto wamekuwa wakijifunza nini kutoka kwa wazazi wao. Ubaya wa mtu na uzuri wa mtu ni matokeo ya wapi ametokeo......Lakini.......

■ Pamoja na wakati mwingine baadhi ya watu kutokea kwenye background ngumu, lakini juhudi za kujitambua kwa mtu binafsi huwa ni njia nyingine bora ambayo inamsaidia mtu kubadili mwelekeo wa maisha yake bila kujali ametokea familia ya aina gani, walevu, wachawi, familia duni na yenye maadili hafifu, lakini anaweza kuwa Baba bora, mama bora pale tu atakapoukubali ukweli wa kwamba familia niliyotoka si familia iliyonijenga vyema, hivyo huyo mtu hubadilika na kutumia mapungufu ya historia yake kama changamoto yakuchukua initiatives za kubadili mwelekeo wa maisha yake.

■Na hivyo mtu huyu huanza kupita njia mpya na bora yenye manufaa kwake na jamii yake. Ndiyo ule msemo unakuja "To be born in a poor family is not a problem but if you die poor their must be a problem somewhere. Hata kuzaliwa na familia ya watu walevi, familia isiyo na maadili sio tatizo bali kuendekeza na kuishi mfumo huo huo wa maisha ndiyo tatizo.

■ Nilipojitambua kuwa mimi ni mwanaume na nilijua kuwa kuwa mwanaume basi kuna wakati utakuwa mume wa mtu na taswira ya familia yangu inabebwa na kila maamzi ambayo ntakuwwa nayafanya kama Baba na kiongozi wa boma langu. Hivyo basi nimetumia muda mwingi mno  kujifunza, is where i came to realize that a man should be a responsible for himself, his wife and community in General.

■ Wengine tunatokea kwenye makabila ambayo they believe a woman is weak and she supposed to down/undermined kwa sababu hawapaswi kuwa na sauti, huo ni urithi usio na tija wala ustawi wa familia nyingi hasa kipindi kile cha nyuma.

■ Mbali ya kujifunza kwa Baba ambavyo amekuwa baba bora kwetu katika malezi, familia na hata kwa mama, lakini alikuwa na matamanio yakuniona kuwa natumia neema ya kumjua Mungu, kuishi chini ya malezi bora na kufundishwa njia bora za kuwa mume, lakini pia binafsi nimekuwa na juhudi kubwa za kuendelea kujijua na kujua ni nani anapaswa kuwa sehemu ya maisha yangu yaliyobaki.

■ Nimejifunza kanuni za kuwa na ndoa bora, familia bora na kuwa Baba na mume bora kwa mke wangu, lakini pia imenipa utulivu, akili ya ndani yakutambua whom i should marry. Ok nimewaona wengi lakini kwa kweli Agatha ni mmoja tu nae ndiye wewe na who derseves to be my wife ni wewe kipenzi and my promise always as long as nimepata mke wa ndoto zangu basi you will never regret having me the rest of your life

■A man is a head of family, kichwa kiko juu ndani ya kichwa kuna uso, macho, masikio, mwonekano, pua, mdomo na akili ziko kichwani, what does it mean, ia maanisha kuwa a man should be smart, visionary, Humble and the level of wisdom must be in a high level so that he can make right and correct decision ambayo yatakuwa na tija kwake na kwa wengine.

■A man is a leader ambae kikawaida kabisa anapaswa kujua whom can be a right choice for him. Napaswa kujua aina ya mke wa kuoa kwa kutambua potential yake, uwezo wa kiakili, hekima, level of humbleness na how she can be supportive and if she can be supported anaweza kufanya jambo likatokea, hilo linategemeana na mwanaume mwenyewe ana jicho lipi la tatu la kutambua mwanamke sahihi wakuambatana nae katika kujenga taasisi bora ya ndoa.

■ Nimekuwa nikijifunza sana hasa kwa ndoa zilizofanikiwa katika malezi, uchumi, mwanamke kuwa jasiri, ndoa zenye furaha nk, msingi wa kwanza ni uchaguzi sahihi wa mkena kutambua potential yake, ndoa is not just love, sex, but kuna more and more factors ambazo must be considered ili kujenga ndoa bora na yenye matokeo bora. I can mention more than 20 marriage both waliookoka na watu wengine tu wenye imani zingine how much succesful and what are the reason of their achievement.

■ Mwanaume akitambua nguvu ya mwanamke, akili na utulivu wa akili + awe mcha Mungu sio mhudhuria ibada za kanisa basi just know ndoa hiyo itakuwa imara na yenye matokeo bora kwenye aspects zote za maisha, Elimu, afya, malezi, uchumi na kila mmoja anaweza kuishi kwenye kusudi ambalo ameumbiwa na Mungu hapa Duniani.

■ Agatha, wewe ni mwanamke bora na sahihi sana kwangu kwa kuzingatia mambo mengi ambayo nimeyabaini kwako and i am so confidently to have you as my wife. Ipo nguvu na imani kubwa mno juu yako si tu kwa sababu wewe ni mrembo, mzuri na mwenye akili tulivu lakini una extra character ambayo it needs a man serious who can see that character bila kupepesa macho.

■Moja kati ya ndoto yangu ni kuwa na wewe na ahadi yangu kwako basi wewe utakuwa miongoni mwa wanawake wenye furaha na ndoa zao kwa sababu tu mimi najitambua na kutambua majukumu yangu kama mwaume bora wa kizazi hiki, i always speak this kwa ujasiri kwa sababu najua moja kati ya changamoto zinazoumiza ndoa nyingi ni ubabe wa wanaume, kuwafanya wake zao kuwa watumwa na wengi kujisahau kusimama kwenye nafasi zao kama leaders.

■ Najua zipo changamoto zinaweza kutokea kwa sababu tupo duniani lakini je how as a man, a leader should stand and deal with the situation ndiyo hapo mambo huanza kutofautiana.

■ Wewe ni mwanamke bora sana kwangu, na juzi nilimwambia mama yangu kuwa nimepata mwanamke bora kwenye maisha yangu, mwanamke ambae nilikuwa namuwaza na kumwota kwa miaka mingi naiona familia yangu ikiwa bora sana. Akasema bila shaka atakuelewa na mtafunga ndoa yenye baraka nyingi, Moyo wangu una amani na binti huyo na ni chaguo sahihi kwako ingawa sijamwona kwa sura.

■ Ninayo mengi yakuandika hapa ila niseme tu, Mungu atatupa muda mzuri sana wa kufurahia matunda ya ndoa yetu na tutapata watoto wazuri wenye tabia njema kama tulivyo wazazi wao.

■ Natamani tufanye joint bora sana ambayo itatupa utajiri na uimara wa kipato kabla ya kuturn 40 years ya kuzaliwa kwangu ambapo ni almost 10 yrs from now. 

■ Una kipaji kikubwa sana cha kiongozi, uwasilishaji wa mada na ukaeleweka na ninaona hapo kuna namna tunaweza kufanya kwa pamoja na kutengeneza fedha nyingi amabazo zitatupa utajiri mwingi sana.

Natamani NDIYO yako leo ili tuanze mchakato wa kufunga ndoa yetu na ukieleweka mapema tutafunga ndoa before September.

Wewe your matured, ndoa ni msingi mwingine bora wakufanya maisha kuwa halisi, being alone utulivu pia wakufocus kwenye mambo huwa upo chini ukilinganisha na watu walio ndani ya ndoa na Kibiblia ni kuwa mwanaume akipata mke anakuwa amepata kitu chema na amepata kibali kwa Bwana, hivyo kuna some blessings mtu akiwa single anaweza asielewe sana but it works and I know.

Ndoa ni familia tatu, moja wana ndoa wenyewe ( mimi & you) halafu kuna your family side and my family side. I have tried to understand where your coming from na kujua walau background yako, hivyo najua mke napata kutoka kwenye familia gani and how your family depends on you. Shortly as long as nimekupenda wewe basi mimi nimependa na boga lake. 

Tuna uchumi mdogo kwa sasa ila i am sure within five yrs of our marriage sisi tutakuwa watu wengine kabisa financially na i blv having you is total combination of achieving our goals. Wazazi wetu wataenjoy maisha before the end of their life hapa duniani. 

Lakini i have so many project ambazo natamani kuzifanya na mke wangu as my real partnership, marafiki wengi wameingia kwenye migogoro pale faida inapoanza kutokea so i dont need that is better i do it with my wife for the seek of our beloved children.

Jumapili nitapata muda mzuri sana wa kuketi na wewe kuzungumza and the only topic itakuwa ni hii.

Nakupenda Agatha, mke mtarajiwa 
One of the most beautiful wife.


Friday, February 2, 2024

"Sura ya Mungu" (Kiebrania: Kigiriki: Kilatini: imago Dei) ni dhana na fundisho la kitheolojia katika Uyahudi na Ukristo.[1] Ni kipengele cha msingi cha imani ya Uyahudi-Kikristo kuhusiana na ufahamu wa kimsingi wa asili ya mwanadamu. Inatokana na maandishi ya msingi katika Mwanzo 1:27, yanayosomeka hivi: "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba." Maana kamili ya kifungu hiki imejadiliwa kwa milenia.

Kufuatia mapokeo, idadi fulani ya wasomi wa Kiyahudi, kama vile Saadia Gaon na  Philo, walisema kwamba kufanywa kwa mfano wa Mungu hakumaanishi kwamba Mungu ana sifa zinazofanana na za binadamu, bali ni kinyume chake: kwamba kauli hiyo ni lugha ya kitamathali inayotolewa na Mungu. heshima maalum kwa wanadamu, ambayo hakutoa kwa uumbaji wengine
Kufuatia mapokeo, idadi fulani ya wasomi wa Kiyahudi, kama vile Saadia Gaon na  Philo, walisema kwamba kufanywa kwa mfano wa Mungu hakumaanishi kwamba Mungu ana sifa zinazofanana na za binadamu, bali ni kinyume chake: kwamba kauli hiyo ni lugha ya kitamathali inayotolewa na Mungu. heshima maalum kwa wanadamu, ambayo hakuwapa viumbe wengine.

Historia ya tafsiri ya Kikristo ya sura ya Mungu imejumuisha mistari mitatu ya kawaida ya uelewaji: mtazamo wa kimsingi unaweka sura ya Mungu katika sifa za pamoja kati ya Mungu na ubinadamu kama vile busara au maadili; ufahamu wa kimahusiano unabishana kwamba taswira hiyo inapatikana katika mahusiano ya kibinadamu na Mungu na kila mmoja; na mtazamo wa utendaji hufasiri taswira ya Mungu kuwa jukumu au kazi ambayo kwayo wanadamu hutenda kwa niaba ya Mungu na kumwakilisha Mungu katika mpangilio ulioumbwa. Maoni haya matatu hayashindani kabisa na kila moja inaweza kutoa ufahamu wa jinsi wanadamu wanavyofanana na Mungu. Zaidi ya hayo, maoni ya nne na ya awali yalihusisha umbo la Mungu la kimwili, la kimwili, linaloshikiliwa na Wakristo na Wayahudi pia.
Mafundisho yanayohusiana na sanamu ya Mungu hutoa msingi muhimu kwa maendeleo ya haki za binadamu na hadhi ya kila maisha ya binadamu bila kujali tabaka, rangi, jinsia au ulemavu, na pia yanahusiana na mazungumzo kuhusu mwili wa binadamu.

Vyanzo vya Biblia

MBEGU HUOZA NA KUOTA.

Unapanda nini kwa watu na unategemea kuvuna nini baada ya kupanda mbegu ambayo leo hii umekazana sana kuipanda. 
Katika safari ya maisha kuna namna mtu huchagua kuishi hasa kwenye eneo la tabia na kiukweli kabisa tabia ya mtu ndiyo picha ambayo watu wanaweza kuitumia kwa ajili ya kumwelezea huyo mtu na watu hawawezi kusema tofauti na mtu ambavyo anaishi na kubahave.

Na katika mfumo wa maisha yetu kuna aina mbili tu za tabia ambazo zinatumika kumtambulisha mtu kwa watu au ndiyo alama ya utambulisho wake kwa watu wanaomfahamu.

1. Tabia njema
2. Tabia mbaya

1. Kwenye Tabia njema : Ni mkusanyiko wa mambo yote chanya ambayo mtu anayafanya kwa ajili yake na kwa ajili ya wengine mfano mtu akiwa ni mtu wa ibada, anafanya kazi kwa bidii, mwaminifu, mwenye huruma, kusaidia wengine, kuchukulia mambo katika mtazamo chanya hata kama kuna namna ameumizwa lakini anafikiri lengo la kwanza kabla ya mtokeo haya ilikuwa ni nini, mkweli mwenye upendo, mwenye nia ya kujenga na kuboresha zaidi kuliko kuharibu na kuumiza nk. Hiyo inaweza kuwa ni tabia njema sana.

2.Tabia mbaya: Ni tabia ambayo ndani yake huwa na malengo maovu tu hata kama kwenye sura ya nje inaonekana ni mambo mazuri mfano kutumia nafasi tulizonazo vibaya, kubana haki za wengine kwa manufaa binafsi, kuumiza wengine kwa sababu ya nafasi uliyo nayo, chuki bila sababu ya msingi, kuwa na wajibu wa jambo fulani lakini hufanyi na unajua ukifanya wengine pia watanufaika, uchoyo,  kukosa utu, rushwa, fitina na mambo mengine yafananayo na hayo. Hayo yote yanaingia kwenye kundi la tabia mbaya.

Rafiki yangu yote ambayo nayafanya mimi leo au unayafanya wewe leo fahamu tu kuwa hiyo ni mbegu na ipo siku mbegu hiyo itaota na kustawi vyema kabisa whether ni mbegu ya magugu au mbegu ya ngano bora.

Baada ya Baba yangu mzazi kuondoka duniani baadhi ya marafiki zake wengine ambao hata tulikuwa hatuwajui walikuja nyumbani, wengine tulikuwa tunakutana nao njiani wanasema hivi kwa maisha ya Baba yenu na namna ambavyo aliwekeza mambo mema kwa watu basi hamwezi kuishi kama yatima hata siku moja.

Kijana mmoja ambae kiumri yeye kwangu ni mkubwa tu tukakutana nae akaulizia habari za mzee wangu nikamwambia mzee amesharudi mbinguni kwa Baba alissikitika sana lakini akasema Baba yako alinitendea jambo hili na hili wakati maisha yangu bado yako gizani siwezi kumsahau kabisa na mimi ndiyo kaka yako wa hiari tangu kipindi hicho hadi leo amekuwa kaka kweli kweli ila ni kwa sababu ya Baba yangu.

Wapo wengi sana ambao kwa wema na uzuri wa mzee wangu leo hii singida imekuwa zaidi ya nyumbani kwetu Kahama, tulijua pengine baada ya mzee kufariki tungerudi nyumbani kwa sababu tu tuko pekee yetu singida na tulikuja singida kwa sababu ya kazi ya Baba pia lakini kitu kilichotubakisha Singida ni wema wa mzee wangu kwa watu.

Nakumbuka siku moja Baba aliwahi kuniambia hivi, watendee watu wema, maana hiyo ni roho ya Mungu, fikiria dhambi za Adamu pale edeni lakini uchukue moyo wa Mungu baada Adamu na Hawa kukosea nini kilitokea, baada ya maneno hayo akamalizia kwa kusema hivi.

Mbegu ya wema inaweza kuchelewa kumea kwa sababu ubaya na uovu una nguvu katika sura ya nje lakini kwa sababu wema huwa una nguvu ya ndani na mizizi yake ni 
1. Upendo 
2. Utu
3. Amani
Basi hata kama utaonekana kwa sura ya nje ni dhaifu ipo siku moja nguvu yake itaonekana katika matokeo ya matendo yake, Mungu alikasirika sana, alichukia sana kwa makosa ya watu ambao aliwaamini, walimwangusha lakini mwisho wa siku nguvu ya upendo, Thamani, Mungu aliona hakuna kitu naweza kufanya zaidi ya kusamehe na kuanza upya na ndiyo matokeo ya ulimwengu tulio nao.

Baba amelala lakini watoto wake tunakula matunda ya matendo yake kwa watu ambao kwa asilimia kubwa sio ndugu zetu, sio watu wa kabila moja na sisi wala si watu tunaotoka nao ukanda mmoja, sisi sio matajiri kwamba watu wanatupendea utajiri wetu, wala baba hakuwa tajiri bali alikuwa na moyo wa upendo na utu sana.

Mzazi/Mlezi/kiongozi, Boss, mwajiri jifunze kuwatendea watu mambo mema, waelekeze, waonye kwa nia ya kujenga sio kukomoa, saidia watu kama unajua sio kujifanya mjuaji kwa lengo la kuumiza wengine.

Kama ambavyo mbegu njema yaweza kuota na kuleta matokeo basi fahamu hata mbegu ya uovu huota na kuleta matokeo yake pia. Tofauti ya matokeo ya hizi tabia mbili moja hunufaisha hata kizazi chako bali nyingine inaweza kuwa chanzo cha kuumiza kizazi chako ukiwa wewe umelala.

Jifunze kuishi vyema, matendo yako yawe yenye lengo la kujenga zaidi kuliko kuangamiza, hakuna faida utapata ukimuumiza huyu wala hakuna tuzo ya kuwaumiza wengine bali unachimba kaburi la watoto wako na kizazi chako cha kesho.

Kuna vijana wanapitia magumu kwa sababu ya wazazi wao, wanakosa nafasi kwa sababu ya tabia za wazazi wao, watu wanasema watu wa ukoo huu ni wabaya sana mkiwapa nafasi itakuwa kama baba yao alivyokuwa, masikini ya Mungu kizazi chako kinaumia kwa sababu ya matendo yako mabaya.

Kuna nafasi ya kubadilika, uyafanyao leo sio ujanja, wala haimanishi wewe una akili nyingi kuliko wengine, hata ambayo unayafanya kwa siri, unawaficha wanadamu lakini Mungu aonae sirini anajua na ipo siku matokeo ya maamzi ya kuumiza watoto wengine itazaa matunda tu hasa kama hatotokea mtu hapo katikati wa kuvunja hiyo chaini ya chuki na ukatili dhidi ya wengine.

Saidia watu kwa lengo chanya, onya watu, adhibu watu kwa lengo la kujenga sio kukomoa, duniani tunokosea hakuna mkamilifu duniani ila tunasaidiana kwa upendo ili kuendelea kutunza amani na furaha zetu.

Chagua leo ni mbegu ipi bora kwako kati ya hizi mbili ?