Saturday, June 25, 2022

IS UP TO YOU

Ni ngumu sana mtu akikusimulia hadithi ya maisha yake, historia yake, familia yake na hata eneo analotoka. Historia inaweza kulazimishwa kuwa sio kweli kwa sababu tu ya mwonekano wa mtu katika wakati wa sasa lakini ukweli ni kwamba kuna watu wana historia ngumu sana za maisha yao ya utotoni, familia na hata jamii wanayotoka kwa ujumla wake.....

Kichwa cha andiko hili ni "IS UP TO YOU" kwa Tafsiri isiyo rasmi sana katika lugha yetu pendwa ya kiswahili ni JUU YAKO. Histori sio sababu ya kushindwa kuwa unavyotaka au kuwa ninavyotaka. Wataalamu wa uchumi na fursa wanaandika kuwa "Every human being has an equal chance to utilise the opportunity available in this World" kwamba kila mtu Ana nafasi sawa na binadamu mwingine inayoptaika chini ya Ulimwengu huu.

Nikiikataa hali kwa vitendo na kutokuridhika nayo kwa vitendo ni rahisi zaidi kuifanya jana yako kuwa Histori na sio maisha yako tena, kwa sababu tu, hakuna aliyezaliwa kuwa kwenye aina Fulani ya maisha, sijazaliwa kuwa tajiri bali nimepewa fursa ya kuwa namna nataka, sijazaliwa kuwa masikini ila nimepewa fursa ya kuugeuza umasikini wangu kuwa namna nataka mimi ili mradi naishi kwenye dunia yenye fursa sawa kwa wote.

Nimesoma historia ya sadio Mane, moja kati mastaa wengi kwenye ulimwengu wa soka, ambae pamoja na kwamba sasa ni miongoni mwa mastaa wakubwa ulimwenguni kwa upande wa soka, lakini ukweli ni kwamba yeye ni kati ya vijana wengi wanaotoka kwenye familia masikini sana kwenye bara letu la Afrika, ametokea familia, kijiji kisichotia matumaini hata ya kuwa na uhakika wa kula mlo mmoja, kaya masikini zenye kunuka umasikini kwa kiwango cha juu sana...

Bambali ni kijiji maarufu sana kule Senegal, na umaarufu huu umekuja kwa sababu ya Sadio Mane. Saidio Mane, ameitanbulisha Bambali dunia kupitia 
1. Kuamini kuwa dunia ina fursa sawa..
2. Kukataa kuishi maisha ya wazazi wake 
3. Amekubali  kuwa game changer...
4. Ameigeuza Histori ya kwao kijijini Bambali kuwa sehemu ya tumaini jipya kwa vijana na jamii kwa ujumla...

Akiwa katika umri mdogo, wazazi wake walitamani sana, mtoto wao kuwa Mhadhiri wa chuo kikuu kwa sababu is good paying job, lakini waliamini ndiyo ingekuwa njia bora ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini mkubwa katika familia yao....

Walichowaza ni shule, alichowaza Sadio Mane, akili ya Sadio haikuwaza kuwa na hela ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini, kujenga nyumba nzuri kwa wazazi wake na nyumba yake pia, hakuwaza gari moja au mawili, hakuwaza juu yakuwapeleka watoto wake shule nzuri kwa sababu ya mshahara wa Mkufunzi wa chuo kikuu, Sadio hakuiona furaha kupitia chaki za chuo kikuu bali....

Naisoma vyema haistoria yake, inasema baada ya wazazi wake kuwa na mtazamo tofauti na mtazamo wake, yeye akiwa na matamanio na imani kuwa miguu yake ndiyo utajiri wake kipawa chake, ni ndiyo utajiri wake, na miguu yake ndiyo utajiri halisi wa kuitoa familia na jamii yake kwenye giza nene la umasiki hivyo mshahara wa mkufunzi wa chuo ni kwa ajili yake na familia yangu ila sio kwa ajili ya Vijana na wakazi wa Bambali nyumbani kwao....

Hakuona fahari kuishi kwenye nyumba nzuri iliyozungukwa na nyumba za majini na tembe, hakuna furaha ndani yake......aliamini kuwa yeye ni game changer, he will, and he will make sure Bambali is place where all dreamers will live their dreams....

Baba na mama hapana, nataka kuwa mcheza mpira mshughuli, kipaji changu ni mtaji wangu, kipaji changu ndipo maono ya Baba yangu wa mbinguni ameyafungamaisha, hivyo siwezi kuishi matamanio yetu, sitaki kuishi tittle na fahari ya watu, bali nataka kuishi lile kusudi la Mungu kupitia kipaji changu...

Sioni furaha moyoni kuwa Lecture, mimi sikuzaliwa kuwa mwalimu, sikuzaliwa kuvaa suti wakati natimiza majukumu yangu, mimi ni mpira wa miguu, miguu hii ndiyo italeta mabadiliko katika familia yangu na kijiji kwa ujumla......

Baba na mama hapana, tunataka uwe mhadhiri wa chuo kikuu, ni kazi nzuri sana yenye malipo mengi na posho za kutosha, utatusaidia wazazi wako na wadogo zako, hatutaki kukuona unacheza na kuongelea mpira....

Siku moja alitoroka kwenda Dakar mji mkuu wa Senegal kwa ajili ya kuanza safari ya ndoto zake, a man from a very dark place, a village guy but he trusted his mission and he commented because he believed and he was seeing 👀 what is behind his foots

Toroka hiyo haikuwa kwa sababu yake bali kwa sababu ya Bambali, na Senegal kwa ujumla. Mungu alimtazama Sadio Mane, moja kati ya vijana wa kiafrika mwenye kuishimu na kuishika dini yake ya kiislamu kwa kwa ratiba na kanuni zote katika dini yake.

Leo nilipokuwa nikisoma historia hii kubwa kabisa, ilinipa nguvu na shauku yakukushirikisha kijana mwenzangu kuwa, haku giza mbele yako lisiloweza kuondolewa na mwanga, haijalishi uzito wa giza, haijalishi ni ukubwa wa mlima mbele yako kwa kiwango gani, cha msingi ni kuamini na kuchukua hatua ya kuanza kuufukuzia mwanga mbele yako....

Kuna wakati nilijiona nisiye na faida, niliona kila kitu hakiwezekaniki duniani, niliona na kuhisi kuchoka kimwili na kiakili lakini, historia ya Mane inanifanya kuinuka kwa nguvu na ujasiri mkuu nikiamini kuwa my dreams are in my authority and nobody can take it away from me by any means.....

Mazingira ya vijana wengi wa kiafrika historia zetu sio rafiki lakini tusimame na kufuta vumbi la umasikini wa familia zetu, tuishi kuwa wakubwa kwa sababu tumeumbwa kuwa wakubwa na inawezekana kwa sababu wea re the champion
Champions 🏆 
Hero 
Historia changer
Stand and take a step
0719110760
0755632375
Visit my new Page on Instagram @amaris_media1
@moses_mgema
www.mosesmgema.blogspot.com


No comments:

Post a Comment