Saturday, October 12, 2019

ULIZALIWA KUTATUA CHANGAMOTO/YOU WERE BORN TO SOLVE CHALLENGES.

Your a problem solver.......
Wakati mwingine ni ngumu kuelewa mtu anapokupa scenario ya changamoto Fulani amabayo anapitia, au amewahi kupitia kwenye maisha yake.
Unaweza usimwelewe sana kwa sababu unahisi jambo hilo ni dogo au hakuna binadamu anaweza kuchomoka kwenye changamoto ambayo amejaribu kukusimulia, hii ni kwa sababu inaonekana kuwa kuubwa sana.
Kuna mambo mtu anapitia kwenye safari yake yake ya maisha akikusimulia unaweza kusisimkwa na mwili na hata mwili mzima.
Lakini kiukweli maisha bila changamoto maana ya maisha inakosekana kabisa, watu wanakwenda shambani, maofsini, shuleni, na kila mahali lengo ikiwa ni kutatua changamoto.
Unalowa na mvua, unachomwa na jua, miiba na kadhia mbalimbali lengo ni kutatua changamoto njaa.
Watu wanakwenda maofsini mapema, wanachelewa kulala wakiwa wanafanya mambo Fulani lengo ni kutatua changamoto.
Maisha hasa maana yake ni Changamoto, huyo ndiyo maana ya maisha kwenye dunia hii
...........................
> Huwezi kuwa bora bila kupitia changamoto.
> Ubora na uwezo wako huwezi julikana bila kutatua changamoto Fulani kwenye maisha.
> Waliofanikiwa walitatua changamoto na matatizo ya watu kwenye jamii ndiyo zikawafanya kuwa hapo walipo.
>Kuna watu wanafurahia maisha lakini nyuma ya furaha hizo kuna watu walitatua changamoto.
√••••••••••
Mwanadamu amejengwa na ameaminiwa na Mungu kuwa problems solver. Kwa hiyo kama kuna changamoto unapitia basi mshukuru Mungu kwa kuruhusu changamoto hizo.

Usiruhusu changamoto zikakurudisha nyuma, zikakukatisha tamaa, na kukuondoa kwenye mipango, malengo na maono yako.
Wapo watu makazini, mashuleni kwenye biashara wao ni kukatisha watu tamaa, hawakubali kazi zako, wapondaji, wanakudharau nk. Yote hayo yabaki kuwa mawe ya kukanyaga na kukuvusha kwenda ng'ambo ya pili.
Huwezi kuwa imara kama

YAWEZEKANA WEWE NI KATAPILLA, SOMA NA KUJIJUA WEWE NI NANI....

*-MFUMO WA MAISHA-*
•Dunia imeubwa kwa mgawanyo sawa wa muda, majira na nyakati, mpangilio wa kizazi kimoja kwenda kizazi kingine.
•Mzazi mmoja kwenda kwa mtoto na mtoto akileta mjukuu, vitukuu mpaka vilembwe, dizaina na mratibu wa mambo yote haya ni Mungu.
•Uwepo wa mtu kwenye kizazi Fulani, kwenye miaka Fulani lilikuwa kusudi, majira na wakati sahihi wa kila mtu kuwa tumboni mwa mama hatimae duniani kwa mwaka, sikunde, dakika saa, Siku, wiki mwezi,mwaka kwa muongo, karne na millennium pia.
• Waliozaliwa miaka ya mwanzoni mwa 1900, hao ndiyo Mungu aliwaamini kuwa hadi kufikia wakati wa Tanzania inataka kuwa nchi huru wataweza kupambana kwa hoja na watu kutoka bara Ulaya na nchi itakuwa huru.
• J.k. Nyerere na wenzake wakazaliwa na hatimae kukuwa, kwa ushirika wao walipambana na watu toka Ulaya, walionekana sokwe, wajinga, wapuuzi, waliumia, walibaguliwa na kuteseka lengo ikiwa ni kuhakikisha nchi yetu inapata uhuru na hatimae baada ya miinuko, miiba, jua, makorongo, milima na changamoto zote toka enzi za kina kinjikitile Ngwale, Mangi sina, na watawala wa kichifu ambao walikutana na ukatili wa kijerumani Leo Tanzania imekuwa nchi ya watu weusi na hata tunaona fursa za kusema na kufurahia kwa sababu ni wakati wetu na sisi.
• Tukiwa na matajiri na watu wa aina mbalimbali hapa nchini Leo kina Nyerere, chief mkwawa, Kijikitile Ngwale na wengine hawapo tena duniani na wakati mwingine uzuri wa Tanzania hawaujui kabisa wamelala na zama zao zimepita.

•√MFUMO WA MAISHA.......
•Mfumo wamaisha umegawanyika katika makundi tofauti tofauti, na mgawanyo huu umekuja ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pakuishi na kufurahia zawadi ya Mungu ambayo ni pumzi ndani yetu.
• Kuna watu wamekuja kama waandaji wa mazingira ili wengine wafurahie ndiyo maana walizaliwa katika kipindi ambacho kila mtu WA kizazi hiki anajiuliza ni kwa namna gani watu waliweza kuishi enzi hizo ?....Je maisha bila simu, internet, lami, ndege nk yaliwezekanaje ?.
• Yaliwezekana kwa sababu kwa majira na nyakati Mungu aligawanya na kila mtu kwa kizazi chake aliaminiwa kuishi kwa miaka na karne yake na waliweza kwa sababu waliumbwa kwa muundo wa kuyaweza na kuyakabili maisha na mazingira ya kizazi chao.
• Wengine wameumbwa kama makatapilla na walishushwa duniani kwenye Yale mazingira magumu ampapo Hummer, Range, Harrier, Scuba, Subaru, Prado, Rav4, nk visingeweza kumudu mazingira hayo...
• katapillar likaja kuyakabili mazingira hayo na kusafisha, kushusha milima, mabonde, kung'oa visiki, kufukia mashimo, makorongo, kupasua miamba, na kuhakikisha kwa kiasi Fulani levo inakuwa sawa kwa ajili ya magari mengine.

• Baadhi ya watu ni makatapilla kwenye maisha, wapo kwa ajili ya kuwatengenezea wengine mazingira na barabara nzuri.
• Katapilla hukutana na visiki, miamba, makorongo, milima na miinuko mingi na kwa sababu hiyo hulazimika kung'oa, kupasua miamba, kukata miti, kufukia mashimo, makorongo na kusawazisha vyema na kisha kuweka jamvi zuri lami nk.
• Hivyo basi kama wewe uliishi maisha ya katapilla au unapitia maisha hayo kwa sasa usipende sana au kulazimisha na wengine kuishi maisha hayo wakati unyoofu na usawa wa barabara upo levo tayari.
• Acha wengine wafurahie ubora na uzuri wa barabara hiyo, wasimulie na kuwambia changamoto ulizopitia ili kuwapa changamoto ya kuilinda na kuitunza barabara hiyo vizuri, usilazimishe na wengine wapitie mapito uliyopitia wewe kwa kuwanyanyasa, kuwa mbabe, na kutumia nafasi ukiyonayo kuwaumiza wengine bila sababu za msingi.
• Kumuumiza, kumnyanyasa, na kutaka afanye matakwa yako hata kama anaona hatari mbele sio sahihi, wala humjengi Bali unajiumiza mwenyewe ukizani unamkoa kumbe unajiumiza wewe mwenyewe.

• Mtu hafundishwi kwa manyanyaso, masimango Bali hufundishwa kwa utaratibu mzuri na kupewa nafasi yakuonyesha ubora wake.......Ubabe, kutumia nafasi za utajiri, uongozi kuwanyanyasa na kuwadidimiza wengineo sio sawa na lazima ukumbuke kuwa maisha ni kama jua tu huanza kwa upole na kufurahiwa na watu lakini saa nane hakuna awezaye kukaa juani, na jioni jua huwa tamu na kila mtu aweza kulifurahia tena.
• Ndiyo maana Yesu alifanyika katapilla kwa niaba yetu, kilichobaki kwetu nikufuata misingi bora ya Imani ambayo aliyeileta aliumizwa nayo na leo tunafurahia.
• Katapilla Yesu alichonga barabara, alichomwa na miiba, walimpiga mijeredi, wakamtemea mate yetu, lakini kumvisha taji ya miiba kichwani ili Mimi na wewe tuwe tulivyo leo.
• Fikiria kama huyu Mungu angetaka kila mtu alipie pumzi yake ingekuwaje nafikiri hakuna angeweza kuishi.
• Kama wewe ni tajiri, kiongozi au mzazi usipende waliokuja na kukuta Mungu ameshakuinua kuwanyanyasa, kuwakandia na wakati kuumiza nafsi zao bila sababu ya msingi.
• Wambie kwamba haikuwa rahisi kuwa hapo ulipo, ulipitia changamoto nyingi, ambazo leo ndiyo zimekufanya ukawa hapo, hivyo kila mtu afanye kazi, asome kwa bidii na kutimiza jukumu lake sawasawa ili kulinda hatua ambayo mmenikuta nayo na ikiwezekana kwa sababu sasa haupo pekee yako, uunganishe nguvu na team yako kufikia malengo makubwa zaidi.
Note.....
Kama wewe ni boss, mzazi, kiongozi tumia changamoto ulizokutana nazo kuwakumbusha tu kwamba kuna milima mirefu, miamba, miiba nk. Mpaka kufikia hapo ulipo.
•Changamoto ni maisha ya mwanadamu ila  kwa majira na nyakati zina changamoto zake.
• Kama ulikuja mjini na madaso, usilazimishe na wengine wavae madaso wakati mitumba ya wachina imejaa k/koo.
Katika yote Mungu ndiyo msingi wa yote.
Kama umebarikiwa wewe basi wabariki na wenzako kwa wema na Mungu atakujazia
Prepared by
Moses Zephania Mgema
0755632375/0715366003
mgemamoses@gmail.com
mosesmgema.blogspot.com

Sunday, October 6, 2019

KILE CHA ZIADA NDO DUNIA INAKIHITAJI KUTOKA KWAKO, SIO ELIMU , KIPAJI NK KATIKA KARNE HII.......BALI KILE KINACHOKUFANYA UWE TOFAUTI NA WENGINE.

-Kila kijana anatamani kuwa mtu fulani kwenye maisha yake, leo, kesho hata kesho kutwa
- Ni furaha ya kila mtu kutimiza mambo yafuatayo....
1. Ndoto na malengo.
2. Kuwa na fedha na kazi nzuri.
3. Kufanya kila kitu unachokitaka.
> Pamoja na kutamani yote hayo lazima kama vijana tujikumbushe haya yafuatayo....
1. Dunia ya leo haitafuti mtu wa kusaidia katika eneo lolote la maisha Bali mtu mwenye kuleta na kuongeza ufanisi.
2. Dunia ya leo inahitaji ulicho nacho cha pekee (Your uniqueness) mfano kwa nini tukuajili wewe kati ya maafsa masoko 200 ambao wanataaluma kama yako, nini cha ziada kwako ambacho wengine hawana.
3. Wewe mwimbaji kwa nini uje wewe wakati kuna waimbaji wengi wanaoimba aina ya mziki wako.......nk.

åDunia ya leo ina kila aina ya watu inaowahitaji, wamejaa hawana kazi, wanafanana kwa minajiri ya taaluma, wanavipaji, kila eneo wapo, kitu ambacho kimepelekea kwamba Watu ndo watafute kuliko wao kutafutwa.

å Miaka ya nyuma, mtu angeajiliwa ikiwa hajamaliza darasa la 7, mtu angeenda form one akiwa na kazi lakini leo kila mahali pamejaa na maofsi hayahitaji watu tena Bali watu wanazihitaji nafasi ambazo hazitoshi tena.
√•. Shahada na Masters  sio sababu tena ya mtu kukupa kazi kwa sababu watu wa aina yako ni wengi sana wamejaa kila kona.
å Kumbe nini sasa kinaweza kukupa thamani na kukufanya uhitajike zaidi na hii dunia ni (Utofauti juu ya ubora, maarifa ya ziada, ujuzi na ubunifu wa pekee ambao wengine hawana.
å Leo kuna watu hawana hata elimu ila wapo kwenye nafasi nzuri sana na wanakula maisha kwa sababu tu wameweza kujitofautisha na wengine, wamejiongeza na kujitengenezea thamani na mazingira ya kuhitajika zaidi kuliko watu wengine.
√•  Cha kwako cha ziada ni kipi....tunatafuta MC, msemaji wa makongamano, mwalimu, mwimbaji, Daktar, mshauri wa ndoa na mambo ya kijamii nk. Kipi kinatufanya tumwache wa karibu na mwenye bei ndogo na kukufuta wewe wa mbali.
å kwa nini tukuajili, kwa nini tukupe milioni kumi kwa mwezi, kwa nini uwe mtu Fulani.
å Ni kwa sababu ya kitu kidogo tu kinachokufanya uhitajike *-UWE WEWE-* kile kidogo kinachokutofautisha na wenzako wenye kipaji, elimu, sawa na wewe.
åkwa nini wanunuzi wa mahitaji waje kwako sio kwangu wakati wote tunauza madafutali na kalamu za aina moja, kwa nini nije kushona kwako sio kwa James, kwa nini nije kula kwako sio kwa mama John........?
> Kile kitu cha ziada ulichonacho chenye ubora ndo kinachonifanya nije kwako, Lugha nzuri ya biashara, huduma nzuri ya chakula, usafi na nadhifu, kujali na kuthamani wateja ndiyo sababu inayonifanya kuja kwako.....
Je kama wote tunawahudumia vizuri wateja zetu nifanyaje....
>Mfanye kuwa rafiki wa karibu
> Tumia mapungufu ya mwenzako kuwin.
å Dunia ya leo imejaa changamoto na ushindani wa hali ya juu katika kila jambo so ni vyema kujitofautisha kwa mtazamo chanya kwenye kila kazi unayofanya.......
Dhahabu ni Dhahamu hata kama inaonekana kufifia kwa sasa, ila huwezi kuilinganisha na kioo hata kama kiooo kinang'aaa kiasi gani..
BE YOU
BE UNIQUE
BE DIFFERENT
WALK ON WHAT OTHERS ARE SHOWING WEAKNESSES.
USE EVERY OPPORTUNITY WHICH COMES AHEAD OF YOU EFFECTIVELY.........
MAKE PEOPLE TO NEED YOU TO SATISFY THEIR NEED......

Prepared by
MO_MGEMA........INSTA
Moses Zephania....FB
0715366003.......WHATSUP
Dar ea salaam