Sunday, May 19, 2019

THAMANI NA FAIDA YA UTULIVU WA AKILI KATIKA MAAMZI NA MAISHA KWA UJUMLA

Hello Friend.
Rafiki na ndugu yangu nikushirikishe jambo hili la thamani na lenye maana sana kwenye maisha yako.

Kwenye maisha ya kila siku kuna mambo mtu anakutana nayo, mazuri kwa mabaya, ambayo yanamfanya kuishi kwa amani na furaha au kama ni Magumu au mabaya yanamfanya kuishi kwa kukosa amani, furaha na utulivu kuanzia kwenye akili mpaka huku nje.

Nikuambie leo rafiki tangu, kukosa utulivu, amani na furaha ya akili, inaondoa uwezo wa kufikiri sawasawa na sahihi na hii inapelekea kuondoa afya na ubora wa akili yako.

Matokeo yake unajikuta unaamua vibaya kila jambo na kuleta athali kubwa kwenye mfumo mzima wa maisha yako.

Changamoto zipo, ugumu wa maisha upo, wakati mwingine unafanya kazi kwa bidii, maarifa, ujuzi na kwa kila namna lakini hatua unayopiga ni ndogo au wakati mwingine hakuna kabisa.

Nikuambie kitu................

Utulivu ni jambo moja la msingi na muhimu sana kwenye maisha ya mtu kwa sababu ukiwa na utulivu wa akili na nafsi pia itatulia, matokeo yake sasa ni......
1. Utaamua vyema
2.Utaona njia ya kutatua tatizo/ changamoto hiyo
3. Maamzi yako hayatakuwa na matokeo hasi.
4. Kiwango cha Maamzi sahihi kitakuwa juu
5. Afya ya akili na nafsi itachukua nafasi yake.
6. Utaona watu/Mtu sahihi wakumshirikisha changamoto yako na wakati mwingine kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo.
7.Utajenga ujasiri zaidi na kujiamini hata wakati mwingine hutayumbishwa na aina yoyote ya changamoto hata itakuwa ngumu kiasi gani.
8. Utakuwa msaada kwa wengine
9. Utaishi kwa tumaini na kujiamini vyema
10.Hutoyumbishwa na mazingira hata yaweje.

Kwa ujumla utulivu unafaida na thamani kubwa mno kwenye maisha ya mtu ya kila siku.

Hivyo usikubali tatizo, au aina yoyote ya changamoto ikakuondoa kwenye utulivu, ingawa kuna matatizo ambayo ukiyapata hakika yanaumiza na kukatisha tamaa lakini bado utulivu na hekima ukiruhusu vitawale na kuzuia Maamzi ambayo yanaongozwa na mazingira, mihemuko, na maumivu basi kwako itakuwa kheri.
Be blessed so much for reading this beautiful message.
Musa Zephania Mgema
0715366003/0755632375
mgemamoses@gmail.com
mosesmgema12.blogspot.com
Dar es salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment