Saturday, May 18, 2019

NI WEWE MWENYE MAAMZI NA MAISHA YAKO.

Hello Friend.
Nia yakufikia ndoto na malengo yako unayo wewe mwenyewe, lakini changamoto na vizuizi vimekuwa vingi na wakati mwingine ni vikubwa kuliko nguvu na uwezo ulio nao wewe, na kuna wakati unafikia mahali unakata tamaa. Lakini ni............

Mambo machache unapaswa kujifunza na kuelewa kwamba, haya yote yanakuja kwa sababu kwanza, Mungu amekuamini na ana uhakika kabisa kwa nguvu na uwezo alioweka ndani yako unaweza kukabiliana na aina hizo za changamoto na wewe ndo mtu sahihi kupitia changamoto au milima hiyo ya maisha.

Lengo ni kwamba anakunoa ili uwe kisu kikali zaidi ambacho kitakuwa na uwezo wakulalua kila aina ya jambo liliko mbele yako.

Huwezi kuwa mwalimu mzuri wa nyimbo, ujasiriamali, mambo ya kijamii, huduma kwenye nyumba za ibada bila kupitishwa.

Huwezi kuwa mwandishi, public speaker, motivational speaker simply, huwezi kumiliki fedha kwa njia rahisi kesho utashindwa na utaanguka na kukata tamaa na kufa kabisa.

Dhahabu haiwezi kuwa dhahabu safi bila kupita kwenye moto, moto unaifanya ing'ae na thamani yake kupanda na kila mtu kuihitaji kwa gharama yoyote ile. Ndivyo ilivyo hata kwenye maisha yetu kama binadamu.

Tunakuwa vizuri zaidi kwenye maeneo ya kazi zetu, kwenye matumizi ya vipaji vyetu pale tu inapotokea umepambana sana kufikia mahali ambapo ulitamani kuwa hapo kabla.

Mapambano ya muda mrefu ambayo ulikutana nayo njiani, ndiyo sababu ya wewe kuthamini kazi uliyo nayo, kipaji ambacho wengine wanacho ila bado hawajafika pale ulipo wewe Leo na wanatamani siku moja wawe hapo lakini bado wako mbaaali sana.

Kwa hiyo usikatishwe tamaa na vikwazo vichache vilivyopo njiani, pambana hakikisha focus yako iko klia isiyoyumbishwa na pepo za kiangazi ambazo zina mwisho na masika yaja.

Usiyumbishwe na kelele za watu hasa ambao wamefanikiwa na kushindwa, maana kila mtu anamtazamo na mawazo yake, hivyo ukiwasikiliza utapotea maana miruzi mingi humpoteza mbwa asie na mmiliki bali mbwa anaemjua bwana wake huitambua sauti ya mruzi wa bwana wake, kwa hiyo usie mbwa mwitu asie na bwana wake.

Maamzi ya kufika mbali kihuduma, kibiashara na kwenye eneo lolote ulilopo iko mikononi mwako, hakuna mtu anaweza kuyaamua maisha yako yaweje kesho isipokuwa wewe mwenyewe, sio mazingira, sio Sera za nchi sio changamoto yoyote bali ni wewe.

>Maamzi yako ndiyo dira yako
>Malengo yako ndiyo dira yako
>Kichwa chako ndo dira yako
>uwazavyo ndivyo unavyoiamua kesho yako.
>Uwezo na kipaji ndani yako ni urithi wa Mungu.

Mwisho
Jitathimini na kujipambanua kama unaona kuwa unapita kwenye njia sahihi ya kuifuluzia ndoto yako

Moses Zephania Mgema
0755632375/0715366003
mgemamoses@gmail.com
www.mosesmgema12.blogspot.Com
Dar es salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment