Tangu mwanzo wa muundo wa dunia, ukisoma historia ya dunia kwa mfumo wa maisha ya kawaida, kwa mitume na manabii walipitia changamoto, shida, vikwazo vingi mpaka kufikia malengo, ndoto hata mafanikio ya ambacho walilenga kukifanikisha hapa duniani.
Ndivyo ilivyo hata kwenye ulimwengu tulio nao leo, mafanikio ya kila mtu yamezungukwa na vikwazo, changamoto, mambo mengi ya kukatisha tamaa, kiasi kwamba sio rahisi kupasua na kufikia malengo na ndoto kama utaruhusu changamoto hizo zikuondoe kwenye njia.
Dhahabu haiwezi kuwa dhahabu kama haijapitia mchakato sahihi wa kupatikana. Ni nini maana yake: Ni kwamba kitu chochote kizuri kinahitaji mtu kujitoa, kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi mkubwa ili kufikia kitu au jambo hilo zuri.
> Ili ufaulu masomo inakulazimisha kusoma kwa bidii na kwakutumia muda mwingi kusoma, kujadili na kujiepusha na mambo mengine ambayo yanaweza kuwa sababu ya wewe kufeli.
>Ukitaka kuwa mwimbaji mzuri unahitaji muda mwingi wa kufanya mazoezi, kusikiliza wengine wanafanya nini, kujifunza kila wakati.
>Ukitaka kuwa tajiri na huna misingi mizuri ya mitaji, huhitaji aibu katika kupambana ili kuweza kutoka mahali ulipo kwenda eneo lingine ambalo unataka kufika, utafanya kazi zisizofaa kwa macho ya kawaida lakini ndo unapaswa kufanya ili kesho yako iheshimike.
>Ukiwa na mtaji na unatokea mazingira mazuri kiuchumi and you're well supported lakini bila kuwa makini, kujinyima, kuongeza ubunifu kwenye biashara au kazi yako utajikuta unafeli.
√ Kwa hiyo unahitajika kufanya kazi kweli kweli katika eneo ulilopo, lakini pia kumbuka yako mengi magumu na yakukatisha tamaa kama hutojipanga kukabiliana nayo unaweza jikuta unaishia njiani,
Chakufanya...........
Kumbuka kuna nyakati ngumu na majira magumu ambayo ni kama Mungu haoni jitihada, nguvu, na maarifa mengi unayotumia ili kuyafanya maisha yako kuwa bora na mazuri
Kumbuka hata katika hayo Mungu amekuamini, hali yako uliyo nayo leo ni ya muda tu wala siyo ya kudumu, cha msingi endelea kupambana, kufanya kazi kwa bidii katika nafasi uliyopo, omba Mungu ipo siku utafanikiwa na kuwasimulia wengine.
> Changamoto ni silaha yako
> Mungu amekuamini na anajua unaweza. Kuna wakati tunapitia maisha yakuumiza kuondokewa na watu wakaribu, Baba, Mama, mke, kuachwa na mpenzi au mke/Mume lakini yote hayo yanakuja kwa sababu Mungu amekuamini sana.
> Don't be taken away from your focus, plans, kimbia kwa kadiri uwezavyo hiyo ndiyo silaha yakufikia unapotaka
Yesu aliumia na alipitia mateso kufikia lengo why not you ?. Zifanye changamoto kuwa sehemu za maisha na huwezi kuzimaliza na kila hatua unayopiga ndo zinavyozidi kuwa nyingi lakini pia katika hayo njia za kutatua zipo.
Mungu amekuamini, usimwangushe chini, pigana, pambania mafanikio yako huo ndo msingi sahihi wa maisha ya mtu mwenye lengo la kutimiza ndoto zake.
Musa/Moses Zephania Mgema
mgemamoses@gmail. com
0715366003/0755632375
Dar es salaam, Tanzania.