Sunday, July 22, 2018

DUNIA MPYA YA KUJIAJILI NA MAFUNDISHO HASI JUU YA MFUMO RASMI WA ELIMU

Habari, imeandikwa na.....
Moses z. Mgema
Ulimwengu unakwenda kasi sana, mabadiliko na mifumo ya maisha ya watu kila siku  unabadilika sana, ongezeko la maendeleo ya sayansi na teknolojia umekuwa kwa kasi sana kiasi kwamba dunia si tu imekuwa ni kama kijiji kimoja Bali imesogea kabisa kwenye viganja vya mikono yetu.
Taarifa mbalimbali umepatikanaji wake umerahisishwa sana kwenye nyanja zote za Habari ziwe in Habari rasmi, michezo, burudani, kijamii, kidini, taaluma na masuala ya siasa, biashara na uchumi.
Kutokana na ongezeko la upatikanaji huu wa taarifa na Habari watu wamefunguka na wamejua mambo mengi ambayo hapo awali haikuwa rahisi kuyapata hasa kwa watu ambao hawakupata nafasi ya kwenda shule.
Upatikanaji huu wa taarifa umejenga jamii kubwa iliyo elimika na kujitambua kwa kiasi kikubwa sana.
Watu wamepata taarifa wamejenga maisha yao.
Na mambo mengine mbalimbali ambayo kwa hakika pasipo ukuaji wa technologia na mafumo wa Habari na mawasiliano sijui tungekuwa wapi.....
Lakini katikati ya ukuaji wa mfumo wa habari lakini pia watu wengi wanajaribu kuipotosha jamii kwa Habari ya taaluma rasmi hasa ukizi gatia kuwa mtazamo wa zamani ulimwandaa mtu kuajiliwa kuliko kujiajiri.
Ilifahamika kuwa MTU aliyekwenda shule alikuwa na uhakika wa maisha yake ukilinganisha na MTU ambae hajaenda shule maana huyu angepata ajira ambayo ingeendesha maisha yake.
Lakini leo hii idadi ya wasomi imeongezeka sana ulimwenguni, kuanzia Nchi za dunia ya tatu mpaka kwa mataifa yaliyopiga hatua kiuchumi na mambo mengine ya kijamii.
Kutokana na idadi hiyo kuwa kubwa uwiano wa ajira zinazotengenezwa kwenye mataifa hairingani kabisa na idadi ya wasomi wanaohitimu kila mwaka kutoka vyuo mbalimbali duniani.
Hivyo ongezeko la watu kutokuwa na ajira inazidi kuwa kubwa kila kukicha na suluhisho lake ni kama halipati ufumbuzi zaidi yake linazidi kuongezeka sana
Lakini kwa wasomi wenye kuelewa maana ya Elimu toka zamani bado haiwapi shida wala changamoto
Maana kuwa na elimu ni kuelimika, kuwa mfano kwa wasio wasomi, kuleta mabadiliko ya fikra na mitazamo kwenye jamii na kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yetu.
Wasomi wengi wamefanya ivo, lakini shida inatokea kwa baadhi ya watu kupotosha uma kuwa elimu sasa haina maana sana maana watu wanamaliza vyuo lakini hakuna kazi.
Swali dogo.......?
Nani alikuambia msomi ni wa kuajiliwa tu au nani kakuambia kwenda shule lengo lake ni moja tu ? Hapo tunakosea
Maana ya elimu
Ni kuelimika
Kupata maarifa
Kufungua macho na kuziona fursa nje ya ajira
Kuwafanya wengine wasio na taarifa kuwa na taarifa
Kuwa chachu ya maendeleo
Kutengeneza ajira kwa wasio wasomi.
Kuhamasisha watu kuona thamani ya elimu
Mwisho kuajiliwa kama last option.

Note.
Kuna watu mitaani hata kwenye social media wanahamisha kuwaaminisha watu kuwa sasa elimu haina thamani tena, hapana
Mtazamo wa elimu ni kuleta mageuzi ya fikra kwa mtu mmoja mmoja mpaka jamii kwa ujumla, kazi ni ziada.
Kwa hiyo tusidanganyike watu wakaacha vyuo au kutokwenda shule kabisa kisa ajira hakuna ajira zipo vichwani mwetu tutumie vizuri
Tuachane na wapotoshaji wasio jua kuwa hata maarifa na madarasa wanayosoma online ni maarifa ya waliopita shule.
Elimu ni msingi imara wa mafanikio kwa kizazi mpaka vizazi
Kuajiliwa kuna mwisho Bali elimu ni hazina kwa vizazi na vizazi.
Tuwapuuze, tusome zaidi
Ili kuiendelea kuifanya dunia kuwa mahali salama na penye furaha ya kuishi
"This place is the better place for everyone

No comments:

Post a Comment