Monday, January 22, 2024

Dunia imebeba mambo mengi sana, kati ya mambo hayo mengi kuna watu pia wa aina tofautitofauti, wazuri na wema lakini pia kuna wabaya au wasio na maadili.

Ulimwengu umetupa machaguo mengi ambayo yanatufanya kuchagua kwenye angle mbalimbali za maisha, na uchaguzi ambao tunafanya kwenye haya maisha hudetermine au kuamua either hatima na mwelekeo wa maisha kwenye angle husika, tulipokuwa watoto wazazi, ndugu na hata walimu wetu walitusisitiza sana kusoma kwa bidii ili kesho zetu ziwe bora, wazazi wakatuambia mambo mengi kwa habari ya ibada na mambo mengi.

Na kila mtu alivyochagua utotoni ndiyo ilivyo hata kwenye mwelekeo wa maisha yake ya sasa na yanayoendelea. Whether mazuri, yenye unafuu na tumaini au mabaya kabisa. It was a choice of everyone na uchaguzi huo huwa na matokeo yake.

The way i am ni kwa sababu ya jana yangu, hata kesho yangu itaamuliwa na leo yangu, how i make right choices and make a follow up on whatever i decide to make and follow the path. 

Katika nyakati hii: kuna mambo matatu ambayo as a man i need to make sure i decide well 
1. Eneo la maisha yangu na Mungu (Relationship with God).
2. Eneo la Finance (economy)
3. Eneo la mahusiano (Ndoa)

A man was created as visionary human being, vision bearer, Kiongozi, a man to support and make his family fulfl  its purpose as family (family purpose).

Ili familia iwe bora na hodari katika angle zote za maisha kuanzia mke, watoto na hata uchumi na mahusiano ya familia na Mungu basi it needs a strong man who knows his role and he is perfoming his duties perfectly.

Hivyo mwanaume mkamilifu na mwenye maono chanya, usahihi wake huanzia kwenye uchaguzi wa mke sahihi ambae ataambatana nae kwenye safari ya kujenga familia bora na imara katika maeneo yote ambayo nimeyataja hapo juu.

Unapokuwa kiongozi (Kwa nature a man is leader of a family) lazima pia ujue mtu sahihi ambae utaambatana nae katika ujenzi wa taasisi bora inayoitwa familia. Mfano raisi anapochaguliwa, moja ya kigezo cha kupima ufanisi wake katika kujenga mwelekeo wa nje ni katika eneo la uteuzi wa wasaidizi wake. Hao ndiyo hudetermine either atafanikiwa au ataanguka.

Hata kwenye familia kibiblia kabisa, mwanaume mwenye hekima, malengo, maono na mwenye kuitambua njia yake (Kama kiongozi)  basi hata uchaguzi wa mke wake mara zote huwa  ni wa viwango vya juu mno.

Nimeishi miaka 30 sasa tangu nimezaliwa, nimesoma, nimeokoka, nimejibidisha katika kusoma neno la Mungu ili kumwelewa Mungu katika cycle zote za maisha yetu duniani, nimesoma na kusikiliza kujua nafasi ya family kingdom ( kingship & Queenship) how it works successful and how can be in a hall of hell when you make a mistake as a family father. 

Imenipa somo zuri sana kupitia utulivu na kukubali kujigunza kwa unyenyekevu, uongozi wa familia, uongozi katika maeneo mengine ya maisha (Hapa nikatambua kuwa nahitaji kuwa Mume bora, Baba bora na kiongozi bora wa familia yangu, kuanzia mke, watoto wangu na hata kwa ndugu zangu both upande wa mke wangu na hata kwetu pia). Na hapa ndipo  nilimwambia Mungu sifa za mke wangu ni zipi when i was at the age of 20 after my A-level studies).

Ukizaliwa mwanaume mwenye sifa za kiume lazima uwe kiongozi bora, mfano bora, mwenye kuimarisha na kusapoti familia yako kwa asilimia 100, iwe katika ukame au ustawi you must be a strong man and who is fighting for the happiness and joyful of a family.

Ubora wa mume kwa mke na ubora wa Baba kwenye familia haupimwi kwa ubabe, mamlaka aliyo nayo, nafasi yake kama kiongozi, kuwapatia watoto na mke mahitaji yao ya chakula, kulala, afya na mahitaji mengine kama hayo, hapana pamoja na hayo yote, mume bora ni yule ambae anaweza kutambua uwezo na ubora wa mke wake na namna ambavyo anaweza kumsapoti, kumwi-encourage, to be there for her always na kuhuishi maono yake bila woga.

Hii imekuwa mission yangu siku zote na ndiyo maana hata kuingia kwenye mahusiano ya ndoa imenichukua muda mrefu sana kwa sababu wherever i think huyu ni yeye basi i came to find some missing katika kiwango kikubwa cha sifa za mke sahihi wa maisha yangu.

Ashukuriwe Mungu mwaka 2022 when i was asking God about geting this job, nilimwambia tu katika mahitaji yangu kwake ( 1naomba nipate kazi ni wakati mwingine sahihi kwangu, 2 ukinipa kazi nataka nioe ni wakati wangu sahihi kupata mwenza wa maisha ambae ana sifa nilizowahi kuandika 10 iliyopita).

The good thing nilipata kazi na mwaka jana january 2023 nilikutana na mwanamke ambae moyo wangu ulishuhudiwa huyu ndiye yule mwenye zile sifa za kwenye ile notebook ( It was 25 au 24 January pale fpct kibaoni.

It was a surprise to me kwa sababu nilikuwa kwenye mazingira ambayo haikuwa rahisi kwangu kuamini au kukubaliana na mazingira ambayo yalikuwa yanatokea lakini it was a time.

Imenichukua muda mrefu sana kukubaliana na hali ambayo sikuitegemea na ndiyo maana imechukua muda mrefu sana (mwaka) nakuambia tuonane naghairi au naweza kuja then napotezea tu kwa sababu kuna some issues i wanted to confirm from you na hata kwenye mazingira yangu menngine.

Sasa ni wakati sahihi sana
Agatha its a right time wa mimi na wewe kuanza mahusiano rasmi ili tuweze kufunga ndoa takatifu mbele ya madhabahu ya Mungu wetu.

Najua katika nyakati kama hizi huwa ni nyakati ngumu sana kwa mwanamke kuamua either kwa sababu yuko kwenye mahusiano mengine, au yuko dilema kwa sababu ya vijana wengi kupeleka maombi kwake, anaifikiria familia yake na namna ya kuamua kwa ajili ya kesho yake pia. Haya huwa ni maswali magumu mno ambayo mwanamke huwaza na kufikri na wakati mwingine kubaki bila majibu sahihi.

But i present this message to you kwa mara ya kwanza kabisa na kwa ajasiri kuwa wewe ndiye mke wangu wa maisha na i can't wait to see my the rest of my life spending with you Baby love.

You such an amazing woman, wanderful, charming with great love, passionate na mwenye huruma nyingi sana. It was year of studying you, it was a year of learning a lot from you, majibu Mungu hadanganyi na wewe ni mtu sahihi sana kwangu.

Nikupe uhakika wa mambo machache sana
▪︎Mimi kwako ni mwanaume bora sana. Zile sifa za mwanaume wa ndoto zako ni mimi.
▪︎Ninachokuhakikishia wewe ni kwamba, utakuwa ni miongoni mwa wanawake wachache ambao ndoa zao zitakuwa ni ndoa bora na za mfano.
Kwangu wewe ni malikia na sifa za malikia ni to have joyful life.
Nakupenda Agatha P. Andrea
Dada zangu wanakupenda and they can't wait to see you, ile picha ya moro niliyoweka status tulipotoka Moro was such an amazing to her.
Nakupenda  nakupenda tena
Allow me niwe mkwe wa Mama Agatha na Baba Andrea prosper.

Soon its soon

Wednesday, December 27, 2023

As you wish watoto wako waielewe misingi ambayo umeiweka kama mzazi vilevile chukua muda wako mwingi kuwasoma na kuwapa nafasi yakuwa karibu nao ili kuwafahamu zaidi.
Msingi wa malezi sio provision of food, health care, Education and all important needs only, hapana malezi bora ni zaidi ya hivyo vyote na mzazi bora ni yule ambae anatumia muda mwingi kujua misingi ya yule mtoto kuzaliwa ( kutambia kusudi la kuumbwa kwake) 

Sunday, September 24, 2023

IFANYE NDOTO HALISI YA MTOTO UNAEMLEA IWE KWELI L

Ndoto za watoto wengi wa Afrika zimeshindwa kuwa kweli kwa sababu ya watu waliopewa nafasi yakuwasimamia vijana na watoto wa Kiafrika, pengine ni mzazi, mlezi hata viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali, Mashirika binafsi ambayo yamekuwa yakifadhiliwa na mashirika ya ndani na mashirika ya nje kwa lengo la kuhakikisha watoto wanapata nafasi yakuishi ndoto na malengo yao.

● Wazazi/walezi kwa asilimia kubwa wamekuwa chanzo cha mauaji ya mtu aliyekusudiwa na Mungu kwa sababu ya nafasi zao kwa watoto na vijana wanaowalea. Ni jambo la kawaida kwa mzazi/Mlezi kutaka mtoto wake kuishi matakwa yake ambayo mara nyingi huwa ni yakutafuta hadhi na heshima kwa marafiki na jamii inayomzunguka. Hivyo kwa matakwa hayo basi analazimika kumtengeneza mtu asiye halisi kwa nafasi yake yeye kama mzazi au mlezi.

● Ni jambo la kawaida mtoto kuonekana hana akili darasani anapochagua kufanya masomo ya sanaa kwa sababu jamii yetu inaamini mtoto anapofanya masomo ya sayansi huyo anauwezo mkubwa wa kiufahamu ukilinganisha na wale ambao wanafanya masomo ya sanaa wanapokuwa shuleni, vilevile ni jambo la kawaida kwa mtoto/kijana kuwekwa kwenye kundi la watu wa hovyo, wasio na akili pale tu anapokuwa na matokeo yasioridhisha anapokuwa shuleni.

●Andiko langu halijajikita kwenye kufanya promosheni ya watoto kutokuwekewa mazingira ya usaidizi kwenye misingi ya kuonyeshwa njia bora za malezi hapana, andiko langu lina lengo lakukuonyesha wewe mzazi/Mlezi na wewe kiongozi wa taasisi za serikali/mashirika binafsi  unanafasi ya kumwonyesha njia bora mtoto wako kwenye ule wito mkuu alioitiwa na Mungu duniani. Pengine kwa macho ya hadhi wito wake haukuvutii lakini ndiyo eneo lake bora kuliko  maeneo ambayo wewe unaona kwa macho ya fikra zako ndiyo eneo sahihi la mtoto wako kufuata.

● Tumeua vipaji na karama za watoto wetu kwa sababu tumeacha wajibu wakufuata misingi bora ya malezi ambayo yanafanya promosheni ya kile ambacho mtoto amekibeba ndani yake ambao ndiyo uwezo halisi wa mtoto wako. Ni rahisi zaidi mzazi/mlezi kumzuia mtoto asipractice kipaji chake cha kucheza mpira, kuimba na mambo mengine ya vipaji kwa sababu yeye (Baba/mama/Mlezi) alitaka kuwa daktari na akashindwa basi anataka mtoto wake awe daktari ili kutimiza matakwa na ndoto yake kupitia mtoto wake.

●Ukweli ni kwamba ulichopewa wewe na Mungu sicho alichopewa mtoto wako kukifanya hapa duniani, hapa duniani kila mtu ana kusudi lake, wito wake na amepewa vifaa saidizi kulingana na kile ambacho Mungu alikikusudia kitokee kupitia yeye huyo mtoto wako, nje na hapo unalazimisha samaki kupanda mti na simba kuwa fundi wakuogelea.

● Ni kweli mtu anaweza kulazimishwa na mazingira kufanya kile ambacho sio kusudi lake na akafanya vizuri mfano mtoto anaweza kulazimishwa kusoma aina fulani ya professional, anaweza kufanya vizuri sana hata kuwa miongoni mwa watu bora katika hiyo kada lakini kila jambo tunalofanya duniani ambalo ni kusudi halisi la Mungu basi ndani yake huwa na passion nje yakuwa ni jukumu ambalo linapaswa kutekelezwa.
● Mfano nikiwa na passion yakuwa kiongozi, jambo la kwanza halitakuwa maslahi yangu binafsi nitatamani kuona nafasi yangu kama kiongozi inakuwa na matokeo chanya kwa wale ninaowaongoza kwanza kabla yangu, naweza kupitia maumivu makali sana, kwa mimi ni kiongozi basi nitakubali kupitia dhoruba na changamoto zote kwa ajili ya wengi. Nachukua mfano wa Yesu kristo mwana wa Mungu, the Role model of all Role modes duniani, yeye alikubali kuwa sadaka ili kuonyesha njia kwa sisi ambao ni wafuasi wake, si kwa kulazimishwa ila ni kwa sababu alikuwa mfano bora kwetu.

●Mtu akiwa anafanya kazi ambayo ni kusudi lake, kinachotangulia kwanza ni passion, kabla ya maslahi binafsi, uzuri wakufanya kitu ambacho ni kusudi lako, hata kama ili uweze kufikia ile pick, kiwango cha juu cha ubora kuna maumivu atayapitia lakini kwa sababu tu kuna ile nguvu ya asili ndiyo inayompa hamasa, bado imani na tumaini lakuifikia kile anakiona ataendelea kupush kwa nguvu, maarifa, uvumilivu, ubunifu na hata kama kuna gharama za ziada zitahitajika basi atatafuta namna ya kuhakikisha anagharamikia ili tu apate kile anachohitaji.

●Mfano nimehudhuria mafunzo ya huduma ya mtoto ambayo yamekuwa yakiandaliwa na shirika la compassion International Tanzania, nimekuwa nikijifunza jambo anaposimama Mkufunzi Ndugu Letema Laizer, namna ambavyo ule uhusika anavyouvaa na kile kitu bora anachokitoa kwa wanafunzi wake, lakini unaona ile passion aliyonayo katika kufanya kazi ya ukufunzi. Wakati mwingine kuna baadhi ya technical issues zinakuwa zinajitokeza wakati wa mafunzo lakini, he will always find ways to solve the problems whether in the night wakati nyie mmelala atafanya so unaona tu kuwa kando ya kuwa ni kazi yake lakini anaenjoy kuifanya na katika kuenjoy huko basi kuna toa kitu ambacho huleta picha halisi ya huduma ya mtoto kwa watendakazi nakuiona ile huduma ikiingia ndani ya watenda kazi kama sindano inayoingia na kutoa simu ambazo wanakuwa nazo wanapokuwa wametoka kwenye vituo vyao vya kazi kutokana na baadhi yao kupitia changamoto kadhaa zenye kuvunja moyo na kuondoa nuru ya huduma ya mtoto ndani yao.
●Mtu mwingine ambae ananisimamia mimi katika utekelezaji wa majukumu yangu, mzee wangu Raphael Lyela (Balozi) zile article zake haziji tu kwa sababu anajua ila ni kwa sababu ni kitu ambacho he was born to do, whether iwe kwa payless kwa maana ya fedha. Yeye anapoona ujumbe umewafikia vijana na kuona matokeo ya kazi yake ikibadilisha mentality ya vijana basi that is an enjoyment for him. Kuna matokeo makubwa sana kupitia program za vijana anazofanya kupitia whatsap groups, lakini zile Camps za Youthkingdom Ministry, amazing sana. Hapa sio pesa bali ule wito mkuu ndani yake ndiyo unaweza kuleta matokeo ambayo mwanzo haikuwa priority kwake.

●Ninachojifunza zaidi sasa ninapoelekea kuwa baba na nikiwa mlezi wa vijana kituoni, naona wajibu wangu mkuu ni  kuhakikisha nasimamia ndoto za vijana na kusimamia zichupue na kustawi kwa misingi ya malezi bora kwa vijana. Kuifanya ndoto ya mtu kuwa kweli sio jambo la kulala na kuamka tu ni kama ambavyo tunaweza kuandaa shamba, kulima, kupalilia, kumwagilia, hapo katikati kuna kamchakato fulani ambacho kinahitaji uvumilivu ili kupata matokeo tarajiwa.
●Changamoto tunayopitia walezi wengi, tunaishi kukariri mfumo fulani wa maisha, kutaka ile public popularity, sifa fulani mwanangu anasomea udaktar, anasomea uhandisi nk. Mambo hayo ni mazuri lakini kama yanapita kwenye njia au mfereji ambao sio wake hata utendaji wake kesho unaweza usiwe bora kama ambae ukiacha kuwa ni taaluma yake, na ni kazi inayomwingizia kipato basi huwa ni huduma kwa upande mwingine na hao ndiyo wako kujitolea kufanya jambo lolote akiamini kuwa kwa sababu jambo hilo liko ndani ya uwezo wake basi wataona alichonacho na hicho ndiyo kitamtambulisha na kumpa nafasi ya kutengeneza uhitaji kwa jamii/taasisi kupitia yeye. Mtu anaanza kwa kujitolea akiamini anahitaji jukwaa, (Platform kuonyesha kile alichonacho) akipata hiyo fursa basi mengine hubaki kuwa ni historia, i take some examples of Secular muscians hapa Tanzania, Harmonize alipata dakika tano mbele ya Diamond pale Dar live, Mbagala Zakiem na ikawa nitolee na aliamini anaweza, nani leo hamfahamu Harmonize hata kama sio mfuasi wa hizo kazi zake lakini umewahi kumsikia au kusikia nyimbo zake hata kwenye vyombo vya usafiri. Naturality is more power compare to Artificiality.

●Kwa hiyo Malezi bora sio kuwalazimisha watoto/Vijana kutembea kwenye mawazo na matamanio yako wewe kama mzazi/Mlezi/kiongozi wa taasisi lakini malezi bora ni kuonyesha njia penye lile kusudi la Mungu ndani ya mtoto au kijana unae mlea na kumsimamia wewe.

●Do not use your position as a parent/guardian or a leader to kill the dream of a child or young person. If you don't know something, look for solutions and more knowledge on how to nurture your child's potential.


Mimi ni kijana wa Balozi Raphael Lyela.
0755632376
0719110760
www.mgemamoses.blogspot.com

Monday, September 4, 2023

The story of life begins as, you live a dream and you imagine through your mind, you imagine many things that give you a picture of tomorrow that you wish to have. This is the dream of every child as well as young people, this exists in all angles of human life, Education, work / employment / owning a large business that affects the economic area with positive results, having faith in the sense of believing in God and living his philosophies in the sense of praying to him as well as doing good worship the last area is relationships, where in this area everyone wishes to find the right wife/husband even if he does not have those qualities, but at the end of the day in this area everyone wants something better.

Thursday, August 31, 2023

incentives.

• Sixth, all employees must have a path to give feedback on the success of the process.

• Seventh, all employees must actively participate in the procedure.

• Eighth, the change may involve strategically-planned corporate “interventions” such as mergers.

Organizational Leaders

Many business experts believe that this type of leadership should come from the human resources department. An article in Forbes Magazine says the most important factor in organizational change is managing human capital. The article author says that human resource departments should focus more on being “strategic business partners” and less on implementing HR policies. The article goes on to say that the most important components of the development are identifying options for change that are available to the corporation and then to look at employees in terms of management talent and how to recruit, train and keep that talent.

HR also should be responsible for creating a motivational program that would permeate the entire organization. Obviously, the kind of assessment and change discussed here necessitates the leadership of people who understand human and organizational behavior and other components of the challenge of organizational change. Universities offer degree programs for professionals that include undergraduate and graduate degrees as well as doctoral degrees and certifications. Certificates can generally be earned in less than a year and can supplement other business degrees. Students take courses in areas like communications, conflict resolution, staff development, and human resource management.

ELIMU YA PADRE WA KANISA KATOLIKI

(Sehemu ya Tatu)

Na. John-Baptist Ngatunga
___________________________

Sifa za Kipee za Viongozi wa Kanisa Katoliki:

1. Baadhi ya Sifa hizo ni kwamba, Viongozi hawa kwa kawaida huwa hawahangaiki na Vioja; wanahangaika na Hoja. Ukija na Hoja watakujibu kwa Hoja; ukija na Vioja wala hawakuhoji. Wanajibu Hoja kwa Hoja sio Hoja kwa Vioja.

2. Mfumo wao wa kutatua changamoto daima huwa ni Majadiliano zaidi kuliko Mabishano. Hawawezi na hawapendi kubishana, ila wanapenda kujadiliana. Hii ni kwasababu wanajua kuwa kubishana ni kutaka kujua nani yuko sahihi ila kujadiliana ni kutaka kujua nini kipo sahihi. 

3. Wanapenda kucheza na Masuala (Issues) sio watu. Wanajadili Masuala hawajadili sana Matukio au watu. Ndio maana hata linapotokea jambo la Kitaifa kama hili suala la Mkataba wa Bandari kati Tanzania na DP World waliongelea suala lenyewe yaani MKATABA na wakajikita katika Hoja hiyo. Hawajamlenga Mtu au Watu. Wamezungumzia Mkataba (Issue) sio Watu na Dini zao au Makabila yao.

4. Hawana desturi ya kukurupuka katika Maamuzi yenye maslahi mapana kwa Jamii. Wanajipa muda wa kutosha kulitafakari jambo, kusali na kuliombea Taifa au Jamii, kufanya Tafiti juu ya jambo kabla ya kutoka hadharani na matakamko. Ndio maana wakitoa WARAKA au TAMKO unakuwa Mjadala wa Kitaifa. Na ndiyo desturi ya Wanafalsafa (They don't rush to conclusion without premisses).

Tofauti na baadhi ya Taasis ambazo hukurupuka tu kama chafya na kutoa matamko bila kufanya Tafiti. Wakati mwingine badala ya kujikita katika NINI, wao wanajikita katika NANI. Badala ya kujibu Hoja kwa Hoja wenyewe wanawashambulia watoa Hoja. But it's not to the Catholic Church.

5. Kwa kuzingatia historia ya Maisha yao ya Kitaaluma, usomi, akili, upeo na uelewa mkubwa walio nao;  itoshe tu kusema kuwa Kanisa Katoliki ni moja ya Taasisi zinazoongozwa na Viongozi wenye Matumizi mazuri sana Akili. Na kwamba 'Intelijensia' ya Kanisa Katoliki huwa haibabaishi, haibahatishi, haikisii, haikurupuki, haionei, haidanganyi. Ipo objective na inatenda haki.

6. Na kutokana na hilo sitakuwa nimekosea nikisema, "The Catholic Church is the Big Brain Institution; Full of Competent, Confident and Confidential Intellectuals led by the Power of the Holy Spirit to lead God's people bodily and Spiritually" (Kanisa Katoliki ni Taasisi yenye Akili kubwa; iliyojaa Wasomi Mahiri, wanaojiamini na wasiri wanaoongozwa na Nguvu ya Roho Mtakatifu kuwaongoza watu wa Mungu Kimwili na Kiroho).

7. Viongozi hawa ni Watu wenye Moyo wa kusaidia sana Jamii kwa kutoa Huduma mbalimbali za Kijamii ili kuiinua Jamii kutoka Lindi na Tupe la Umasikini. Angalia Huduma za Kijamii zitolewazo na Kanisa: Elimu, Afya, Maji, Nishati ya Umeme, Ajira, na nyingine nyingi.

8. Hawa Viongozi wakiliamua jambo lao, ni lazima tu litafanikiwa kutokana na umakini, umahiri, uchapakazi, kujitoa, uadilifu, Imani. Angalia Jinsi Taasis za Elimu na Afya wanazozianzisha, kuzisimamia na kuziendeleza zinavyofanya vizuri: Angalia Vyuo Vikuu kama:
(i) St. Augustine University of Tanzania (SAUT) 
Pamoja na Vyuo vyake Vishiriki vyote

(ii) Ruaha Catholic University (RUCU)

(iii) Catholic University of Health and Aliened Sciences (CUHAS -BUGANDO)

(iv) Mwenge Catholic University (MWECAU) 

Sijavitaja Vyuo vya Kati, Seminari Ndogo na Shule za Sekondari ambazo zinafanya vizuri sana Kitaifa na Shule za  Msingi.

Angalia pia Hospitali mbalimbali:
(i) Hospitali ya Rufaa Bugando (Mwanza)
(ii) Hospitali ya Peramiho (Ruvuma)
(iii) Hospitali ya Ndanda (Mtwara)
(iv) Hospitali ya Ifakara (Morogoro)
(v) Hospitali ya Lugarawa (Njombe)

Zijavitaja Vituo vya Afya na Zahanati.

Na kwa hapa Tanzania ukiiondoa Serikali katika suala la utoaji wa Huduma za Jamii, Taasis inayofuata ni Taasis inayoongozwa na Viongozi hawa: Maaskofu, Mapadre, Watawa (Mabrother na Masista) yaani Kanisa Katoliki. Na usipolitaja Kanisa Katoliki kwa hilo utakuwa aidha haujui au unachuki binafsi.

9. Viongozi wa Kanisa Katoliki wanaupenda UKWELI. Na Mtumishi wa Mungu Father John Hardon, SJ aliwahi kusema, "Our Duty as Catholics is to know the Truth; to live the Truth; yo defend the Truth; to share the Truth with others; to suffer for the Truth" (Kazi yetu kama Wakatoliki ni kuujua Ukweli; kuuishi Ukweli; kuulinda Ukweli; kuutetea Ukweli; kuwashirikisha wengine Ukweli; kuteseka kwaajili ya Ukweli).

Na kimsingi huyo UKWELI ni YESU KRISTO. "Yesu akawaambia, 'Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba; ila kwa njia ya Mimi'" (Yohane 14:6)

10. Kutokana na ukweli huo, Viongozi hao wa Kanisa Katoliki huheshimiwa sana na Waamini wao. Na hapa nikuambie tu ukweli kwamba kwa Muamini Mkatoliki, anawaheshimu Viongozi hawa pengine kuliko Kiongozi wa aina yoyote ile unayoijua wewe.

Na linapotokea jambo lenye ukinzani kati ya Viongozi wao na Mtu au kundi fulani la watu, ni rahisi sana kwa Mkatoliki kuufuata upande wa Viongozi wao. Ukitaka kuamini hiki ninachokuambia, fuatilia suala zima la TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA (TEC)  KUHUSU MKATABA WA BANDARI.

Sio kwamba Waamini hawa Wakatoliki wanafuata tu mkumbo la hasha. Hii ni kwasababu wanawajua vizuri sana Viongozi wao kuwa wako serious (makini) sana na mambo yao. Ni Viongozi ambao wanaongea wanachokimaanisha na wanakimaanisha wanachokiongea.

Sio kama walivyo baadhi ya Viongozi wengi wanaoleta Propaganda za kishamba na Siasa za kitoto ambazo zina athari kwa Jamii wanayoiongoza halafu wenyewe hawajali, wabinafsi na wanaoyajali matumbo yao tu bila kuwa na jicho la huruma kwa raia wengi wanaotaabika kwenye wimbi la ufukara ulipitiliza.

Viongozi ambao wakati mwingine unaweza ukadhani labda Akili zao zina makengeza. Wanatamani kukiona hiki ila macho hayana ushirikiano na mshikamano na uso wao. Ni Viongozi ambao wanajua Ukweli lakini hawako tayari kukusema ukweli au wanaogopa kumshauri Boss wao kisa tu Boss ameshaonesha mwelekeo fulani wanaoujua kwahiyo wanaogopa kumshauri tofauti na ukweli kwa kuogopa kuvipoteza Vyeo vyao.
Very hopeless Leaders!!

11. Viongozi wa Kanisa Katoliki wana BUSARA. Na ninaposema Busara namaanisha, "Matumizi sahihi ya Maarifa". Ni wasomi walioelimika. Yaani ni wasomi wanaojua kuitumia Elimu yao kwa manufaa yao na manufaa ya Jamii inayowazunguka. 

Unajua, hapa Tanzania tuna Wasomi wengi sana na tuna Viongozi wengi sana Wasomi ambao hawajafanikiwa kuelimika. Waliosoma ni wengi ila walioelimika wako wachache sana. Wengi wamesoma ila wachache wameelimika. 

Ndio maana tuna baadhi ya Viongozi ambao jinsi wanavyotumia Elimu na Akili zao katika baadhi ya Maamuzi huwezi kuamini kama kweli walifundishwa na Walimu wenye Vyeti halali au ni wale wa Vyeti Feki. Ukiwasikiliza jinsi wanavyotengeneza Logic zao katika maongezi unaweza ukadhani labda ni watoto wanaojifunza kuongea.

12. Viongozi wa Kanisa Katoliki ni mfano halisi wa MCHUNGAJI MWEMA ambaye Yesu Kristo Mwenyewe kwa kinywa chake alimsema, "Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema hutoa nafsi yake kwa ajili ya kondoo...... Mimi ndimi mchungaji mwema, nawajua walio wangu, nao walio wangu wanijua Mimi" (Yohane 10:11,14)

Mchungaji Mwema ana sifa kuu Tatu:
1. Mwema
2. Huitoa nafsi yake kwaajili ya kondoo wake
3. Huwajua kondoa wake nao walio wake wanamjua

Hawa Viongozi ni WEMA kwa kuwa wana NIA NJEMA na Wakatoliki na hata wale wasiokuwa Wakatoliki yaani ambao hawamo katika 'Zizi' la Ukatoliki (Yohane 10:16). Maana yake Mapadre na Maaskofu wetu ni WEMA kwa Watanzania wote. 

Viongozi hawa WANAZITOA NAFSI ZAO kwaajili ya Taifa la Mungu. Ndio maana wanapambana kuzitetea Rasilimali za Taifa hili kwa manufaa ya Watanzania wote japo wasiojua wanawatukana badala ya kuzijibu Hoja zao kwa Hoja.

Wanawajua Waamini wao wanataka nini na Waamini wao nao wanawajua Viongozi wao na wanawaheshimu. Ndio maana nilisema kwa Mkatoliki kindakindaki, huwezi kumwambia chochote kinyume na Wachungaji wao akakuelewa. Hii ni kwasababu Maaskofu na Mapadre wanajuana na Waamini wao.

Hapa nimejaribu kugusia tu kwa uchache kuhusu namna Padre wa Kanisa Katoliki anavyopitia Maisha ya Kimalezi ya Kiroho, Kielimu na Kijamii kwa wale wenye Wito wa Upadre. Lakini kama ulikuwa umenifuatilia toka mwanzo nimeelezea kuhusu upatikanaji wa Viongozi hawa na Elimu zao. Sasa kazi ni kwako kupima kati ya Elimu ya Viongozi wa Kanisa Katoliki na Elimu ya hao Viongozi wanaokuongoza Kidini au Kisiasa nani wanatumia vizuri Elimu  na Maarifa yao?

Niishie hapa!!