Friday, May 3, 2024

faida za kumjua Mungu kwa viwango na kumtafuta kwa bidii

Bwana Yesu asifiwe


            Mpendwa katika bwana karibu tujifunze faida za kumjua MUNGU nakumtumikia kwa viwango kwakuwa neno la MUNGU linasema mtu akimtumikia MUNGU atamuheshimu ona niaraha iliyoje kwa mwanadamu kuheshimiwa na MUNGU tuntumikie MUNGU kwa viwango na kwa uaminifu na tutauona ukuu wake

FAIDA ZA KUMTUMIKIA MUNGU
1.utatimiziwa mahitaji yako yote hata bila koumba
       Yesu aliwafundisha wanafunzi wake pamoja na wote waliokuwa wamekusanyika [makutano],aliwaambia kuhusu kumtumiakia na kuutafuta kwanza na kuyafanya mapenzi ya Mungu na kumtafuta kwa bidii na haki ya mbinguni na mengine yote Mungu wa mbinguni atawapa
MATHAYO 6;33 [bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake,na hayo yote mtazidishiwa]
basi Mngu anajua yakwamba sisi ni wanadamu na tunahitaji mambo mengi hata kama tumeakoka bado tunahitjia nambo ya kawaida kama mavazi,chakula na malazi kwahiyo ni haki yetu kupata hayo kutoka kwa MUNGU wetu ila kwanza tumtafute MUNGU kwa bidii na kwa uaminifu

2.kupata kibali kwa MUNGU na wanadamu
        Unapomtumikia Mungu kwa uaminifu na kuitatuta haki yake  utapata kibali mbele za Mungu na wanadamu pia kutokana Mungu kutenda matendo ya ajabu kupitia wewe na Mungu wa mbinguni atakuheshimu WARUMI 14;18 [kwakuwa yeye amtumikiaye kristo kakika mambo hayo humpendeza Mungu,tena hukubaliwa na wanadamu] kwa hiyo tunaona jinsi tukimtumikia kristo ya kuwa tunapata kibali mbele za wanadamu kwa hiyo mpendwa umeona jinsi ambavyo ilivyofaida kutumikia Mungu lakini pia utapata mambo mengi kwasababu Mungu anajua ya kuwa unahitaji yote hayo. Basi ndugu zangu tumtumikie Mungu bila ya kuogopa wala kuhofu chochote maana Mungu yuko upande wetu kila siku

3.kupata baraka nyingi zaidi
            Mungu anapomuona mwanadamu anamtumikia na kushinda majaribu yote anayopitishwa na kumtolea sadaka Mungu kwa uaminifu Mungu anaahidi baraka nyingi juu yetu tunamkumbuka baba yetu ibrahimu alivyomtumikia Mungu kwa uaminifu na hata kuvumiliana na hali yake ya kukosa mtoto kwa miaka mingi sana na Mungu alivyouona uvumilivu wake akaamua kumuahidi mtoto Mungu akamwambia sara mwaka ujao katika majira kama haya Bwana atakufanyia kicheko na kweli Mungu akatimiza ahadi yake sara akapata mimba na kushangaza dinia kwa mzee kumzaa mtoto isaka lakina baada ya kuzaliwa isaka Mungu aliamua kuipima imani ya ibrahimu kwa kumwambia amtoe isaka baada ya ibrahimu kutii Mungu alimuapia baraka zaidi

4.ulinzi wa mji na mali za mtu[nyumba]
         Mungu hawezi kumuacha mtoto wake apate shida na aonewe na shetani kwa hiyo kwa uwezo wetu wanadamu hatuwezi kufanya neno lolote katika kujilinda wenyewe bila msaada wa Mungu. hapa tunajifunza kumtegemea Mungu kwa kila jambo hata kama utapata shida na matatizo mengi ujue ya kwamba hatuna msaada mwingine zaidi ya Mungu wa mbinguni , hapa duniani tunapata shida lakini tujipe moyo tutaushinda ulimwengu ZABURI 127;1 [BWANA asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure BWANA asipoulinda mji yeye aulindae akesha bure   kwahiyo tunapaswa kumshirikisha MUNGU katika kila jambo na mali zetu tulizonazo.

   HITIMISHO
zipo faida nyingi zitokanazo na kumtumikia Mungu hizo ni chache tu . Basi tuwe na matumaini katika mambo yote kwamba Mungu anakwenda kutenda hata kama utaona yakwamba tatizo ulilokuwa nalo linapita akili zako we muachie Mungu yeye amesema akili zetu zinapofika mwisho ndipo yeye anapoanzia lakini pia mtunzi wa zaburi amesema tusizitegemee akili zetu wenyewe Mungu wa mbinguni akubariki.


                                            

No comments:

Post a Comment