Sunday, September 24, 2023

IFANYE NDOTO HALISI YA MTOTO UNAEMLEA IWE KWELI L

Ndoto za watoto wengi wa Afrika zimeshindwa kuwa kweli kwa sababu ya watu waliopewa nafasi yakuwasimamia vijana na watoto wa Kiafrika, pengine ni mzazi, mlezi hata viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali, Mashirika binafsi ambayo yamekuwa yakifadhiliwa na mashirika ya ndani na mashirika ya nje kwa lengo la kuhakikisha watoto wanapata nafasi yakuishi ndoto na malengo yao.

● Wazazi/walezi kwa asilimia kubwa wamekuwa chanzo cha mauaji ya mtu aliyekusudiwa na Mungu kwa sababu ya nafasi zao kwa watoto na vijana wanaowalea. Ni jambo la kawaida kwa mzazi/Mlezi kutaka mtoto wake kuishi matakwa yake ambayo mara nyingi huwa ni yakutafuta hadhi na heshima kwa marafiki na jamii inayomzunguka. Hivyo kwa matakwa hayo basi analazimika kumtengeneza mtu asiye halisi kwa nafasi yake yeye kama mzazi au mlezi.

● Ni jambo la kawaida mtoto kuonekana hana akili darasani anapochagua kufanya masomo ya sanaa kwa sababu jamii yetu inaamini mtoto anapofanya masomo ya sayansi huyo anauwezo mkubwa wa kiufahamu ukilinganisha na wale ambao wanafanya masomo ya sanaa wanapokuwa shuleni, vilevile ni jambo la kawaida kwa mtoto/kijana kuwekwa kwenye kundi la watu wa hovyo, wasio na akili pale tu anapokuwa na matokeo yasioridhisha anapokuwa shuleni.

●Andiko langu halijajikita kwenye kufanya promosheni ya watoto kutokuwekewa mazingira ya usaidizi kwenye misingi ya kuonyeshwa njia bora za malezi hapana, andiko langu lina lengo lakukuonyesha wewe mzazi/Mlezi na wewe kiongozi wa taasisi za serikali/mashirika binafsi  unanafasi ya kumwonyesha njia bora mtoto wako kwenye ule wito mkuu alioitiwa na Mungu duniani. Pengine kwa macho ya hadhi wito wake haukuvutii lakini ndiyo eneo lake bora kuliko  maeneo ambayo wewe unaona kwa macho ya fikra zako ndiyo eneo sahihi la mtoto wako kufuata.

● Tumeua vipaji na karama za watoto wetu kwa sababu tumeacha wajibu wakufuata misingi bora ya malezi ambayo yanafanya promosheni ya kile ambacho mtoto amekibeba ndani yake ambao ndiyo uwezo halisi wa mtoto wako. Ni rahisi zaidi mzazi/mlezi kumzuia mtoto asipractice kipaji chake cha kucheza mpira, kuimba na mambo mengine ya vipaji kwa sababu yeye (Baba/mama/Mlezi) alitaka kuwa daktari na akashindwa basi anataka mtoto wake awe daktari ili kutimiza matakwa na ndoto yake kupitia mtoto wake.

●Ukweli ni kwamba ulichopewa wewe na Mungu sicho alichopewa mtoto wako kukifanya hapa duniani, hapa duniani kila mtu ana kusudi lake, wito wake na amepewa vifaa saidizi kulingana na kile ambacho Mungu alikikusudia kitokee kupitia yeye huyo mtoto wako, nje na hapo unalazimisha samaki kupanda mti na simba kuwa fundi wakuogelea.

● Ni kweli mtu anaweza kulazimishwa na mazingira kufanya kile ambacho sio kusudi lake na akafanya vizuri mfano mtoto anaweza kulazimishwa kusoma aina fulani ya professional, anaweza kufanya vizuri sana hata kuwa miongoni mwa watu bora katika hiyo kada lakini kila jambo tunalofanya duniani ambalo ni kusudi halisi la Mungu basi ndani yake huwa na passion nje yakuwa ni jukumu ambalo linapaswa kutekelezwa.
● Mfano nikiwa na passion yakuwa kiongozi, jambo la kwanza halitakuwa maslahi yangu binafsi nitatamani kuona nafasi yangu kama kiongozi inakuwa na matokeo chanya kwa wale ninaowaongoza kwanza kabla yangu, naweza kupitia maumivu makali sana, kwa mimi ni kiongozi basi nitakubali kupitia dhoruba na changamoto zote kwa ajili ya wengi. Nachukua mfano wa Yesu kristo mwana wa Mungu, the Role model of all Role modes duniani, yeye alikubali kuwa sadaka ili kuonyesha njia kwa sisi ambao ni wafuasi wake, si kwa kulazimishwa ila ni kwa sababu alikuwa mfano bora kwetu.

●Mtu akiwa anafanya kazi ambayo ni kusudi lake, kinachotangulia kwanza ni passion, kabla ya maslahi binafsi, uzuri wakufanya kitu ambacho ni kusudi lako, hata kama ili uweze kufikia ile pick, kiwango cha juu cha ubora kuna maumivu atayapitia lakini kwa sababu tu kuna ile nguvu ya asili ndiyo inayompa hamasa, bado imani na tumaini lakuifikia kile anakiona ataendelea kupush kwa nguvu, maarifa, uvumilivu, ubunifu na hata kama kuna gharama za ziada zitahitajika basi atatafuta namna ya kuhakikisha anagharamikia ili tu apate kile anachohitaji.

●Mfano nimehudhuria mafunzo ya huduma ya mtoto ambayo yamekuwa yakiandaliwa na shirika la compassion International Tanzania, nimekuwa nikijifunza jambo anaposimama Mkufunzi Ndugu Letema Laizer, namna ambavyo ule uhusika anavyouvaa na kile kitu bora anachokitoa kwa wanafunzi wake, lakini unaona ile passion aliyonayo katika kufanya kazi ya ukufunzi. Wakati mwingine kuna baadhi ya technical issues zinakuwa zinajitokeza wakati wa mafunzo lakini, he will always find ways to solve the problems whether in the night wakati nyie mmelala atafanya so unaona tu kuwa kando ya kuwa ni kazi yake lakini anaenjoy kuifanya na katika kuenjoy huko basi kuna toa kitu ambacho huleta picha halisi ya huduma ya mtoto kwa watendakazi nakuiona ile huduma ikiingia ndani ya watenda kazi kama sindano inayoingia na kutoa simu ambazo wanakuwa nazo wanapokuwa wametoka kwenye vituo vyao vya kazi kutokana na baadhi yao kupitia changamoto kadhaa zenye kuvunja moyo na kuondoa nuru ya huduma ya mtoto ndani yao.
●Mtu mwingine ambae ananisimamia mimi katika utekelezaji wa majukumu yangu, mzee wangu Raphael Lyela (Balozi) zile article zake haziji tu kwa sababu anajua ila ni kwa sababu ni kitu ambacho he was born to do, whether iwe kwa payless kwa maana ya fedha. Yeye anapoona ujumbe umewafikia vijana na kuona matokeo ya kazi yake ikibadilisha mentality ya vijana basi that is an enjoyment for him. Kuna matokeo makubwa sana kupitia program za vijana anazofanya kupitia whatsap groups, lakini zile Camps za Youthkingdom Ministry, amazing sana. Hapa sio pesa bali ule wito mkuu ndani yake ndiyo unaweza kuleta matokeo ambayo mwanzo haikuwa priority kwake.

●Ninachojifunza zaidi sasa ninapoelekea kuwa baba na nikiwa mlezi wa vijana kituoni, naona wajibu wangu mkuu ni  kuhakikisha nasimamia ndoto za vijana na kusimamia zichupue na kustawi kwa misingi ya malezi bora kwa vijana. Kuifanya ndoto ya mtu kuwa kweli sio jambo la kulala na kuamka tu ni kama ambavyo tunaweza kuandaa shamba, kulima, kupalilia, kumwagilia, hapo katikati kuna kamchakato fulani ambacho kinahitaji uvumilivu ili kupata matokeo tarajiwa.
●Changamoto tunayopitia walezi wengi, tunaishi kukariri mfumo fulani wa maisha, kutaka ile public popularity, sifa fulani mwanangu anasomea udaktar, anasomea uhandisi nk. Mambo hayo ni mazuri lakini kama yanapita kwenye njia au mfereji ambao sio wake hata utendaji wake kesho unaweza usiwe bora kama ambae ukiacha kuwa ni taaluma yake, na ni kazi inayomwingizia kipato basi huwa ni huduma kwa upande mwingine na hao ndiyo wako kujitolea kufanya jambo lolote akiamini kuwa kwa sababu jambo hilo liko ndani ya uwezo wake basi wataona alichonacho na hicho ndiyo kitamtambulisha na kumpa nafasi ya kutengeneza uhitaji kwa jamii/taasisi kupitia yeye. Mtu anaanza kwa kujitolea akiamini anahitaji jukwaa, (Platform kuonyesha kile alichonacho) akipata hiyo fursa basi mengine hubaki kuwa ni historia, i take some examples of Secular muscians hapa Tanzania, Harmonize alipata dakika tano mbele ya Diamond pale Dar live, Mbagala Zakiem na ikawa nitolee na aliamini anaweza, nani leo hamfahamu Harmonize hata kama sio mfuasi wa hizo kazi zake lakini umewahi kumsikia au kusikia nyimbo zake hata kwenye vyombo vya usafiri. Naturality is more power compare to Artificiality.

●Kwa hiyo Malezi bora sio kuwalazimisha watoto/Vijana kutembea kwenye mawazo na matamanio yako wewe kama mzazi/Mlezi/kiongozi wa taasisi lakini malezi bora ni kuonyesha njia penye lile kusudi la Mungu ndani ya mtoto au kijana unae mlea na kumsimamia wewe.

●Do not use your position as a parent/guardian or a leader to kill the dream of a child or young person. If you don't know something, look for solutions and more knowledge on how to nurture your child's potential.


Mimi ni kijana wa Balozi Raphael Lyela.
0755632376
0719110760
www.mgemamoses.blogspot.com

Monday, September 4, 2023

The story of life begins as, you live a dream and you imagine through your mind, you imagine many things that give you a picture of tomorrow that you wish to have. This is the dream of every child as well as young people, this exists in all angles of human life, Education, work / employment / owning a large business that affects the economic area with positive results, having faith in the sense of believing in God and living his philosophies in the sense of praying to him as well as doing good worship the last area is relationships, where in this area everyone wishes to find the right wife/husband even if he does not have those qualities, but at the end of the day in this area everyone wants something better.