Sunday, July 30, 2023

Unyenyekevh, Usikivu,  Utulivu hutoa nafasi yakujifunza mara kwa mara kutoka kwa kila Rika, mazingira yote, kwa wenye elimu na wasio na elimu, kwa wazoefu na wasio na uzoefu, kwa wanaojua na wasio jua, hilo litakuwa jicho lako la tatu kukusaidia kuona kile ambacho kwa macho yako hayo mawili huwezi kukiona. Watu wengi tumepoteza uwezo wakuona kwa sababu tunaamini tunajua kila kitu kwa sababu ya nafasi tulizo nazo, Utajiri, uongozi ambao unatupa nafasi ya kufanya maamzi. 
kumbuka rafika hata Dr Philip Isdor Mpango amewahi kuwa chini ya PM Kasimu Majaliwa, lakini leo imekuwa kinyume chake, unyonge wa mtu leo haimanishi hawezi kuwa mnyonge, kiongozi wa leo anaweza kuongozwa kesho, na anaeongozwa leo anaweza kuwa kiongozi kesho.
Binadamu ni mbegu halisi ya Mungu hakuna mwanadamu anaweza kuiua mbegu hiyo, inaweza kupitia misukosuko tu lakini haiwezi kufa...
Waulize waliomsulubisha Yesu, habari zake wanazo

Najifunza kunyenyekea zaidi.