Sunday, January 1, 2023

HERI YA MWAKA MPYA RAFIKI YANGU

Heri ya mwaka mpya rafiki yangu, ndugu na jamaa yangu wa karibu. Ni siku 366 zimekatika tangu mwaka ulipoanza 2022, ndani ya siku hizi yapo mengi ambayo yametokea, mazuri, magumu yenye kuumiza, kufurahisha lakini yote kwa yote Mungu ni mwema kwa sababu hata katika nyakati zote Mungu bado anabaki kuwa nguzo na dereva wa maisha yetu hivyo tumshukuru Mungu kwa hali zote...

▪︎Mwaka ni zawadi kubwa sana ambayo Mungu humpa mwanadamu kwa lengo moja tu kuyakamilisha yale ambayo alikupangia kuyafanya hapa duniani, hivyo basi ukiona bado unapata nafasi ya kuingia mwaka mpya fahamu kuwa kuna jambo unapaswa kulifanya hapa duniani kwa ajili yako, familia, Taifa na jamii inayokuzunguka na ukamilifu wa hayo yote ni ukamilifu wa kusudi la Mungu ndani yako....
▪︎Hivyo mshukuru sana Mungu kwa neema hii kubwa lakini pia fahamu kubwa bado unadeni kubwa duniani ndiyo maana bado unaishi, pengine unaweza kujiuliza ni mara ngapi umesafiri lakini hata harufu ya ajali hukupata ni mara ngapi umeugua lakini ukapona,
▪︎ je ni mara ngapi umekosea lakini bado upo huru ?. Katika hayo yote kuna watu walisafiri lakini walirudi wakiwa kwenye masanduku, wapo waliougua hawakupona kabisa lakini wapo waliofanya kosa dogo lakini wapo gerezani au hata kuondolewa kazini au kupata adhabu kubwa ambayo imewaumiza sana.....

▪︎Cha msingi ni kutambua kuwa Mungu anapokuepusha na majanga au changamoto yeyote ile bado anakusudi na wewe hapa chini ya jua na mbingu.
▪︎ Fahamu kuwa una kusudi maalumu ambalo unapaswa kulitimiza kwa nguvu zote na Mungu atakusaidia sana...
▪︎Mwaka unapoanza ni vyema sana kupanga mipango na malengo yako kwa kuzingatia uwezo wa utekelezaji wake, hapa angalia je malengo haya ninayo panga ndani ya mwaka huu nitaweza kuyatimiza au nitajipa mzigo ambao siwezi kuufikisha hata robo ya malengo yenyewe.....
▪︎Kuweka mipango na malengo ni jambo rahisi sana lakini changamoto kubwa sana ni namna ya utekelezaji wa malengo na mipango hiyo. Unapozungumzia malengo au mipango ili itimie inahitaji sana viwezeshi ndiyo uone matokeo ya malengo hayo..
Mfano....
▪︎Ukipanga kujenga nyumba basi unahitaji kitu cha kwanza kabisa ni kuwa na fedha ambayo itaweza kusaidia wewe kuanza hatua ya pili baada ya kupanga malengo yako, kuamua pekee halitosis kama huna fedha za kulifanya lengo hilo kufanyika...
▪︎Malengo mengine hayahitaji fedha ila yanahitaji uelewa, utayari wa kutoka ndani mwako sio kwa sababu kuna mtu alikusukuma kuanza jambo hilo, kwa kufanya hivyo ni rahisi sana kutenda kwa ukamilifu na kwa kujitoa zaidi maana utafahamu nini ambacho unakifanya kwa sababu utakuwa umefanya utafiti wa kutosha na umejiridhisha kuwa jambo hili naweza kulibeba na kulifikisha kwa wakati na kwa ufanisi na ubora....
▪︎Mwanzo wa mwaka mara zote kila mtu huwa na hamasa, shauku na nguvu ya kupanga malengo na pengine kuanza kwa nguvu mno lakini baada ya miezi mitatu tu watu wengi huachana na malengo na mipango yao na kushika njia zingine kabisa ambazo hata hazikuwa kwenye mipango wala mlengo ya mwaka kabisa....

Hii inachangiwa sana na mambo kadhaa ambayo yamekuwa na athali hasi kwa watu wengi....

1. KUKOPI MIPANGO NA MALENGO.
▪︎Watu wengi hawana malengo ila wengi tunakopi mipango na malengo kutoka kwa watu wengine, umemsikia rafiki yako, mhamasishaji Fulani, umesoma kitabu Fulani ukaona malengo Fulani basi unapita nayo kama mwewe kaona kifaranga.
▪︎Malengo haya hayawezi kutimia kwa sababu hujui kwa kina juu ya malengo na mipango hiyo hivyo kama njia uiendayo hujui basi ni rahisi zaidi kupotea na kutokifika mahali unapokwenda maana pia hujui hata uendako....

2. KUHAMASIKA NA MWAKA MPYA...
▪︎Mwaka ni mabadiliko ya majira ambayo hubadilika kila baada ya miezi 12 lakini uhalisia wa maisha unabaki kuwa ni uleule tu kwamba maisha yanaendelea, mwaka mpya unapoanza wengi huhamasika sna kwamba nilikosea mwaka uliopita sasa naanza mwaka mpya ngoja nianze upya lakini wakati mwingine tunapoteza malengo endelevu kwa kigezo cha mwaka mpya hivyo kupoteza focus, hatupaswi kupanga mipango na malengo kwa hamasa ya mwaka mpya bali tupange malengo na mipango ya mwaka kwa nguvu ya kiuchumi, uwezo binafsi wa kibailojia na mazingirq ambayo unaishi.....

3. MIPANGO NA MALENGO YA KUWAFURAHISHA MARAFIKI ZETU...

▪︎Watu wanaweka malengo kwa lengo la kuwafurahisha ndugu, jamaa na marafiki, tusionekane watu tusio na malengo, hivyo mtu anaweka malengo ili akiulizwa na marafiki zake awe na neno la kusema nao ili asionekane ni mtu asiye na mipango wa dira ya mwaka.
NB....

Zipo sababu zingine nyingi ambazo zinapelekea kufeli kwa mipango na malengo ya watu wengi baada ya miezi mitatu au miezi sita tabgu mwaka kuanza.
▪︎Ushauri wangu kwa mwaka huu basi ni vyema sana kujitambua binafsi, kutambua uwezo wako wa kifedha, akili, nguvu ya utendaji na maarifa ya utekelezaji wa kila malengo unayopanga kila mwanzo wa mwaka.
▪︎Kuwa na malengo mazuri bila utekelezaji ndugu zangu ni kuichosha akili na nafsi bila sababu za msingi. Fanya malengo na mipango kwa urefu wa kamba yako, hakuna malengo bora kuliko malengo yako, ubora wa malengo ni matokeo ya mipango na malengo yako mwenyewe....
▪︎Usipange malengo kwa kufurahisha umma, panga malengo kwa kuzingatia uwezo, nguvu, eneo ulilopo, ujuzi maarifa na nafasi ya utekelezaji wa malengo hayo....

▪︎Kuna wakati unaweza kuwa na nguvu ya kifedha, mazingira lakini ukakosa muda wa kufuatilia malengo yako kwa sababu muda wako unaamuliwa na wajiri wako, hivyo set malengo na mipango kwa kuzingatia sana factors zote kwa maana ya Internal and external factors......
Panga malengo kwa kuzingatia sababu nyingi ambazo zinaleta ukamilifu wa kile unachotaka kukifanya kila mwaka....
▪︎Sio kila mwaka uweke malengo kuna mwaka unapaswa kukamilisha malengo yaliyosalia ya mwaka unaopinduka na hapo utajiona bora na mwenye manufaa hapa duniani....
Kumbuka...
Hakuna Malengo bora yasiyokuwa na matokeo chanya....
Heri ya mwaka mpya
Musa Zephania Mgema 
0755632375