Sunday, April 17, 2022

Nimezaliwa na kukulia kwenye miaka amabayo, kipindi cha maadhimisho ya sikuu mbalimbali ulikuwa unchukuliwa katika hali ya siku maalumu sana. Mfano ni katika sikukuu za kiserikali alimaarufu kama (public holiday), sikukuu hizo zilikuwa zikitengeneza hisia na hali ya tofauti na siku zingine, mfano siku ya tarehe 9, disemba hali ya nchi kwenye siku hiyo ilionyesha kuwa kweli tunakumbuka siku muhimu na maalumu sana kwa Taifa letu, kumbukizi nyingi za matukio ya wakati wa mapambano ya uhuru, hutupa zenye kujenga, kuhamasisha, kuonyesha thamani ya Tanganyika kuwa nchi huru, kwa nini mtanganyika apate uhuru, ilikuwa ni siku maalumu sana ambayo ilijenga umoja, mashikamano na upendo wa that, usingemkuta mtu hata anajihusisha na kazi au majukumu mengine makubwa bali kila mtu alifurahia ukombozi wa Taifa letu miaka mingi nyuma.

Nazikumbuka sikukuu za nane nane, saba saba, Nyerere day, sikukuu ya mapinduzi matukufu ya zanzibar, sikukuu ya muungano, sikukuu ya wafanya kazi na nyingine. Sikukuu hizi zilikuwa na nguvu na zilitengeneza hisia na tafakari kuu kwenye mioyo ya watu kutokana na namna wahusika walivyoziandaa na kuwatazamisha wananchi katika thamani ya sikukuu hizo, ndiyo maana unaona kila mtanzania aliona thamani ya siku hizo hivyo kupelekea kusherekea sikukuu hizo kwa kumaanisha sana.

Vilevile sikukuu ya Christmas na pasaka, zilikuwa ni sikukuu zenye nguvu kuanzia kwenye maandalizi ya familia zetu, nchi, dunia mpaka kanisani, maandalizi yalikuwa ni ya kiwango cha juu sana mpaka yalikuwa yanarejesha sana ile hali ya mazingira ya kuzaliwa kwa Yesu na hata ile hali ya mateso ambayo Yesu aliyapata kwenye kipindi cha mateso yake.