Thursday, September 23, 2021

UJASIRI NDANI YA YESU

Bwana Yesu asifiwe!

Waebrania 10:35 anasema,,"Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu"

Ukisoma mstari huu ndani yake kuna kitu cha thamani na cha ajabu sana kinaitwa "UJASIRI" na huo ujasiri unaweza ukautunza au ukautupa ,"MSIUTUPE" maana yake unaweza kuwa nao na ukautupa.
Ndani ya "UJASIRI" kumebebwa kitu kinaitwa "THAWABU " 
Ukisoma katika kiingereza anasema hivi,,,,"Therefore do not throw away your confidence, which has a great reward."
Kiswahili anasema hivi,," Kwa hiyo, msipoteze ujasiri wenu, maana utawapatia thawabu kubwa" Sasa ukiunganisha na neno la 
Efeso 6:10 anasema "Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake" Utaona neno hili "HODARI" limetumika katika Waebrania 10:35 kama "UJASIRI" ambao ndani yake tunapewa "Thawabu KUBWA".

NINI MAANA YA UJASIRI/UHODARI.
UJASIRI-Maana yake ni uwezo alionao mtu wa kujiamini mbele za Mungu juu ya maisha yake yasiyo hukumiwa na dhambi moyoni mwake.

 1 Yohana 3:21 anasema hivi,,"Wapenzi, miiyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu"
Sasa jiulize swali hili pamoja na mimi, Ni nini kina hukumu moyoni? 
KUHUKUMIWA MOYONI"...kuna letwa na "DHAMBI" iliyo moyoni ambayo inapoteza UHODARI/UJASIRI wa mtu mbele za Mungu.

 Kama umepoteza "UJASIRI" ndani yako maana yake "UMETUPA UJASIRI" wako kwa kuruhusu dhambi iingie kwako, na madhara yake thawabu  unaipoteza ukiwa hapa hapa duniani.

Kama umepata "UJASIRI" wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, maana yake umefutiwa dhambi, na moyoni mwako umepewa

 "UZIMA WA MILELE" Sasa unaporuhusu dhambi unapoteza "UZIMA WA MILELE" uliyo ndani, na maandiko yanasema MNA UZIMA WA MILELE NINYI MNAOLIAMINI JINA LA MWANA WA MUNGU" (1 Yohana 5:13)

SABABU ZA KUTUNZA UJASIRI.
Ni kutufikisha katika Tumaini ambalo Bwana ametuandalia watoto wake .
Waesfeso 3:12 "Katika yeye tuna ujasiri na uwezo wa kukaribia tumaini kwa njia ya kumwamini"
Huwezi kulikaribia "TUMAINI" uliloliweka ndani ya Kristo kama huna "UJASIRI NA UWEZO" unaokupa wewe kutarajia unachokitarajia katika Kristo.

Hakikisha haupotezi "UJASIRI" wako usije ukashindwa kukaribia tumaini lako uliloliweka kwa Yesu. Maana ujasiri na uwezo ndivyo vinakutengezea mazingira ya kukutana jibu lako/yetu. Ujasiri na uwezo unavipata ukiwa ndani ya Yesu.
UJASIRI UNARUHUSU KUPEWA NEEMA NA KIBALI MBELE ZA MUNGU 
.
Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji"
Katika maneno hayo kuna..."KITI CHA NEEMA" na kuna....KUPEWA REHEMA..na pia kuna...KUPATA NEEMA. Kazi moja wapo ya kiti cha Neema ni sisi "TUPEWE REHEMA" kiingireza anasema,,, "GIVEN MERCY" Mercy inamaana ya "HURUMA"
Kwa maana hiyo kiti cha NEEMA kinatoa "HURUMA NA NEEMA" vinavyomsaidia mtu mwenye ujasiri ndani yake kutumia "NEEMA INAYOTOA MSAADA Msabato Neema hutoka kwa Mungu na Kwan njia y'all Neema tunapata kibali mbele Zach Mungu "
Kwa hiyo wakati wowote mahali popote anapohitaji msaada kutoka Kwa Mungu  night Neema yake Pelee ndio sababu yakupokea majawabu na mahitaji yako/yangu, maana kwa njia ya kristo tumepewa neema ya kupokea chochote tuombacho.

Maandiko yanasema hivi,,"Wapenzi, miiyo yetu isipotuhukumu tunaujasiri kwa Mungu, na lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa tumezishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake" (1 Yohana 3:21-22)

Ukiomba na hauna ujasiri ndani yako huwezi kupokea unachokiomba, kwa sababu "NEEMA" ya kukusaidia haipo
 kwa nini haipo?
Kwa sababu huna uwezo wa kusimama mbele za Bwana, maana dhambi hukosesha ujasiri na kibali cha kwenda mbele za Mungu, maana hukumu husimama mbele ya mwenye dhambi na kumwondolea ujasiri.

"TWAJUA YA KUWA MUNGU HAWASIKII WENYE DHAMBI; BALI MTU AKIWA MCHA MUNGU, NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE HUMSIKIA HUYO" (Yohana 9:31)
Hili neno tumejifunza leo Kama msingi wa maombi yetu kwa sababu sisi tumepata Neema ya kristo ambayo imetuokoa na hatuko na dhambi inayohukumu mioyo yetu maana Bwana amekwisha kutusamehe na huo ndio ujasiri tulio nao unatufanya kwenda mbele zake kupeleka mahitaji yetu.
Kwa uhakika huo tunaamini kila tukipelekacho kwa Mungu naamini tutapokea sawasawa na mapenzi take. 
Amen
Prepared by Moses 
Moses z Mgema 
0715366003
24/09/2021