Nimejifunza kanuni moja ya maisha ambayo, kama mtu anaye kusimulia alishafanikiwa na anakueleza wewe mtu ambae bado hujafikia ndoto na malengo yako kwenye maisha,ni ngumu sana kuelewa au kumwelewa mtu huyo, kwa sababu wakati mwingine, unaweza kuhisi anasema hivyo kwa sababu ana mali tayari.
▶️Ukweli ni kwamba kuna kuamua ni aina gani ya maisha ungependa kuishi na ukayaishi, kupenda kuishi maisha fulani ni tofauti na kutamani kuishi aina fulani ya maisha. Watu wote duniani tunatamani kuishi mazuri, ila katikati ya kutamani kuishi mazuri wengi wetu hatupendi kuishi maisha mazuri.
▶️Wengi wetu tunaongozwa na shauku na matamanio ila hatupendi maisha hayo, mwisho wa siku wengi wetu hatuyaishi matamanio yetu kwa sababu uvivu na kutokujituma ndiyo maisha ya watu wengi duniani tumeyachagua. Mtu yuko tayari kufanya kazi ya bei ya ajabu kïsa inampa pumziko la siku nzima, hatoki jasho, mtu yupo tayari kupokea dola tatu kwa siku hata kama anauwezo wakupiga hatua nakufanya kazi ambazo zinaonekana hazina hadhi lakini angalau zinakipato kizuri kuliko cha kivulini.
▶️Uvivu na kutokujituma kazini au katika kutimiza majukumu yetu sawasawa, inadhihirisha ni kwa kiwango gani tunapenda maisha duni na ya ufukara, ukipenda maisha mazuri utajituma na kufanya kazi kwa bïdii, kufanya kazi kwa bidii ni ishara ya kuyachukia maisha duni na umasikini ambayo ndiyo yamekithiri miongoni mwa vijana wengi hasa wakitanzania.
▶️Tumekaa kulalamika, kulaumu na kuwatwisha wengine lawama kama vyanzo vya maisha yetu kuwa yalivyo leo, umasikini wetu uko kwenye nguvu ya kuongea, na utajiri wetu uko kwenye nguvu yakufanya maamzi na kufanya utekelezaji wa vitendo. Kusema, kuongea na kuzungumza kwa wenye akili ni vyanzo vya fedha, ajira, biashara na utajiri, kwa mpumbavu ni dambo la lawama, majivuno, umbea, masengenyo na maneno bila utekelezaji wa vitendo, ni wazuri wa kunogesha mazungumzo na wavivu wakutekeleza yale wanayoyazungumza.
▶️Hatua za mwenye bidii huleta mavuno, hatua za mtu wa mipango ni utekelezaji na mipango humwonyesha utekelezaji na uwezekano wa kisichowezekana katika mitazamo ya wengi. Ukipenda kufanya kazi za kawaida jifunze kuwa mbunifu kwa sababu katika ule uzoelefu ukitiwa nakshi huja na matokeo chanya sana.
▶️Mtu tajiri akiandika ukweli mchungu, fukara na masikini huyachukulia maneno hayo kama matusi, dhihaka, majivuno, kiburi na dharau kwa wasio nacho, huu ni mtazamo wa watu masikini na fukara wa kuanzia ufahamu, kiroho na kimwili pia, bali maneno yenye kuchoma na kuumiza kwa sababu yanaweka wazi udhaifu na unalengo la kuponya, hujenga mtazamo chanya, na kuleta mapinduzi ya fikra ambayo pia huamsha hasira ya kupambana ili kuondokana na hali duni aliyo nayo mtu husika na huchukua hatua pia yakuanza.
▶️Nilichojifunza ni kwamba duniani hakuna fungu la kupata wala fungu la kukosa, bali aina ya maisha ninayoyataka yako ndani ya uwezo wangu wa kimtazamo, naona nini, natenda nini, nalenga wapi, nachukua hatua gani ni kwa kiwango gani nayachukia maisha duni kwa kiwango gani napenda maisha ya raha mstarehe.
▶️Aina ya maisha ninayotaka inaanzia kwenye fikra zangu, taarifa, maarifa ya aina gani napenda kuyatumia, aina ya watu nachangamana nao, marafiki pamoja na mazungumzo yao, uchaguzi wa mpenzi wa maisha, mumeo/mkeo, mpenzi/mchumba ni wa aina gani, Je ni mshikaji wako, rafiki yako, business/mfanyakazi mwenzako ambae una uhuru wakushikishana nae kwenye mipango na malengo ya familia yenu au mpo kutimiza majukumu ya ndoa yakiisha unarudi kwenye Ios au Adroid ya samsung na Tecno yako
▶️Kwa nini huyu ni rafiki yako au kwa nini cycle ya watu watu wako ni wainga fulani, unapata nini kupitia wao, mademu, umbea, utani kupindukia au mawazo gani, mazungumzo yenu hata kama hamjatoboa yakoje, umbea, starehe, mpira mchna kutwa,, kwenda kuchoma muda wote, ni aina gani ya watu umekubali wawe kampani yako.....
▶️Aina ya watu, marafiki, namna unavyowaza, mitazamo, aina ya mchumba au mke uliye nae ndiyo uhalisia wako wewe, na ndiyo picha yako wewe hasa ile ya ndani. Maisha ya mtu ni matokeo ya kile kilicho ndani ya mtu husika....
▶️Ni maneno mazito kiasi fulani, lakini ni elimu ambayo inamgusa kila mtu, mama, Baba, kaka dada na mimi mwenyewe. Kiufupi maisha yako ndani ya uwezo wangu/wako, ukiamua kuishi high class, middle class au lower class au lowest class. chambua aina ya watu wakutembea nao, badili fikra zako, kubali kuanza upya katika fikra zak
▶️Sijaoa, sijawa na maisha ninayotaka, yawezekana pia kampanh imara sana, ila aina watu wangu wa muhimu wanajulikana, mke wangu ni sio tu atakuja kuwa mke bali hata yeye anajua kuwa mimi ndiyo rafiki yake namba moja, mshikaji wangu.
Vijana tupambane, tujitathimini, tuache uvivu tufanye kazi kwa bidii, tusichague kazi, matatizo yako yasiwe sababu ya kuyatumia kama mtaji hapana, ziugeuze changamoto na shida zako kuwa mtaji, badiliko la fikra na mawazo yako kuwa furaha yako, fanya kazi kwa bidii, panga kuwa tajiri, chukia umasikini, penda utajiri.
Pambana hata kama huoni, giza limetanda kila mahali, usikate tamaa, alfajiri iko karibu sana, mapambazuko yamekaribia na jogoo anawika jua ng'ambo imefika. Katika yote hayo Mungu ni wa kwanza.
Mgema moses
Singida Tanzania