Umefika mahali umeyachukia maisha, umesikia maneno ya walimwengu kuwa riziki ni mafungu saba, umeyabeba nakuyakiri kwenye moyo wako na akili imepokea na kujenga picha kwamba wewe uko upande wa fungu la kukosa.
Umefika mahali juhudi za jana ambazo hazikukupa matokeo uliyotarajia zimekufanya uichukie jana na kuamini kuwa haiwezekani tena, Umekaa chini umesońoneka, huzuni imejaa moyoni, huoni tumaini tena wala mwanga na mwelekeo mpya wa kesho yako, umejiinamia kwa uchungu na uchovu mwisho umelia umechoka
Ushauri wangu kwako.............
Kesho yako usikubali iamuliwe na jana, jana imepita, ifanye kuwa darasa, ujifunze kuwa pamoja na juhudi yawezekana kuna mahalï nimekosea, au nilipatia ila kuna eneo nilïkuwa sifanyi kwa usahihi, fanya Tathimini yako binafsi, jikague kwa uaminifu baada ya evaluation yako ya uhakika, majibu utakayopata usiyapindishe, yakubali halafu yafanyie kazi.
Penye udhaifu wako kubali halafu aanza kupafanyia kazi, penye uimara wako jitahidi kuongeza jitihada mara dufu, jiboreshe zaidi.......
Baada ya hapo simama chukua hatua ya imani, anza upya kwa nguvu kubwa, ikanyage jana kawa jiwe la kuvukia mto, tembea mbele, tazama kesho kwa kujenga msingi imara leo.
Bora kesho msingi wake ni leo, jana imepita, haiwezi kufutwa ila inaweza kufanyiwa masahihisho leo, nakuleta matokeo tarajiwa kesho....
Wote tunapitia changamoto lakini tunakabiliana nazo kwa kuamini kiĺa jambo hutokea maisha for a reason not otherwise.
Moses zephania Mgema