Sunday, August 18, 2019

JE UNAISHI VILE ULITAKA KUWA HAPO KABLA..........?

..Vijana wengi tumekuwa na ndoto kubwa maishani, kila mtu ukimuuliza kuhusu maisha yake anakuambia nataka kuwa mtu Fulani hapo baadae.
Maisha haya yameanza tangu tukiwa watoto wadogo, ukiulizwa swali, jibu lake nataka kuwa daktari, Rubani, mwalimu, raisi nk. Haya ndiyo maisha na mfumo ambao mwanadamu ameumbwa nao, kuishi kwa kutamani kuwa mtu Fulani au kuwa sehemu fulani baada ya muda fulani kupita.
Pamoja na ndoto na malengo mengi tuliyonayo, changamoto kubwa imebaki katika kuyafikia yale tunayoyatamani au kuyaota, wengi tumefeli kuwa vile tulitaka kuwa na kuna sababu nyingi ambazo zinachangia kutokuishi maisha ya ndoto zetu  either kwa sababu za kimazingira, malezi, mifumo na mambo mengine kibao.

Pamoja na sababu nyingi ambazo zinaweza kuwa ndiyo sababu ya kutokufikia shauku na matanio ya mioyo yetu kuwa mahali fulani, lakini hizi ndizo sababu kubwa zinazowafanya watu wengi kutokutimiza malengo na ndoto zao.

1. Kutamka na kutenda kuna ombwe.
Wengi ni wazungumzaji ila sio watekelezaji wa kile wanachokizungumza na kukifikiri, unakuta mtu ana mipango mizuri lakini kufanyia kazi maono, ndoto, malengo, mipango na anachokizungumza ndiyo hapo changamoto inapoanzia.

2. Mipango mingi ambayo ni ngumu kutekelezeka.
Watu wengi wamekuwa wakiishi kwenye malengo mengi makubwa ambayo wakati mwingine ni makubwa na mengi ukilinganisha na uwezo wa mtu, mwisho wa siku anachopanga na anachotenda ni tofauti anakuwa confused na anaishindwa kujua aanze na lipi amalize na kipi au afanye jambo gani maana ana malengo mengi uwezo mdogo.

3. Watu wa sababu na lawama.
Watu wengi tunaishi kwenye kubebesha watu wengine mizigo ya lawama na kutengeneza sababu ambazo ni excuses zisizo na sababu za msingi sana mfano mtu unakuta ansema ningesoma, ningezaliwa sehemu fulani au nisingezaliwa kwenye umasikini, baba na mama wasingekufa mapema nk, lawama na malalamiko yasiyo na maana yamewafanya watu wengi kuishi maisha ambayo hawakuyatarajia kuyaishi hapo kabla.

4. Kupeperushwa na stori za vijiweni/kukosa msimamo wa kusimamia malengo na ndoto.
Watu wameshindwa kuishi maisha yenye mipango halisi ya maisha yao kwa sababu wamekuwa kama Bendera, akisikia stori Fulani ya kuvutia kuhusu mafanikio basi yuko tayari kuondoka kwenye malengo na mipango yake, mfano, mtu akisikia biashara Fulani inalipa, bila utafiti anaacha biashara yake na kuhamia huko, watu wengi wamekuwa ni watu wa kutanga tanga muda mwingi.

5.kutokutambua uwezo halisi/kutokujijua
Watu wengi hawajijui, hajui ana uwezo gani, hii inapelekea kufanya kila kitu kilichopo mbele yake. Kujitambua na kutambua uwezo wako ni moja ya nyenzo inayoweza kumfanya mtu akaishi kwenye ndoto na malengo yake.

6.Kutokutambua nyakati.
Kumbuka kwenye maisha kuna wakati wa kuandaa shamba, kulima, kupanda mbegu, kuota kwa mbegu, kumwagilia na kupalilia, kuweka  dawa, mazao kuanza kutoa matunda, hatimae matunda au mazao kukomaa. Wengi tunatamani kuanzia kwenye ukomavu wa matunda kwa sababu hatutaki kuchomwa na miba, jua, kunyeshewa mvua ila tunataka kula.

7.Hatukubali vile tulivyo.
Baadhi yetu huwa hatukubali kuwa tulivyo kwa wakati uliopo, hatupendi kuonekana uhalisia wetu kitu ambacho kimetufanya watu wengi kuishi kwa aibu na kuchagua kazi. Kumbuka kuna wakati unaenda mwanza ukitokea Dar unalazimika kupita  Kenya kwa sababu ya sababu za namna ulivyo, usilazimishe kula Serena hotel wakati uwezo wako ni kula kwa mama Ashura.

8.Elimu, Baba alikuwa Fulani.
Hadhi imewafanya watu wengi sana hasa vijana kuondoka kwenye malengo yao na ndoto hasa kwenye kipindi hiki ambacho ajira zimekuwa ngumu kupita Jana. Nikukumbushe kwamba ujenzi wa ndoto huanza na chochote ulichonacho. Mtu akitaka kuwa raisi, anaanza na levels za chini, diwani, au mbunge haya yote ni madaraja ya kutimiza malengo yake. Wakati mwingine sio straight Bali inamikunjo, milima na mambonde lakini haiondoi ukwel kwamba ndoto yako inatimia pale tu ubapokuwa na dhamira ya kweli toka moyoni.

9.Kutokufanya jambo ni kujipunguzia connections na firsa.
Fursa huja kwa namna ya ajabu sana, fursa sio kuwa na namba ya mtu fulani, sio kuwa karibu na viobgozi Bali wakati na mahali sahihi pakupata connection na fursa ni kile kidogo ulichoamua kukipa thamani, mfano kijana mwenye degree muuza genge la nyanya, matunda na mbogamboga anakutana na watu wangapi na wa aina gani kwa siku, je boda boda, huba driver nk. Je ni sawa na mkaaji ?.

Opportunities come where there is a beginning.
Hivyo basi hizi ni sababu na changamoto ambazo zimewafanya watu wengi na zinaendelea kuwatafuna watu wengi bila kujua, wengi wakiamini ipo siku watatoboa bila hata kuwa na chochote mkononi.

Moses Zephania Mgema
0715366003/0755632376
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam, Tanzania